KITAAB AT-TAWHIID
باب (22) ما جاء أن بعض هذه الأمة تعبد الأوثان
وقوله تعالى: {أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيباً مِنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَؤُلاءِ أَهْدَى مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلاً} سورة النساء:51
وقوله تعالى: {قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُمْ بِشَرٍّ مِنْ ذَلِكَ مَثُوبَةً عِنْدَ اللَّهِ مَنْ لَعَنَهُ اللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ الْقِرَدَةَ وَالْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ الطَّاغُوتَ} سورة المائدة:60
وقوله تعالى: {قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَى أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِمْ مَسْجِداً} سورة الكهف:21
عن أبي سعيد رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: “لتتبعن سنن من كان قبلكم، حذو القذة بالقذة، حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه. قالوا: يا رسول الله، اليهود والنصارى؟ قال: فمن؟ “ 4 5 أخرجاه
ولمسلم عن ثوبان رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: “إن الله زوى لي الأرض، فرأيت مشارقها ومغاربها، وإن أمتي سيبلغ ملكها ما زوى لي منها. وأعطيت الكنْزين الأحمر والأبيض. وإني سألت ربي لأمتي أن لا يهلكها بسنة بعامة، وأن لا يسلط عليهم عدوا من سوى أنفسهم فيستبيح بيضتهم؛ وإن ربي قال: يا محمد، إذا قضيت قضاء فإنه لا يرد، وإني أعطيتك لأمتك أن لا أهلكهم بسنة عامة، وأن لا أسلط عليهم عدوا من سوى أنفسهم فيستبيح بيضتهم ولو اجتمع عليهم من بأقطارها، حتى يكون بعضهم يهلك بعضا ويسبي بعضهم بعضا” ورواه البرقاني في صحيحه
وزاد: “وإنما أخاف على أمتي الأئمة المضلين الساعة حتى يلحق حي من أمتي بالمشركين، وحتى تعبد فئام من أمتي الأوثان، وإذا وقع عليهم السيف لم يرفع إلى يوم القيامة. ولا تقوم. وإنه سيكون في أمتي كذابون ثلاثون؛ كلهم يزعم أنه نبي، وأنا خاتم النبيين لا نبي بعدي. ولا تزال طائفة من أمتي على الحق منصورة لا يضرهم من خذلهم حتى يأتي أمر الله تبارك وتعالى
:فيه مسائل
الأولى: تفسير آية النساء
الثانية: تفسير آية المائدة
الثالثة: تفسير آية الكهف.الرابعة: وهي أهمها: ما معنى الإيمان بالجبت والطاغوت؟ هل هو اعتقاد قلب، أو هو موافقة أصحابها مع بغضها ومعرفه بطلانها؟
الخامسة: قولهم: إن الكفار الذين يعرفون كفرهم أهدى سبيلا من المؤمنين
السادسة: وهي المقصودة بالترجمة: أن هذا لا بد أن يوجد في هذه الأمة، كما تقرر في حديث أبي سعيد
السابعة: التصريح بوقوعها، أعني عبادة الأوثان في هذه الأمة في جموع كثيرة
الثامنة: العجب العجاب: خروج من يدعي النبوة، مثل المختار، مع تكلمه بالشهادتين، وتصريحه بأنه من هذه الأمة، وأن الرسول حق، وأن القرآن حق. وفيه: أن محمدا خاتم النبيين، ومع هذا يصدق في هذا كله مع التضاد الواضح، وقد خرج المختار في آخر عصر الصحابة، وتبعه فئام كثيرة
التاسعة: البشارة بأن الحق لا يزول بالكلية كما زال فيما مضى، بل لا تزال عليه طائفة
العاشرة: الآية العظمى: أنهم مع قلتهم لا يضرهم من خذلهم ولا من خالفهم
الحادية عشرة: أن ذلك الشرط إلى قيام الساعة
الثانية عشرة: ما فيهن من الآيات العظيمة.منها: إخباره بأن الله زوى له المشارق والمغارب، وأخبر بمعنى ذلك، فوقع كما أخبر، بخلاف الجنوب والشمال. وإخباره بأنه أعطي الكنْزين. وإخباره بإجابة دعوته لأمته في الاثنتين. وإخباره بأنه مُنع الثالثة. وإخباره بوقوع السيف، وأنه لا يرفع إذا وقع. وإخباره بظهور المتنبئين في هذه الأمة. وإخباره ببقاء الطائفة المنصورة. وكل هذا وقع كما أخبر، مع أن كل واحدة منها من أبعد ما يكون في العقول 1
الثالثة عشرة: حصر الخوف على أمته من الأئمة المضلين
الرابعة عشرة: التنبيه على معنى عبادة الأوثان
MLANGO WA 22 YALIYOKUJA KUBAINISHA YA KUWA BAADHI YA UMMA HUU WATAABUDU MASANAMU
Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Huwaoni wale walio pewa sehemu ya Kitabu? Wanaamini masanamu na Shet’ani!] [An-Nisaa (5: 51)]
Na kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Sema: Je! Nikwambieni yule ambaye ni mwenye malipo mabaya zaidi kuliko hayo mbele ya Mwenyezi Mungu? Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani na amemkasirikia, na amewafanya miongoni mwao manyani na nguruwe, na wakamuabudu Shet’ani.] [Al-Maidah: 60)]
Na kauli Yake Aliyetukuka:
[Wakasema walio shinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutawajengea msikiti juu yao.] [Al-Kahf (18: 21)]
Imepokelewa kutoka kwa kwa Abuu Sa’iyd (Radhi zaAllah ziwe juu yake) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema: [Bila shaka mtafuata nyendo za watu waliokuwa kabla yenu, hatua kwa hatua hata wakiingia kwenye shimo la kenge nanyi mtaingia]. Wakasema: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara?” Akasema: [Nani basi [kama si hao]?] [Imepokewa na Bukhaariy na Muslim]
Na Muslim Imepokelewa kutoka kwa Thawbaan radhi za Allah ziwe juu yake , yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema : [Hakika Mwenyezi Mungu alinikusanyia ardhi na kunionesha, basi nikaona mashariki yake na magharibi yake, na kwa hakika Umma wangu Ufalme wake utafika mpaka yale niliyokusanyiwa na kuoneshwa katika ardhi, na nilipewa hazina mbili nyekundu na nyeupe, na kwa hakika mimi nilimuomba Mola wangu kwa Umma wangu asiwaangamize kwa adhabu ya pamoja au ukame utakao enea kote, na asiwasalitishie adui asiye kua wao, basi akawaangamiza wote , na kwa hakika Mola wangu amesema : Ewe Muhammad , hakika Mimi nikihukumu na kupitisha jambo basi halirudishwi , na kwa hakika Mimi nimekupa kwa ajili ya Umma wako yakwamba sitowaangamiza kwa ukame utakao enea , na sitowasalitishia adui asiye kua wao akawaangamiza , hata kama watakusanyika kwa ajili ya kuwapiga vita kutoka pembe mbali mbali za ulimwengu mpaka itakapokua wanaangamizana na kupigana wao kwa wao na wanashikana mateka wao kwa wao] [Imepokewa na Muslim]
Na Al-Barqaaniyy katika Swahiyh yake akaongezea yafuatayo: [Bali ninachokikhofia kwa Umma wangu ni kupotezwa na viongozi wapotofu ambao wakiangukiwa na upanga, upanga huo hautonyanyuliwa hadi Siku ya Qiyama. Wala Qiyaamah hakitafika mpaka baadhi ya Ummah wangu wawafuate makafiri na waanze kuabudu masanamu. Nawakhofia watakuja miongoni mwao manabii wa uongo thelathini; kila mmoja anadai kuwa yeye ni nabiy na hali mimi ni Nabiy wa mwisho hakuna baada yangu. Lakini kundi moja katika ummah wangu litabakia kuwa katika haki na ushindi, hlitodhurika kwa kuanguka kwa wengine mpaka ifike amri ya Allaah Tabaraka wa Ta’aalaa] [Imepokewa na Al-Barqaaniy fiy Swahiyhih]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1. Tafsiri ya Aya katika Sura An-Nisaa (4: 5).
2. Tafsiri ya Aya katika Sura Al-Maaidah (5: 60).
3. Tafsiri ya Aya katika Sura Al-Kahf (18: 21).
4. Jambo muhimu kabisa kuhusu maana ya Al-jibt na Atw-Twaaghuwt katika maudhui hii. Je, ni kuitakidi kwa moyo, au kukubaliana tu na wale wanaofanya (shirki) na hali wanachukia na kujua kwamba ni upotofu?
5. Mayahudi kudai kwamba (Makafiri Quraysh) wanaotambua hakika ya kufru yao kwamba wako katika uongofu zaidi kuliko Waumini.
6. Watu kama hao (watakaopotea na kuabudu masanamu) wanapatikana katika Ummah huu wa Kiislamu kama ilivyotajwa katika Hadiyth ya Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhi za Allah ziwe juu yake ). Hii ndio maudhui kuu ya mlango huu.
7. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ kueleza wazi kwamba wengi katika Ummah wake wataabudu waabudiwa wa uongo (masanamu n.k.).
8. La ajabu zaidi ni kutokeza kwa wale wanaodai unabiy kama Al-Mukhtaar[1] juu ya kuwa alikiri shahaadah na kukiri kwake kwamba ni miongoni mwa Ummah wa Kiislamu, na (kukiri kwake) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ ni haki na Qur’ani ni haki, na kukiri kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ ni Nabiy wa mwisho. Lakini inashangaza kwamba muongo kama huyo anajidai unabiy na huku anaaminiwa juu ya kudhihirika kwake kupinga shahaadah yake. Al-Mukhtaar alitokeza katika kipindi cha mwisho wa Maswahaba na akapata wafuasi wengi.
9. Bishara njema kwamba haki haitopotea moja kwa moja kama zamani, bali litabaki kundi moja litakalobakia katika haki.
10. Alama kubwa kabisa ni kwamba wao (kundi la haki) hawatodhuriwa na waliowakhalifu wala wapinzani japokuwa wao watakuwa wachache.
11. Hali hiyo ndivyo itakavyokuwa hadi Qiyama.