MTU ATAFANYA NINI ATAKAPO KOSA MAWE YA KUJISAFISHIA?
Swali: Tumekataza kutumia mfupa au choo cha hayawani katika kujisafishia. Je mtu atakapo kosa Maji na kukosa mawe atafanya nini?
Jibu: Mtu atakapokosa Maji au mawe ya kujisafishia basi atatumia kile atakacho pata kama ni mfupa au hata kama ni choo cha myama. Kwa sababu baadhi ya Wanachuoni wanasema katazo la kutumia mfupa au choo si katazo la kuharamishwa bali ni katazo la karaha. Yaani ni makruhi mtu kutumia mfupa au choo lakini atakapo kosa cha kusafishia na kukawa hakuna kitu kingine basi atafaa kutumia ili kujisafishia ili apata kuswali na asipo pata kitu chochote basi afaa kutumia mkono wake kujisafishia kisha ausafishe mkono wake kwa mchanga kisha atayamamu na aswali kisha atakapo pata maji atajisafisha vizuri kwa neno lake Mtume (ﷺ).
الصعيد الطيب وضوء المسلم، وإن لم يجد الماء عشر سنين، وإذا وجد الماء فليمسه بشرته.] الحديث رواه أحمد في المسند]
[Mchanga msafi ni udhuu wa Muislamu hata asipo pata Maji miaka kumi,na atakapo pata Maji basi ayagusishe Ngozi yake] yaani awe ni mwenye kutumia maji kwa kujisafisha.
Hadihi imepokewa na Imam Ahmad katika Musnad yake.
Na Allah ndie Mjuzi zaidi.