0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MKATABA WA KIISLAMU


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Mtume () alianzisha kanuni ya udugu miongoni mwa waumini, hivyo alikuwa makini kuanzisha mahusiano ya kidugu kati ya Waislam na wasiokuwa Waislamu miongoni mwa makabila ya Kiarabu. Alianzisha aina ya Mkataba uliokuwa na madhumuni ya kuondoa uhasama kati ya Makabila.

Alikuwa makini sana kutoacha mwanya katika mkaraba huo ili mambo ya Jahiliya yasiharibu mazingira mapya aliyokuwa anayajenga.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Huu ni Mkataba kutoka kwa Muhammad, Mjumbe wa Allah kuhusu Muhajirina na Answaar
na Wale waliokuwa nao. Hapa tutapitia baadhi ya vifungu:
1. Kwa hakika wao ni umma mmoja ukiwatoa watu wengine.
2. Muhajirina kafika Makuraishi ni juu yao kutoleana malipo kati yao — wakati wamekosa — na watamkomboa mhalifu wao, kati ya waumini, kwa wema na uadilifu. Kila kabila katika
Answaar watakuwa juu yao, kutoleana malipo ya makosa – malipo yao ya mwanzo na kila kundi katika wao watamkomboa mateka wao, kati ya waumini, kwa wema na uadilifu.
3. Waumini hawatamwacha mwenye deni kati yao, isipokuwa watampa cha kujikombolea kwa wema au malipo ya uhalifu.
4. Kuwa Wachamungu katika Waumini watakuwa dhidi ya yule ambaye amefanya uovu miongoni mwao au anaetaka kufanya dhulma au dhambi au uadui an ufisadi kwa waumini.
5. Yeyote anayeasi au anayetaka kueneza uadui, Mikono (Nguvu za) ya Waumini itakuwa dhidi yake-hata akiwa ni mwanae.
6. Muumni hatomwuwa Muumini mwenziwe;
7. Muumini hatomuunga mkono Kafiri dhidi ya Muumini mwenzake.
8. Kwamba Ulinzi wa Mwenyezi Mungu’ ni mmoja na pia huwafikia Waumini wanyenyekevu.
9. Kwamba yeyote miongoni mwa Mayahudi atakaefuata Uislamu atasaidiwa, hatodhuriwa na adui hatosaidiwa dhidi yake.
10. Amani ya Waumini ni moja haigawiki; Haifanywi amani wakati Waumini wanapigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Masharti ya kuwepo amani ni uadilifu na usawa.
11. Kwamba Waumini hawatamwacha mwenzao masikini bila ya kumlipia fidia, au fidia ya kuuawa kwa mtu.
12. Muhajirina waungane pamoja na walipane fidia, na wawaache huru mateka wa kivita.
13. Kumwuwa Muumini kwa makusudi bila sababu inayokubalika atachukuliwa kisasi isipokuwa walii wa
mwenye kuuwawa atakapoamua vinginevyo.
14 . Waumini ni juu yao wote hayo na si halali kwao ila kufanya.
15. Kwa hakika si halali kwa Muumini kumnusuru mhalifu na kumpa hifadhi na kuwa mwenye kumnusuru au kumhifadhi,
atapata laana na ghadhabu za Mwenyezi Mungu () siku ya Qiyama. Na Toba yake haitapokelewa.
16. Wakafi wowote mtakapotofautiana katika jambo marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu () na kwa Mtume (). (1)


1) Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 502-503

Begin typing your search above and press return to search.