MUISLAMU NA KUFANYA KAZI
Mwenyezi Mungu ameamrisha kutembea katika Ardhi kwa ajili ya kutafuta rizki na akahimiza kuhusu jambo hilo na hilo linadhihirika katika mambo yafwatayo :
1 Mwenyezi Mungu amekataza kuwaomba watu mali madamu Mwanadamu ana uwezo wa kufanya kazi na kupata riziki kwa juhudi zake na kazi yake, na Mtume ﷺ akaeleza yakawmba atakaewaomba watu mali na yeye ana uwezo wa kufanya kazi na kutafuta riziki basi yeye anapoteza hadhi yake mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya watu akasema Mtume ﷺ :
[لا تزال المسألة بأحدكم، حتى يلقى الله وليس في وجهه مزعة لحم] رواه البخاري ومسلم
[Hatoacha mmoja wenu kuomba mpaka akutane na mola wake mtukufu na hana katika uso wake nyama] [Imepokewa na Bukhary 1405 , Muslim 1040]
Na amesema Mtume ﷺ : [Atakaepatwa na matatizo basi akaiepeleka kwa watu matatizo yake hayatatimizwa na atakae yapeleka matatizo yake kwa ALLAH mtukufu basi ALLAH yuko karibu kumtajirisha] [Ahmad 3869 , Abu dawood 1645].
Kila kazi za halali ni kazi nzuri ambazo hazina aibu ndani yake .
Kila kazi za kutengeneza vitu na za huduma na za kuwekeza ni kazi nzuri zenye heshma hazina aibu ndani yake, madamu zipo ndani ya mpaka wa vitu halali , na imekuja katika sheria yakwamba Manabii walikua wakifanya kazi za halali za watu wao, kama alivyosema Mtume ﷺ :
[مَا بَعَثَ اللَّه نَبِيًّا إِلا رَعَى الْغَنَمَ] رواه البخاري
[Mwenyezi Mungu hajamtuma mtume isipokua amechunga mbuzi] [Imepokewa na Bukhary 2143] ,
Na alikua Nabii Zakariyya seremala [Muslim 2379]
Na hivyo hivyo Manabii wengine pia walikua wakifanya kazi kama hizo .
kwa hivyo Muislamu atakaekua na nia nzuri katika kazi yake, na anataka kujitimizia mahitaji yake na ya familia yake, na kuwatosheleza na kutowahitajia watu, na kuwanufaisha wanaohitaji , basi atapata ujira kwa ajili ya kazi yake na juhudi zake .
haya ndio Mafundisho ya Uislamu wala sio kama wengi wasio kuwa waislamu wanavyodi kuwa Uislamu ni Dini ya Uvivu.
Makala haya yameandikwa na
Muhammad Fadhil El Shirazy Al Kindy