0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

50. MLANGO WA KUMWOGOPA ALLÂ (MWENYEZI MUNGU)

باب الخوف


قَالَ الله تَعَالَى: ﴿وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ﴾ [ البقرة: 40 ]

وَقالَ تَعَالَى: ﴿إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ﴾ [ البروج: 12 ]

وَقالَ تَعَالَى: ﴿وَكَذَلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَى وَهِيَ ظَالِمَةٌ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ إِنَّ فِي ذَلِكَ لآيَةً لِمَنْ خَافَ عَذَابَ الآخِرَةِ ذَلِكَ يَوْمٌ مَجْمُوعٌ لَهُ النَّاسُ وَذَلِكَ يَوْمٌ مَشْهُودٌ وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلاَّ لأَجَلٍ مَعْدُودٍ يَوْمَ يَأْتِ لا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلاَّ بِإِذْنِهِ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ﴾ [ هود: 102-106 ]

وَقالَ تَعَالَى: ﴿وَيُحَذِّرُكُمُ اللهُ نَفْسَهُ﴾ [ آل عمران: 28 ]

وَقالَ تَعَالَى: ﴿يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ لِكُلِّ امْرِئٍ مِنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ﴾ [ عبس: 34-37 ]

وَقالَ تَعَالَى: ﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ

ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَى وَمَا هُمْ بِسُكَارَى وَلَكِنَّ عَذَابَ اللهِ شَدِيدٌ﴾ [ الحج: 1-2 ]

وَقالَ تَعَالَى: ﴿وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ﴾ [ الرحمان: 46]

وَقالَ تَعَالَى: ﴿وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ يَتَسَاءلُونَ قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ، فَمَنَّ اللهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ إِنَّا كُنَّا مِنْ قَبْلُ نَدْعُوهُ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ﴾ [ الطور: 25-28 ]

وَالآيات في الباب كثيرة جداً معلومات والغرض الإشارة إِلَى بعضها وقد حصل

وأما الأحاديث فكثيرة جداً فنذكر مِنْهَا طرفاً وبالله التوفيق


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



MLANGO WA KUMWOGOPA ALLÂ (MWENYEZI MUNGU


Mwenyezi Mungu Amesema:

[Na Niogopeni Mimi tu.] [2: 40].

Mwenyezi Mungu Amesema:

[Hakika kutesa kwa Mola wako ni kukali (sana).]  [85: 12].

Mwenyezi Mungu Amesema:

[ Na namna hivi ndivyo inavyokuwa kutesa kwa Mola wako Anapowatesa (watu wa) miji wanapokuwa wameacha mwendo walioambiwa. Hakika teso Lake (Allâh) linaumiza (na) ni kali kabisa. Kwa yakini katika haya kuna mazingatio kwa yule anayeogopa adhabu ya Akhira. Hiyo ndiyo siku itakayokusanyiwa watu, na hiyo ndiyo siku itakayoshuhudiwa (na viumbe wote). Na Hatuiakhirishi ila kwa muda unaohisabiwa (na Mwenyewe Allâh; utakuja tu). Wakati itakapokuja (siku hiyo) kiumbe chochote hakitasema ila kwa ruhusa Yake (Allâh); basi baadhi yao watakuwa wenye hali mbaya (nao ni wale waasi) na (wengine) wenye hali nzuri (nao ni wale wema). Ama wale wenye hali mbaya (kwa sababu ya kufanya kwao mabaya), wao watakuwa motoni, humo wawe wanapiga makelele (ya kama milio ya punda) na kutoa kwikwi.]  [11: 102-106].

Mwenyezi Mungu Amesema:

[ Na Allâh Anawahadharisha Naye.] [3: 28].

Mwenyezi Mungu Amesema:

[ Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye. Na mamaye na babaye. Na mkewe na wanawe. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali itakayomtosha mwenyewe (hana haja ya mwenziwe).]  [80: 34-37].

Mwenyezi Mungu Amesema:

[ Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la Saa (ya Kiyama) ni jambo kuu. Siku mtapoiona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshaye, na kila mwenye mimba ataharibu mimba yake. Na utaona watu wamelewa, na kumbe hawakulewa. Lakini adhabu ya Allâh ni kali. ]  [22:1, 2].

Mwenyezi Mungu Amesema:

[Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake atapata mabustani (Pepo) mawili.] [55:46].

Mwenyezi Mungu Amesema:

[ Wataelekeana wakiulizana Waseme: Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa; Basi Allâh Akatufanyia hisani na Akatulinda na adhabu ya upepo wa Moto. Hakika sisi zamani tulikuwa tukimuomba Yeye tu. Hakika Yeye Ndiye Mwema Mwenye kurehemu.] [52:25-28].


Begin typing your search above and press return to search.