KITAAB AT-TAWHIID
باب فضل التوحيد وما يكفر من الذنوب
وقول الله تعالى: {الَّذِينَ آمَنُواْ وَلَمْ يَلْبِسُواْ إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ} ( )الآية
عن عبادة بن الصامت رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: [من شهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له، وأن محمداً عبده ورسوله، وأن عيسى عبد الله ورسوله وكلمته ألقاها إلى مريم وروح منه، والجنة حق، والنار حق أدخله الله الجنة على ما كان من العمل]. أخرجاه
ولهما في حديث عتبان: [فإن الله حرم على النار من قال: لا إله إلا الله يبتغي بذلك وجه الله]
وعن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: [قال موسى: يا رب، علمني شيئاً أذكرك وأدعوك به. قال: يا موسى: قل لا إله إلا الله. قال: يا رب كل عبادك يقولون هذا. قال: يا موسى، لو أن السموات السبع وعامرهن غيري، والأرضين السبع في كفة، ولا إله الله في كفة، مالت بهن لا إله الله] رواه ابن حبان، والحاكم وصححه
وللترمذي وحسنه عن أنس رضي الله عنه: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: [قال الله تعالى: يا ابن آدم؛ لو أتيتني بقراب الأرض خطايا، ثم لقيتني لا تشرك بي شيئاً لأتيتك بقرابها مغفرة]
:فيه مسائل
الأولى: سعة فضل الله
الثانية: كثرة ثواب التوحيد عند الله
الثالثة: تكفيره مع ذلك للذنوب
الرابعة: تفسير الآية (82) التي في سورة الأنعام
الخامسة: تأمل الخمس اللواتي في حديث عبادة
السادسة: أنك إذا جمعت بينه وبين حديث عتبان وما بعده تبين لك معنى قول: (لا إله إلا الله) وتبين لك خطأ المغرورين
السابعة: التنبيه للشرط الذي في حديث عتبان
الثامنة: كون الأنبياء يحتاجون للتنبيه على فضل لا إله إلا الله
التاسعة: التنبيه لرجحانها بجميع المخلوقات، مع أن كثيراً ممن يقولها يخف ميزانه
العاشرة: النص على أن الأرضين سبع كالسموات
الحادية عشرة: أن لهن عماراً
الثانية عشرة: إثبات الصفات، خلافاً للأشعرية
الثالثة عشرة: أنك إذا عرفت حديث أنس، عرفت أن قوله في حديث عتبان: [فإن الله حرم على النار من قال لا إله إلا الله، يبتغي بذلك وجه الله] أنه ترك الشرك، ليس قولها باللسان
الرابعة عشرة: تأمل الجمع بين كون عيسى ومحمد عبدي الله ورسوليه
الخامسة عشرة: معرفة اختصاص عيسى بكونه كلمة الله
السادسة عشرة: معرفة كونه روحاً منه
السابعة عشرة: معرفة فضل الإيمان بالجنة والنار
الثامنة عشرة: معرفة قوله: [على ما كان من العمل
التاسعة عشرة: معرفة أن الميزان له كفتان
العشرون: معرفة ذكر الوجه
FADHLA ZA TAWHID NA YANAYOFUTA MADHAMBI
Na kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma – hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka.] [Al-An’aam: 82]
Imepokelewa kutoka kwa Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhi za Allah ziwe juu yako) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: [Atakayeshuhudia kwamba hapana Mola apasae Kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, Hana mshirikia, na kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume wake, na kwamba ‘Isa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na neno Lake Alilolitia kwa Maryam na Roho kutoka kwake, na kwamba Pepo ni haki, na Moto ni haki, Mwenyezi Mungu Atamuingiza Peponi kwa kiasi chochote cha ‘amali yake itakavyokuwa] [Imepokewa na Bukhari, na Muslim]
Na Imepokelewa na Bukhari na Muslim Katika Hadithi iliyopokewa toka kwa Utbaan (Radhi za Allah ziwe juu yake): [Hakika Mwenyezi Mungu Ameharamisha moto kwa anayesema: “Laa ilaaha illa-Allaah”, (Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu) akikusudia kutafuta Radhi za Mwenyezi Mungu]
Na Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: [Musa alisema: Ewe Mola! Nifundishe kitu ambacho nikutaje kwacho na nikuombe. Akasema (Mwenyezi Mungu): Ewe Musa: Sema: “Laa ilaaha illa-Allaah.” (Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu) Musa akasema: Ewe Mola wangu! Kila mja anasema hivi. Akasema: Ewe Musa, lau kama mbingu saba na kila kilichokuwemo isipokuwa Mimi, na ardhi saba zikiwekwa katika kiganja cha mizani, na Laa ilaaha illa-Allaah imewekwa katika kiganja kingine cha mizani, basi Laa ilaaha illa-Allaah itazishinda hizo] [Imepokewa na Ibn Hibaan, na Al-Haakim na ameikiri kuwa ni Sahihi]
Na kutoka kwa At-Tirmidhiy aliyoipa daraja ya Hasan, Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema: [Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ewe bin Adam! Lau utanijia na Madhabi ya kukurubia kuijaza Ardhiukinijia, kisha ukakutana nami hunishirikishi na kitu chochote, Nitakujia kwa wingi wa maghfirah kama hayo]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1- Ukunjufu wa fadhila na rahmah za Mwenyezi Mungu ﷻ.
2- Malipo mengi Anazozilipa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Tawhid. (Kumpwekesha Mungu)
3- Tawhid inafuta dhambi juu ya kuwa ina fadhila na Thawabu.
4- Tafsiri ya Aya katika Suwrah Al-An’aam (82).
5- Zingatia nukta tano zilizopatikana katika Hadith ya ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhi za Allah ziwe juu yako).
6- Unapounganisha baina ya Hadith ya (Ubaada bin Asw-Swamit Radhi za Allah ziwe juu yka) na Hadithu ya Utbaan na zinayoifuatia, basi utapata kujua Maana ya kalimah ‘Laa ilaaha illaa Allaah’ inakuwa dhahiri kabisa na kudhihirisha makosa ya walioghurika nayo.
7- Kuzingatia sharti liliomo katika Hadith ya Utbaan (Radhi za Allah ziwe juu yake).
8- Manabii (swala na salamu ziwefikie wao) walikuwa na haja ya kutanabahisha juu ya fadhila za ‘Laa ilaaha illa-Allaah’.
9- Tanbihi kuwa kalima hii ya (Lailaha Illa Allah) itashinda viumbe wote kwa (uzito wake itapo wekwa katika miazni) ingawa wengi wanaoitamka mizani zao zitakuwa khafifu.
10- Dalili yathibitisha kuwa kuna ardhi saba kama ambavyo ziko mbingu saba.
11- Mbingu na ardhi zimejaa viumbe.
12- Kuthibitisha Sifa za Mwenyezi Mungu ﷻ kinyume na madai ya Ash’ariyyah.
13- Unapoifahamu Hadith ya Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake), utaifahamu kauli ya Mtume ﷺ katika Hadith ya ‘Utbaan (Radhi za Allah ziwe juu yake ). [Hakika Mwenyezi Mungu Ameharamisha Moto kwa anayesema: “Laa ilaaha illa-Allaah”, akikusudia kutafuta Wajihi wa Allaah] inaamanisha kwa kuepuka shirki, wala sio kwa kuitamka kwa ulimi tu.
14- Kutaamali mkusanyiko wa sifa zinazolingana baina ya ‘Isa (swala na salamu ziwefikie yeye) na Muhammad ﷺ. Kuwa wao ni Mitume wa Mwenyezi Mungu na waja wake.
15- Kujuwa kuwa ‘Isaa (swala na salamu ziwefikie yeye) alipewa sifa mahususi kuwa aliumbwa kwa ‘Kalimatu-Allaah’ (neno la Mungu).
16- Kujua kwamba ‘Isa (swala na salamu ziwefikie yeye) ni Roho Alioumba kwa amrisho kutoka Kwake.
17- Kujua fadhila za kuamini kuwa kuna Pepo na Moto.
18- Kujua neno la Mtume ﷺ [Kwa kufanya amali yake itakavyokuwa].
19- Kujua kuwa mizani ina pande mbili (za kipimo cha kuliani na kushotoni).
20- Kujua Maana ya ‘Uso wa Mwenyezi Mungu’.