Visa na Kejeli za Makuraishi dhidi ya Waislamu baada ya Hijra, na Mawasiliano yao na Abdillah bin Ubay.
Tumekwisha kutaja mambo yaliyokuwa yakitendwa na makafiri wa Makka katika mateso na matendo mengine maovu dhidi ya Waislamu, pamoja na waliyoyafanya wakati wa kuhama kwa Waislamu. Walistahiki kwa ajili hiyo kuwekewa vikwazo na kupigana nao.
Pamoja na hayo hawakuzinduka na kuacha upotevu wao, na kujizuia na uadui wao dhidi ya Uislamu. Kukosa kuwafanyia dhulma Waislamu na kuona kuwa wamepata amani na makao huko Madina kuliwaongezea chuki. Wakamwandikia Abdillah bin Ubay bin Saluul, ambaye wakati huo alikuwa bado ni Mshirikina, aliyekuwa kiongozi wa Answaar kabla ya Hijra (ni jambo linaloeleweka kuwa wao walikuwa wanamwona kuwa ni Mfalme wao, lau si Kuhajiri Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) na kumuamini watu wa Madina). Walimwandikia barua yeye na Mushirikina wenzake kwa maneno ya mkato :-
”Kwa hakika nyinyi mmemuhifadhi mtu wetu na tunawaomba kwa jina la Mwenyezi Mungu ima mumpige vita au mumfukuze katika mji wenu, vinginevyo tutakuja kuwavamia nyote, tulimalize jeshi lenu na tuwahalalishe wake zenu (1)
Baada ya kupokea barua hii, Abdillah bin Ubay alisimama na kuanza kutekeleza amri za Mushirikina wenzake wa Makka. Hasa kwa vile yeye mwenyewe alikuwa na mfundo wa siku nyingi dhidi ya Mtume (s.a.w) kwa kuIe kuamin; kwake kuwa Mtume (ﷺ) alimnyang’anya ufalme uliokuwa wake.
Abdul Rahmani bin Kaabi alisema; ”Zilipofika taarifa hizo kwa Abdillah bin Ubay, yeye na waliokuwa pamoja naye miongoni mwa Wale wenye kuabudu masanamu walikutanika na kupanga njama za kumpiga vita Mjumbe wa Mwenyez Mungu (ﷺ).” Khabari hizo zilipomfikia Mtume (ﷺ ) aliwaita na kukutana nao na akawaambia, “Kwa hakika nia mbaya ya Makuraishi itawafikisha pabaya, lakini uovu mnaokusudia kuufanya ni mkubwa zaidi kuliko nia ya Makuraishi. Mnataka kuwapiga vita watoto wenu na ndugu zenu?.” Waliposikia maneno hayo kutoka kwa Mtume (ﷺ) wote walitawanyika. (2)
Abdillah bin Ubayi bin Salul alijizuia kupigana vita baada ya kuona ndugu na marafiki zake wamenyong’onyea na kurudi nyuma, hata hivyo ilidhihirika kuwa alikuwa tayari ameshapatana na Makuraishi. Kila ilipotokea fursa aliitumia ili kuingiza fitna kafi ya Waislamu na Mushirikina.
Alikuwa akiwakusanya Mayahudi ili wamsaidie katika kueneza fitna. Lakini Mkataba ndio uliokuwa hekima ya Mfume (ﷺ.) ambayo ilikuwa inauzima moto wa shari zao kila walipojaribu kuuwasha. (3)
1) Abuu Daud
3) Sahihil Bukhari, juzuu 2, Uk. 655, 656, 916, 924