KITAAB AT-TAWHIID
باب من حقق التوحيد دخل الجنة بغير حساب
وقول الله تعالى:
{إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِلّهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ}
وقال: {وَالَّذِينَ هُم بِرَبِّهِمْ لَا يُشْرِكُون}
عن حصين بن عبد الرحمن قال: كنت عند سعيد بن جبير فقال: أيكم رأى الكوكب الذي انقض البارحة؟ فقلت: أنا، ثم قلت: أما إني لم أكن في صلاة، ولكني لُدِغت، قال: فما صنعت؟ قلت: ارتقيت قال: فما حملك على ذلك؟ قلت: حديث حدثناه الشعبي، قال وما حدثكم؟ قلت: حدثنا عن بريدة بن الحصيب أنه قال: لا رقية إلا من عين أو حمة. قال: قد أحسن من انتهى إلى ما سمع. ولكن حدثنا ابن عباس عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: [عرضت علي الأمم، فرأيت النبي ومعه الرهط، والنبي ومعه الرجل والرجلان، والنبي وليس معه أحد، إذ رفع لي سواد عظيم، فظننت أنهم أمتي، فقيل لي: هذا موسى وقومه، فنظرت فإذا سواد عظيم، فقيل لي: هذه أمتك ومعهم سبعون ألفاً يدخلون الجنة بغير حساب ولا عذاب، ] ثم نهض فدخل منزله. فخاض الناس في أولئك، فقال بعضهم: فلعلهم الذين صحبوا رسول الله صلى الله عليه وسلم. وقال بعضهم: فلعلهم الذين ولدوا في الإسلام فلم يشركوا بالله شيئاً، وذكروا أشياء، فخرج عليهم رسول الله صلى الله عليه فأخبروه، فقال: [هم الذين لا يسترقون ولا يكتوون ولا يتطيرون وعلى ربهم يتوكلون] فقام عكاشة بن محصن فقال: ادع الله أن يجعلني منهم. قال: [أنت منهم] ثم قام رجل آخر فقال: ادع الله أن يجعلني منهم. فقال: [سبقك بها عكاشة]
فيه مسائل:
الأولى: معرفة مراتب الناس في التوحيد
الثانية: ما معنى تحقيقه
الثالثة: ثناؤه سبحانه على إبراهيم بكونه لم يكن من المشركين
الرابعة: ثناؤه على سادات الأولياء بسلامتهم من الشرك
الخامسة: كون ترك الرقية والكي من تحقيق التوحيد
السادسة: كون الجامع لتلك الخصال هو التوكل
السابعة: عمق علم الصحابة لمعرفتهم أنهم لم ينالوا ذلك إلا بعمل
الثامنة: حرصهم على الخير
التاسعة: فضيلة هذه الأمة بالكمية والكيفية
العاشرة: فضيلة أصحاب موسى
الحادية عشرة: عرض الأمم عليه، عليه الصلاة والسلام
الثانية عشرة: أن كل أمة تحشر وحدها مع نبيها
الثالثة عشرة: قلة من استجاب للأنبياء
الرابعة عشرة: أن من لم يجبه أحد يأتي وحده
الخامسة عشرة: ثمرة هذا العلم، وهو عدم الاغتـرار بالكثـرة، وعـدم الزهد في القلة
السادسة عشرة: الرخصة في الرقية من العين والحمة
السابعة عشرة: عمق علم السلف لقوله: قد أحسن من انتهى إلى ما سمع، ولكن كذا وكذا. فعلم أن الحديث الأول لا يخالف الثاني
الثامنة عشرة: بعد السلف عن مدح الإنسان بما ليس فيه
التاسعة عشرة: قوله: (أنت منهم) علم من أعلام النبوة
العشرون: فضيلة عكاشة
الحادية والعشرون: استعمال المعاريض
الثانية والعشرون: حسن خلقه صلى الله عليه وسلم
ATAKAE HAKIKSHA TAWHIDI (KUMPWEKESHA MWENYEZI MUNGU) ATAINGIA PEPONI BILA YA HESABU
Na kauli yake Mwenyzi Mungu ﷻ:
[Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa MwenyeziMungu, mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.] [An-Nahl: 120]
Na Amesema:
[Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi,] [Al-Muuminuun:59]
Na Kutoka kwa Huswayn bin ‘Abdir-Rahmaan amehadithia: Siku moja nilipokuwa na Sa’iyd bin Jubayr, aliuliza: “Nani miongoni mwenu aliyeona kimondo (nyota inayofukuza shaytwaan) jana usiku?” Nikajibu: “Mimi nimeiona.” Kisha nikaelezea kwamba sikuwa nikiswali wakati ule sababu nilidonelewa na nge mwenye sumu. Akasema: “Kisha ukafanya nini?” Nikajibu: “Nilifanya Ruqya (kujitibu). Akauliza: “Kitu gani kimekupeleka ufanye hivyo?” Nikasema: “Ni Hadithi niliyoisikia kutoka
Kwa Ash-Sha’biyy.” Akauliza: “Amekuhadithieni nini Ash-Sha’biyy?” Nikajibu: “Amehadithia kutoka kwa Buraydah bin Al-Huswayb amesema kwamba Ruqyah hairuhusiwi isipokuwa kwa ajili ya kijicho na kudonelewa (na mdudu sumu).” akasema (Sa’iyd bin Jubayr): “Amefanya vyema kukomea kwenye aliyosikia. Lakini Ibn ‘Abbaas ametusimulia kwamba Mtume ﷺ amesema: [Nilionyeshwa Ummah (uliotangulia), nikamuona Nabii akiwa na kundi dogo la watu, na Nabii akiwa na mtu mmoja au wawili, na Nabii akiwa hana mtu yeyote. Kisha nikaoneshwa idadi kubwa ya watu niliodhania ni katika Umma wangu, lakini nikaambiwa: Huyo ni Musa na watu wake. Kisha nikatazama nikaona kundi kubwa ambalo nikaamibwa: Hawa ni watu wako, miongoni mwao ni watu elfu sabini watakaoingia Peponi bila hesabu wala adhabu]. Kisha akainuka kuingia nyumbani kwake, watu wakaanza kujadiliaina ni nani hao watakaoweza kuwa. Wengineo wakasema: “Labda ni Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ .” Wengine wakasema: “Labda ni wale waliozaliwa katika Uislamu na hawakumshirikisha Mwenyezi Mungu kwa chochote.” Na wakataja mengine kadhaa, Akawatokea Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ na wakamwambia (waliyokuwa wakiyajadili). Akasema (Mtume ﷺ): [Ni wale ambao wasiotafuta kufanyiwa Ruqya, wala kujichoma chuma cha moto, wala hawaamini Itikadi ya mkosi au nuksi, na kwa Mola wao wanamtegemea Pekee] Ukaashah bin Mihswan akasimama akasema: “Muombe Mwenyezi Mungu niwe mmoja wao.” Akasema: [Wewe ni mmoja wao]. Kisha mtu mwengine akasimama akasema: Muombe Mwenyezi Mungu niwe mmoja wao (pia). Akasema: [Ukaashah amekutangulia] [Al-Bukhari na Muslim]
MASUALA MUHIMU YALIYOMO:
1- Kujua Daraja za watu juu ya Tawhid.
2- Nini Maana halisi ya kuhakiksha Tawhidi.
3- Mwenyezi Mungu ﷻ kumsifia Ibrahim (Amani ya Mungu iwe juu yake) kwamba hakuwa miongoni mwa washirikina.”
4- Mwenyezi Mungu ﷻ kuwasifu Mawali (waja wema) kwa kusalimika na shirki.
5- Kuikwepa Ruqyah na kuchomwa chuma cha moto ni miongoni mwa sifa za Tawhid.
6- Mkusanyiko wa Sifa zote hizi ni kutokana Kumtegemea Mwenyezi Mungu ﷻ.
7- Elimu ya kina ya Maswahaba kwa kujua kwao kuwa wasingeifikia hali hiyo pasina ‘amali njema.
8- Kuwa na pupa (kwa Maswahaba) juu kutenda kila la kheri.
9- Ubora wa umma huu (wa Kiislamu) kwa wingi na ubora.
10- Ubora wa wafuasi wa Musa (Amani ya Mungu iwe juu yake).
11- Kudhihirishwa Umma zote mbele ya Mtume ﷺ.
12- Kila Ummah utakusanywa peke yake pamoja na Nabiy wake.
13- Uchache wa walio itikia wito wa Manabii.
14- (Mtume) Asiepata wafuasi atahudhuri peke yake (Mbele ya Mwenyezi Mungu).
15- Faida ya elimu hii kuwa mtu asidanganyike kwa wingi au kukatishwa tamaa na uchache wa idadi ya watu.
16- Ruhusa ya Ruqya (kuzungua) kwa ajili ya kijicho au kudonolewa na chenye sumu.
17- Elimu ya kina kwa Salaf kama inavyoonekana katika kauli. “Amefanya vyema kukomea kwenye aliyosikia…” Tambua kwamba Hadithi ya kwanza haipingani na ya pili.
18- Kujiepusha kwa Salaf kumsifu mtu bila ya kustahiki.
19- Kauli ya Mtume ﷺ: [Wewe ni miongoni mwao] ni alama ya Unabiy.
20- Fadhila za ‘Ukaashah (Radhi za Allah ziwe juu yake).
21- Kutumia mafumbo, (Maaridh: ni – kutaja kauli isiyo dhahiri, au kielezo fulani cha kutolea tafsiri mbali mbali).
22- Tabia njema za Mtume ﷺ.