0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MSINGI WA KWANZA: KUMJUA MOLA MLEZI

الأصول الثلاثة


الأصْلُ الأوَّلُ: مَعْرِفَةُ الرَّب

فَإِذَا قِيلَ لَكَ :مَنْ رَبُّكَ؟

فَقُلْ: رَبِّيَ اللهُ الَّذِي رَبَّانِي، وَرَبَّى جَمِيعَ الْعَالَمِينَ بِنِعَمِهِ، وَهُوَ مَعْبُودِي لَيْسَ لِي مَعْبُودٌ سِوَاهُ

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

{الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ}

وَكُلُّ مَنْ سِوَى اللهِ عَالَمٌ، وَأَنَا وَاحِدٌ مِنْ ذَلِكَ الْعَالَمِ

فَإِذَا قِيلَ لَكَ: بِمَ عَرَفْتَ رَبَّكَ؟

فَقُلْ: آيَاتِهِ وَمَخْلُوقَاتِهِ، وَمِنْ آيَاتِهِ: اللَّيْلُ، وَالنَّهَارُ، وَالشَّمْسُ، وَالْقَمَرُ، وَمِنْ مَخْلُوقَاتِهِ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالأَرَضُونَ السَّبْعُ وَمَنْ فِيهِنَّ، وَمَا بَيْنَهُمَا

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

{وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ}

وَقَوْلُهُ تَعَالَى:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

وَالرَّبُ هُوَ الْمَعْبُودُ

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ  الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ


Msingi Wa Kwanza: Kumjua Mola Mlezi:

Basi utakapoulizwa: “Nani Mola wako?”

Sema: “Mola wangu ni Mwenyezi Mungu Aliyenilea na Aliyewalea walimwengu wote kwa neema zake. Naye ndiye ninayemwabudu, na sina mwengine ninayemwabudu asie kuwa yeye.

Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

[Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote]  [Suurat al-Faatih’a:2]

Na kila kitu kisichokuwa Mwenyezi Mungu, ni kilichoumbwa nami ni mmojawapo katika kilichoumbwa.

Basi utakapoulizwa: “Umemjua vipi Mola wako?”

Sema: “Kutokana na Alama (ishara) zake na Viumbe vyake. Na miongoni mwa Alama zake ni: Usiku, Mchana, Jua, Mwezi. Na miongoni mwa viumbe vyake ni Mbingu saba na Ardhi saba, na kila kilichokuwemo ndani yake na baina yake”

Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu.]  [Suuratul Fuss’ilat: 37]

Na kauli yake Aliyetukuka:

[Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote]  [Suurat Al-A’raaf:54]

Na Mola mlezi ndiye Mwenye kuabudiwa

Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka.Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua.]   [Sura Al-Baqara: 21-22]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.