KUZALlWA KWAKE, KUKUA KWAKE NA FADHILA ZAKE
Jina lake ni Ali ibn Abi Talib ibn Abdul-Muttwalib ibn Hashirn ibn Abdi Manaf AI-Qurashy.
Ali (r.a.) alikuwa binamu wa Mtume ﷺ.
Mtume ﷺ alimuoza binti yake, Fatimah Az-Zahra’, Naye (r.a.) ni Khalifa wa nne katika Makhalifa Waongofu. Naye ni miongoni mwa Masahaba kumi waliobashiriwa Pepo.
Ali (r.a.) alizaliwa katika mji mtukufu wa Makka kabla ya kutumilizwa Mtume ﷺ kwa miaka kumi. Baba yake ‘Ali (r.a.),Abu Talib, alikuwa na watoto wengi. Mtume ﷺ akamuomba ami yake Abu Talib ampatie ‘Ali (r.a.) amlee. Kwa hiyo ‘Ali (r.a.) aliishi na Mtume ﷺ kutoka udogoni mwake. Na kufuata tabia za Mtume ﷺ.
Alipotumilizwa Mtume ﷺ, ‘Ali (r.a.) alikuwa ni wa kwanza kusilimu katika watoto na akawa anauficha Uislamu wake. Alipotambua Abu Talib, alimuuliza: “Ni dini gani hii ambayo wewe unaifuata?” Akamjibu: “Ewe baba yangu, mimi nimemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na nikayaamini yale aliyokuja nayo Mtume, na nikasali pamoja nave kwa ajili ya Allah na nikamfuata yeye.” Na wengine wamesema kuwa Abu-Talib alimwambia ‘Ali (r.a.): “Ama kwa hakika Muhammad hakukulingania isipokuwa kwenye kheri basi wajibika naye.” [Sayratu ibn Hisham Juz. 1 uk. 246]
Ama Abu Talib hakuamini mpaka kufa kwake bali amekufa katika ukafiri, juu ya mila ya Abdul-Mut’Ialib.
mama yake ‘Ali (r.a.), Fatima bint Asad ibn Hashim ibn Abdi Manaf alisilimu mwanzoni,akahamia Madinah. [Tarikhul-Islam Juz. 1 uk. 265]
Ali (r.a.) aliishi na Mtume ﷺ uhai wake wote walipokuwa Makkah, akawa anamsaidia katika kueneza Uislamu, na kuwasaidia watu ambao wakija Makkah kutafuta haki na kutaka Uisiamu. Yeye ndiye ambaye alimchukua Abu Dharr mpaka kwa Mtume ﷺ, akamsikiliza Mtume ﷺ kisha akasilimu hapo hapo. [Al-Bukheri Juz. 1 uk.499]