0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MLANGO WA 20 MAKATAZO YA LIOKUA YA KUVUKA MIPAKA KWA MAKABURI YA WATU WEMA

KITAAB AT-TAWHIID

باب (20) ما جاء أن الغلو في قبور الصالحين يصيرها أوثانا تعبد من دون الله

روى مالك في الموطأ: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: “اللهم لا تجعل قبري وثنا يُعبد. اشتد غضب الله على قوم اتخذوا قبور أنبيائهم مساجد” 1. ولابن جرير بسنده عن سفيان عن منصور عن مجاهد {أَفَرَأَيْتُمُ اللاَّتَ وَالْعُزَّى} قال: “كان يلت لهم السويق فمات، فعكفوا على قبره”.

وكذا قال أبو الجوزاء عن ابن عباس: “كان يلت السويق للحاج”. وعن ابن عباس رضي الله عنهما قال: “لعن رسول الله صلى الله عليه وسلم زائرات القبور، والمتخذين عليها المساجد والسرج” 2 رواه أهل السنن

:فيه مسائل

الأولى:  تفسير الأوثان
الثانية:  تفسير العبادة

الثالثة:  أنه صلى الله عليه وسلم لم يستعذ إلا مما يخاف وقوعه

الرابعة:  قرنه بهذا اتخاذ قبور الأنبياء مساجد

الخامسة:  ذكر شدة الغضب من الله

السادسة:  وهي من أهمها: صفة معرفة عبادة اللات التي هي من أكبر الأوثان

السابعة:  معرفة أنه قبر رجل صالح

الثامنة:   أنه اسم صاحب القبر، وذكر معنى التسمية

التاسعة:  لعنه زوارات القبور

العاشرة لعنه من أسرجها

MLANGO WA 19 KUTILIWA MKAZO HARAMISHO LA KUMUABUDU MWENYEZI MUNGU KWENYE KABURI LA MTUM MWEMA BASI AKIMUABUDU ALIE KABURINI?

Amepokea Imaam Maalik katika Al-Muwattwaa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: [Ewe Mwenyezi mungu! Usijaalie kaburi langu kuwa Sanamu la kuabudiwa. Hasira za Mwenyezi Mungu zimezidi kwa watu wanaofanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti] [Maalik fiyl Muwattwaa]

na Ibn Jariyr (Atw-Twabariy) amepokea kwa isnaad yake, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Mujaahid kuhusu Ayah: hii [Je, mmeona Laata na ‘Uzzaa?] [An-Najm (53: 19)] Amesema: “(Laata) Alikuwa akiwahudumia mahujaji sawiyq. Baada ya kufa kwake, watu wakaanza kukaa itikafu  kwenye kaburi lake”

Na Hadiyth hiyo imesimuliwa na Abu Al-Jawzaai kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema pia: “Alikuwa akiwakaribisha sawiyq kwa mahujaji.”

Imepokelewa toka kwa Ibn Abbaas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: [Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amewalaani wanawake wanaozuru makaburi, na wanaojenga Misikiti kwenye makaburi na kuyawashia taa makaburi] [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Ufafanuzi kuhusu ‘awthaan’ (masanamu).

2. Ufafanuzi kuhusu ‘ibaadah.

3. Kwamba Mtume   haombi kinga kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa jambo alichokhofia kutokea.

4. Mtume kuambatanisha kwake du’aa: ((Ee Allaah! Usijaalie kaburi langu…)) pamoja na (kukhofia khatari ya) ((watu wanaofanya makaburi ya Manabii kuwa Misikiti)).

5. Kutajwa ghadhabu kali za Mwenyezi Mungu (kwa anayefanya kitendo hicho).

6, La muhimu kabisa ni maelezo kuhusu ‘ibaadah ya Laata ilivyoanza, nalo ni sanamu kuu kabisa kabla ya Uislamu.

7. Asili ya Laata lilikuwa ni kaburi la mja mwema.

8. Laata ni jina la mtu aliyezikwa katika kaburi hilo na ndio maana sanamu hilo likaitwa hivyo.

9. Laana (ya Mtume ﷺ) kwa wanawake wanozuru makaburi.

10. Laana (ya Mtume ﷺ) kwa wanaoweka taa kwenye makaburi.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.