0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MLANGO WA 14 NENO LA MWENYEZI MUNGU: {ATI WANAWAFANYA VIUMBE KUWA KUWA NI WASHIRIKINA WA MWENYEZI MUNGU, NAO HAWAUMBI, BALI WAO NDIO WANAUMBWA? WALA HAWANA UWEZO WA KUWANUSURU WALA WENYEWE HAWAJINUSURU}

KITAAB AT-TAWHIID

باب (14) قول الله تعالى: {أََيُشْرِكُونَ مَا لا يَخْلُقُ شَيْئاً وَهُمْ يُخْلَقُونَ وَلا يَسْتَطِيعُونَ لَهُمْ نَصْراً وَلا أَنْفُسَهُمْ يَنْصُرُونَ

وقوله: {وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِنْ قِطْمِيرٍ إِنْ تَدْعُوهُمْ لا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ وَلا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ}     فاطر:14
وفي الصحيح عن أنس، قال: “شُج النبي صلى الله عليه وسلم يوم أحد، وكسرت رباعيته، فقال: كيف يفلح قوم شجوا نبيهم؟ فنَزلت: {لَيْسَ لَكَ مِنَ الأَمْرِ شَيْءٌ} 

وفيه: “عن ابن عمررضي الله عنهما أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول إذا رفع رأسه من الركوع في الركعة الأخيرة من الفجر: اللهم العن فلانا وفلانا، بعد ما يقول سمع الله لمن حمده ربنا ولك الحمد، فأنزل الله: {لَيْسَ لَكَ مِنَ الأَمْرِ شَيْءٌ} ” الآية
وفي رواية: “يدعو على صفوان بن أمية، وسهل بن عمرو، والحارث بن هشام، فنَزلت: {لَيْسَ لَكَ مِنَ الأَمْرِ شَيْءٌ} آل عمران:128 ”
وفيه عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: “قام رسول الله صلى الله عليه وسلم حين أنزل عليه: {وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الأَقْرَبِينَ} 1 فقال: يا معشر قريش – أو كلمة نحوها – اشتروا أنفسكم، لا أغني عنكم من الله شيئا. يا عباس بن عبد المطلب، لا أغني عنك من الله شيئا. يا صفية عمة رسول الله صلى الله عليه وسلم، لا أغني عنك من الله شيئا. ويا فاطمة بنت محمد، سليني من مالي ما شئت، لا أغني عنك من الله شيئا”
فيه مسائل:
الأولى: تفسير الآيتين

الثانية: قصة أحد

الثالثة: قنوت سيد المرسلين، وخلفه سادات الأولياء يؤمِّنون في الصلاة

الرابعة: أن المدعو عليهم كفار
الخامسة: أنهم فعلوا أشياء ما فعلها غالب الكفار، منها: شجهم نبيهم، وحرصهم على قتله. ومنها: التمثيل بالقتلى، مع أنهم بنو عمهم
السادسة: أنزل الله عليه في ذلك: {لَيْسَ لَكَ مِنَ الأَمْرِ شَيْءٌ}   آل عمران:128

السابعة: قوله: {أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ} ، فتاب عليهم فآمنوا

الثامنة: القنوت في النوازل

التاسعة: تسمية المدعو عليهم في الصلاة بأسمائهم وأسماء آبائهم

العاشرة: لعن المعيَّن في القنوت

الحادية عشرة: قصته صلى الله عليه وسلم لما أنزل عليه: {وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الأَقْرَبِينَ} 1

الثانية عشرة: جده صلى الله عليه وسلم ، بحيث فعل ما نسب بسببه إلى الجنون، وكذلك لو يفعله مسلم الآن

الثالثة عشرة: قوله  للأبعد والأقرب: “لا أغني عنك من الله شيئا” حتى قال: “يا فاطمة بنت محمد، لا أغني عنك من الله شيئا” . فإذا صرح وهو سيد المرسلين بأنه لا يغني شيئا عن سيدة نساء العالمين، وآمن الإنسان أنه صلى الله عليه وسلم لا يقول إلا الحق، ثم نظر فيما وقع في قلوب خواص الناس اليوم، تبين له التوحيد وغربة الدين

MLANGO WA 14 NENO LA MWENYEZI MUNGU: {ATI WANAWAFANYA VIUMBE KUWA KUWA NI WASHIRIKINA WA MWENYEZI MUNGU, NAO HAWAUMBI, BALI WAO NDIO WANAUMBWA? WALA HAWANA UWEZO WA KUWANUSURU WALA WENYEWE HAWAJINUSURU}

Na kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakaye kupa khabari vilivyo kama Yeye Mwenye khabari.]   [Faatir: 14]

Na katika Swahih (Al Bukhari) Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake)  amesema: Alijeruhiwa Mtume ﷺ Siku ya vita vya Uhud meno yake yakavunjika. Akasema: [Vipi Watafaulu watu wanaomjeruhi Mtume wao] Ikateremka Aya : [Wewe huna lako jambo katika haya]   [Al-‘Imran: 128]

Na Imenukuliwa humo (katika sahihi Al Bukhari) kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba yeye alimsikia Mtume ﷺ alipoinua kichwa baada ya kurukuu katika rakaa ya mwisho kwenye Swala ya Alfajiri: [Ewe Mola mlaani fulani na fulani] Mwenyezi Mungu Akateremsha: [Wewe huna lako jambo katika haya]   [Al-‘Imran: 128]

Na katika Riwaya: Akiwaapiza Swafwaan bin Umayyah, Suhayl bin ‘Amr na Al-Haarith bin Hishaam, ikateremka: [Wewe huna lako jambo katika haya]   [Al-‘Imran: 128].

Na Imenukuliwa humo kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: alisimama Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ ilipoteremshwa [Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.] [Ash-Shu’araa: 214]. Akasema: [Enyi hadhara ya Quraysh)) – au maneno kama hayo – [Nunueni nafsi zenu, kwani sitowafaeni chochote mbele ya Mwenyezi Mungu!  Ee ‘Abbaas bin ‘Abdil-Muttwalib! Sitokufaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu!  Ee Swafiyyah shangazi yake Mtume wa Mwenyezi Mungu! Sitokufaa  chochote mbele ya Mwenyezi Mungu! Ee Faatima bint Muhammad! Niombe mali utakayo, [lakini] sitokufaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu]    [Imepokewa na Bukhari, Muslim]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Tafsiri za Aya mbili: (Al-Araaf :191-192 na Fatir:13-14)

2. Kisa cha Uhud.

3. Qunuti ya mbora wa Mitume katika Swalaa ikiitikiwa Amin na Mawalii watukufu nyuma yake (Maswahaba)

4. Wale walioapizwa, ni miongoni mwa makafiri.

5. Maquraysh walifanya mambo ambayo makafiri wengi hawakuyafanya, miongoni mwa hayo Kumpiga na kumpasua Mtume wao, na kuazimia kumuua, na miongoni mwa hayo kuikatakata miili ya waliouawa (katika Waislamu) japokuwa walikuwa ni banu ‘Ammi zao.

6. Mwenyezi Mungu alimteremishia Mtume wake juu hilo [Wewe huna lako jambo katika haya]   [Al-‘Imran: 128].

7. Neno lake Mwenyezi Mungu: [Ama atawahurumia au atawaadhibu,]    Akawakubalia Toba yao wakaamini

8. Kufaa kuQuniti wakati wa Majanga.

9. Kufaa kuwapiza watu kwa mjiana yao na majina ya babazao katika Swala.

10. Kufaa kulani mtu fulani katika Qunuti

11. Kisa cha Mtume alipoteremshiwa juu yake [Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.]

12. Uzito wa jambo hili kwamba Mtume ﷺ (alifanya bidii kutekeleza da’wah hadi) kufikia kuitwa mwendawazimu na ndivyo hali itakavyokuwa kwa Muislamu yeyote atakapofanya hivyo leo..

13. Mtume ﷺ aliwatangazia nduguze wote wa karibu na wa mbali: [Sitowafaeni chochote mbele ya Mwenyezi Mumgu!)) Hata alisema: ((Ewe Fatwima bint Muhammad, sitokufaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu]

Ikiwa mbora wa Miteme kaliweka wazi hilo, kwamba hatoweza kumfaa chochote mbora wa wanawake duniani (binti yake Faatima) na mtu akaamini kwamba Mtume ﷺ hasemi ila haki, kisha tazama yanayotokeza katika nyoyo za watu leo (kupendelea jamaa zao), hapo itadhihirika kwako suala la Tawhiyd na Kushangaza kwa dini!

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.