0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MKATABA NA MAYAHUUDI

Baada ya Mtume () kuhama na kwenda Madina, na kuwa na uhakika wa kukita misingi ya jamii mpya ya Kiislamu kwa kusimamisha umoja wa kiitikadi, kisiasa na kinidhamu kati ya Waislamu, aliona ni bora asimame na kupanga mahusiano yake na wasiokuwa Waislamu. Katika hili hamu yake ilikuwa ni kuimarisha usalama, amani, furaha na kheri kwa watu wote. Pamoja na kulipanga eneo katika makubaliano akaweka kwa ajili ya hilo, kammi za kusameheana na kusahau yaliyopita, kanuni ambazo zilikuwa ngeni kalika ulimwengu ambao ulikuwa umejaa ubaguzi na majigambo.
Watu waliokuwa wakiishi jirani na Madina katika wasiokuwa Waislamu ni Mayahudi, ambao kwa kiasi
walijitahidi kuficha uadui wao dhidi ya Waislamu, hawa hawakuonyesha dalili za mapambano yoyote au uhasama kwa Waislamu moja kwa moja. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () alifunga nao mkataba ambao uliwaachia uhuru wa moja kwa moja katika dini na mali na ambao haukuelekea
kwenye siasa ya kuwafukuza au kuwawekea vikwazo au kuwafanyia uhasama. Vilevile kiliingizwa kipengele hiki katika mkataba ambao ulifanyika kati ya Waislamu wenyewe na ambao umepita utajo wake. Vipengele na vifungu, muhimu vya mkataba huo, vilikuwa ni:-
Vifungu Vya Mkataba:
1. Mayahudi wa Banu Aufi ni umma mmoja pamoja na waumini wengine wa Kiyahudi watahusika na dini yao, na Waislamu watahusika na Dini yao, walioachwa huru wao na nafsi zao; na mambo yatakuwa vivyo hivyo kwa wasiokuwa Banu Aufi katika Mayahudi.
2. Kwa uhakika Mayahudi watagharamia matumizi yao na Waislamu hali kadhalika watagharamia yao. ‘
3. Kuwa watasaidiana kupambana na yeyote atakayempinga mmoja katika ya watu waliotiliana saini Mkataba huu.
4. Kuwa kati yao patakuwa pana kunasihiana na kuamrishana mema na siyo maovu. 
5. Kuwa hatakuwa na madhambi mtu kwa sababu ya mshirika wake.
6. Kuwa kunusuriwa ni kwa mwenye kudhulumiwa.
7. Kuwa Mayahudi wataendelea kuishi pamoja na Waislamu hata kipindi ambacho watakuwa wamo katika vita.
8. Kuwa mji wa Yathrib utaendelea kuwa ni mji Mtukufu wenye kuchungwa haki zake zote, kwa wale wote waliosaini mkataba huu. .
9. Kuwa magomvi na kutokuelewana kunakotishia amani kukitokea miongoni mwa watu wa mkataba huu
utashughulikiwa na kutolewa hukmnu kwa kufata hukumu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kwa hukumu ya Muhammad ().
10. Kuwa Makuraishi hawatadhaminiwa wala wale ambao wanawanusuru.
11. Kuwa kati yao pana kunusuriana, ikitokea Yathrib kuvamiwa; kila watu watawajibika kwa sehemu iliyo upande wao. 
12. Kuwa mkataba huu hautamhusu dhalimu au mtu mtenda madhambi.  (1)

Kwa kuufunga Mkataba huu, Madina na viunga vyake ikawa ni dola ya makubaliano, mji wake mkuu ni Madina na Mtawala wake kufuatana na ibara hii, ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w). Kwa kauli yenye nguvu (ya watu inayofanyiwa kazi) inasemwa kuwa Waislamu ndo waliokuwa wengi Madina na kwa msingi huo, Madina ukawa ndio mji mkuu wa kwanza wa Kiislamu.
Kwa lengo la kupanua eneo la amani na usalama, Mtume (s.a.w) alifanya mikataba ya aina hii na makabila mengine ya jirani, kila moja kufuatana na mazingira yake, baadaye tutalét ufafanuzi wake.


1) IbnHisham, Iuzuu 1, Uk. 503-504.

Begin typing your search above and press return to search.