0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MLANGO WA 04 WITO WA KUSHUHUDIA YA KWAMBA HAPANA MOLA APASAE KUABUDIWA KWA HAKI ILA MWENYEZI MUNGU

KITAAB AT-TAWHIID

باب الدعاء إلى شهادة أن لا إله إلا الله

وقوله تعالى: {قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ}
عن ابن عباس رضي الله عنهما: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم لما بعث معاذا إلى اليمن قال له: [إنك تأتي قوما من أهل الكتاب، فليكن أول ما تدعوهم إليه شهادة أن لا إله إلا الله]
– وفي رواية: [إلى أن يوحدوا الله. فإن هم أطاعوك لذلك فأعلمهم أن الله افترض عليهم خمس صلوات في كل يوم وليلة. فإن هم أطاعوك لذلك فأعلمهم أن الله افترض عليهم صدقة تؤخذ من أغنيائهم فترد على فقرائهم. فإن هم أطاعوك لذلك فإياك وكرائم أموالهم. واتق دعوة المظلوم فإنه ليس بينها وبين الله حجاب]    أخرجاه
ولهما عن سهل بن سعد رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال يوم خيبر: [لأعطين الراية غدا رجلا يحب اللهورسوله ويحبه الله ورسوله، يفتح الله على يديه.] فبات الناس يدوكون ليلتهم أيهم يعطاها فلما أصبحوا غدوا على رسول الله صلى الله عليه وسلم كلهم يرجو أن يعطاها: فقال: [أين علي بن أبي طالب؟]  فقيل: هو يشتكي عينيه. فأرسلوا إليه فأتي به، فبصق في عينيه ; ودعا له فبرأ كأن لم يكن به وجع. فأعطاه الراية فقال:[ انفذ على رسلك حتى تنزل بساحتهم، ثم ادعهم إلى الإسلام وأخبرهم بما يجب عليهم من حق الله تعالى فيه
فوالله لأن يهدي الله بك رجلا واحدا خير لك من حمر النعم]

يدوكون أي: يخوضون 

فيه مسائل:

الأولى: أن الدعوة إلى الله طريق من اتبع رسول الله صلى الله عليه وسلم
الثانية: التنبيه على الإخلاص، لأن كثيرا لو دعا إلى الحق، فهو يدعو إلى نفسه
الثالثة: أن البصيرة من الفرائض
الرابعة: من دلائل حسن التوحيد: أنه تنْزيه الله تعالى عن المسبة
الخامسة: أن من قبح الشرك كونه مسبة لله
السادسة: وهي من أهمها – إبعاد المسلم عن المشركين لئلا يصير منهم، ولو لم يشرك
السابعة: كون التوحيد أول واجب.الثامنة: أنه يبدأ به قبل كل شيء، حتى الصلاة
التاسعة: أن معنى: “أن يوحدوا الله” معنى شهادة أن لا إله إلا الله
العاشرة: أن الإنسان قد يكون من أهل الكتاب وهو لا يعرفها، أو يعرفها ولا يعمل بها
الحادية عشرة: التنبيه على التعليم بالتدريج
الثانية عشرة: البداءة بالأهم فالأهم
الثالثة عشرة: مصرف الزكاة
الرابعة عشرة: كشف العالم الشبهة عن المتعلم
الخامسة عشرة: النهي عن كرائم الأموال
السادسة عشرة: اتقاء دعوة المظلوم
السابعة عشرة: الإخبار بأنها لا تحجب
الثامنة عشرة: من أدلة التوحيد ما جرى على سيد المرسلين وسادات الأولياء من المشقة والجوع والوباء
التاسعة عشرة: قوله: [لأعطين الراية … إلخ] علم من أعلام النبوة
العشرون: تفله في عينيه علم من أعلامها أيضا
الحادية والعشرون: فضيلة علي رضي الله عنه
الثانية والعشرون: فضل الصحابة في دوكهم تلك الليلة وشغلهم عن بشارة الفتح.الثالثة والعشرون: الإيمان بالقدر، لحصولها لمن لم يسع لها، ومنعها عمن سعى
الرابعة والعشرون: الأدب في قوله:[على رسلك
الخامسة والعشرون: الدعوة إلى الله إلى الإسلام قبل القتال
السادسة والعشرون: أنه مشروع لمن دُعوا قبل ذلك وقوتلوا
السابعة والعشرون: الدعوة بالحكمة لقوله: “أخبرهم بما يجب
الثامنة والعشرون: المعرفة بحق الله في الإسلام
التاسعة والعشرون: ثواب من اهتدى على يديه رجل واحد
الثلاثون: الحلف على الفتيا

MLANGO WA WITO WA KUSHUHUDIA YA KWAMBA HAPANA MOLA APASAE KUABUDIWA KWA HAKI ILA MWENYEZI MUNGU

Na kauli Yake Ta’aalaa:

[Sema: Hii ndiyo Njia yangu – ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua – mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.]  [Yusuf:108]

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhi za Allah ziwe juu yake): kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Alipomtuma Mu’aadh Yemen alimwambia: [Hakika wewe utakutana na watu miongoni mwa Ahlul-Kitaab, basi jambo la kwanza la kuwalingania liwe ni kushuhudia kwamba: Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu]

Na katika riwaya nyingine: [Walinganie] Kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Watakapokutii hilo, wajulishe kwamba Mwenyezi Mungu Amewafaradhishia Swala tano usiku na mchana. Watakapokutii hilo, basi wajuilshe kwamba Mwenyezi Mungu Amewafaradhishia Zaka iichukuliwe kutoka kwa matajiri wao na kupewa masikini wao. Watakapotii hilo, basi tahadhari na kuchukua bora za mali zao, na tahadhari na Du’a ya aliyedhulumiwa, kwani hakuna kizuizi baina yake na Mwenyezi Mungu]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na kutoka kwao wawili (Bukhari na Muslim: Imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Sa’d (Radhi za Allah ziwe juu yake ) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema siku ya Khaybar: [Kesho nitamkabidhi bendera mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda. Mwenyezi Mungu Atampa ushindi kupitia mikononi mwake]. Watu wakakesha usiku wakishughulika kujadili nani atakayepewa bendera. Asubuhi walimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ kwa hamu wakitegemea kupewa bendera. Mtume ﷺ akauliza: [Yuko wapi ‘Ali bin Abiy Twaalib?]. Wakajibu: Anauguwa macho yake mawili. Akaagizwa akafika. Mtume ﷺ akamtufia kwenye macho yake kisha akamwombea akapona kana kwamba hakuwa na maumivu yoyote. Mtume ﷺ akampa bendera akamwambia: [Waendee kwa taratibu na upole mpaka ufikie katikati yao, kisha waite katika Uislamu na wajulishe wajibu wao katika haki ya Mwenyezi Mungu. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu Akimuongoa mtu mmoja katika Uislamu kupitia kwako, basi ni bora kuliko ngamia wekundu]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1- Kulingania kwa Mwenyezi Mungu ﷻ ni miongoni mwa njia za kumfuata Mtume wa Mwenyezi mungu .

2- Kutanabahisha juu ya ikhlas kwa kuwa watu wengi wajidai kulingania katika haki lakini ni kwa ajili ya maslahi ya nafsi zao.

3– Kulingania kwa ‘Baswiyraa’ (utambuzi,) ni faradhi mojawapo.

4- Miongoni mwa dalili za uzuri wa Tawhiy ni kumtakasa Mwenyezi Mungu ﷻ  na kila aibu na kasoro.

5- Uovu wa shirk (kumshiikisha Mungu) ni kumtukana Mwenyezi Mungu ﷻ (kwa kumnasibisha na yasiyomstahiki.)

6- Nalo ndilo muhimu zaidi ni kumuepusha Muislamu na watu wa shirki ili asiwe kama wao, hata kama yeye hashirikishi.

7- Ya kwamba Tawhid (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ndio wajibu wa kwanza kabisa.

8- Ni kwamba Ataanza na Tawhid kabla ya kila kitu, hata Swala.

9- Kwamba Maana ya “Wampwekeshe Mwenyezi Mungu” ni sawa na maana ya kushuhudia ya kwamba Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu.

10- Huenda mtu akawa ni miongoni mwa Ahlul-Kitaab na asijue maana ya Tawhid au kuitekeleza. Au anaweza kuwa anajua, lakini matendo yake yakawa kinyume.

11- Kutanabahisha juu ya kufundisha kwa utaratibu maalumu (jambo moja baada ya jingine.

12- Kuanza kufundisha mambo muhimu zaidi kisha linalofuatia kwa umuhimu.

13- Wanaostahiki kupewa Zaka.

14- Mwalimu amuondoshee utata Mwanafunzi.

15- Makatazo kwa (Wakusanyaji wa Zaka) wasichukue mali zilizo bora kabisa za watu.

16- Kuogopa Du’a ya aliyedhulumiwa.

17- Maelezo kuwa Du’a ya aliyedhulumiwa haina kizuizi baina yake na Mwenyezi Mungu.

18- Miongoni mwa dalili za Tawhid ni yalio mjiria mbora wa Mitume na mbora wa Mawalii miongoni mwa Shida, njaa na magonjwa.

19- Kauli yake, (Mtume ﷺ) [Nitampa bendera …] ni alama ya Unabii.

20- Kumtufia (Ali Radhi za Allah ziwe juu yake) pia ni alama miongoni mwa ala ya Unabiy.

21- Ubora wa ‘Ali (Radhi za Allah ziwe juu yake).

22- Ubora wa Maswahaba kuwa walikesha usiku wakiwazia (nani atakayepewa bendera) na kisha kushughulishwa kwao na bishara ya ushindi wa mji.

23- Kuamini Qadari kwa kuwa hiyo (yaani bendera) alipewa mtu ambaye hakuitaraji au kuiomba, na wakanyimwa walioitaraji.

24- Adabu katika kauli yake Mtume ﷺ, [Waendee kwa taratibu na upole…].

25- Kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kuwalingania katika Uislamu kabla ya vita.

26- Ruhusa ya kupigana na waliolinganiwa Uislamu lakini wakakataa.

27– Kulingania kwa hekima kama alivyosema Mtume ﷺ: [… na wajulishe ya wajibu wao].

28- Kujua haki za Mwenyzi Mungu ﷻ katika Uislamu.

29- Thawabu za mtu moja aliyeongoka kupitia mikononi mwake.

30- Kuapa (kwa jina la Mwenyezi Mungu) juu ya Fatwa (kwa kuisapoti).

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.