0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUWATENDEA WEMA WAZAZI WAWILI

KUWATENDEA WEMA WAZAZI WAWILI

Wazazi wawili wanayo haki kubwa kutoka kwa watoto wao, kama walivyo na haki watoto kutoka kwa wazazi wao. Mwenyezi Mungu  Ameweka wazi kabisa haki za Pande zote mbili. Mwenyezi Mungu hakuwaachia wanadamu wajipangie wenyewe haki zao, bali Yeye Mwenyewe Amechukua jukumu la kuwapangia kila moja haki yake ili asipatikane na upungufu au dhulma katika kugawa hizo haki. Wazazi wana nafasi kubwa katika Dini ya Kiislamu. Wao ndio sababu ya kupatikana mtoto, baada ya kuvumilia na kusubiri juu ya shida nyingi kisha kuzaliwa mtoto. Kwa kuvumilia kwao na kusubiri juu ya shida zote, wamepata cheo kikubwa mbele ya Mwenyezi Mungu .

Mwenyezi Mungu ﷻ ameambatanisha haki yake pamoja na haki ya wazazi wa wili. katika aya kadha katika kitabu chake kitukufu, nayo ni haki ya wazazi wawili. Jueni kwamba mafungamano makubwa baina ya mja na Mola wake ni kuumcha Mwenyezi Mungu  na kusimamia haki za wazazi na kusimamia haki za waja wake.

Amesema Mwenyezi Mungu  ﷻ

وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا} النساء :36}

[Mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili]     [Al Nnissa:36]

Jueni waja wa Mwenyezi Mungu kwamba kuwafanyia wema wazazi wawili ni wajibu hata kama ni makafiri, imepokewa na Asema:

قدمتْ عليّ أمي وهي مشركة في عهد رسول الله -صلى الله عليه وسلم-، فاستفتيت رسول الله -صلى الله عليه وسلم-، قلت: وهي راغبة، أفأصل أمي؟ قال: نعم، صلي أمك رواه البخاري ومسلم

[Amenijia mamangu na yeye ni mshirikina wakati wa Ahadi ya mtume (yani kipindi mtume amefanya itafaki a mushrikina ) nikamuliza Mtume ﷺ ni kasema (amenija) na yeye ataka ni muunge je ni muunge mamangu? Akasema Mtume ﷺ : [Ndio muunge mamako]. [Imepokewa na Bukhari na Muslim].

Wema kwa wazazi haukatiki hata kama watakuamrisha kumkufuru Mwenyezi Mungu na kumshirikisha.Isipokuwa itakuwa haifai kuwatii kwa hilo.

Amesema Mwenyezi Mungu 

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُوَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُون} لقمان:14-15

[Na tumemuusia mwanadamu kuwafanyia ihsani wazazi wake mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumnyonyesha na kuja kumuachisha kunyonya katika miaka miwili- basi unishukuru Mimi na wazazi wako; marejeo yenu ni kwangu. Na wazazi wako wakikushurutisha kunishirikisha na yale ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani]   [Luqman:14-15]

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu alitanguliza haki za wazazi wawili kuliko jihadi. Imepokewa Hadithi na ‘Abdillah Ibn Mas’oud Amesema:

سألت النبي -صلى الله عليه وسلم- أي العمل أحب إلى الله تعالى؟ قال: الصلاة على وقتها، وقال: قلت: ثم أي؟ قال: بر الوالدين، قلت: ثم أي؟ قال: الجهاد في سبيل الله متفق عليه

[Nimemuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu ni amali gani inayo pendeza mbele ya Mwenyezi Mungu? Akasema: Kuswali kwa wakati wake. Nikasema kisha ni amali gani? Akasema: kuwafanyia wema wazazi wawili. Nikasema kisha amali gani? Akasema: jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Imepokewa na Muawiya bin Jahim Amesema: Amekuja mtu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema nataka kwenda jihadi, na nimekuja kukushauri. Akasema Mtume ﷺ je una mama? Akasema ndio. Akasema Mtume  jilazimishe na mama yako, kwani pepo iko chini ya miguu yake.

Na Mtume  anaomba kwa aliyepata wazazi wawili au mmoja wao na hakuingia peponi kwasababu yao basi mtu huyu amekhasirika].

Na visa vya wale watu watatu waliofunikwa na pango na hawakuweza kutoka akasema mmoja wao angalieni amali njema mliyomfanyia Mwenyezi Mungu, mumuombe Mwenyezi Mungu kupitia amali hiyo huenda Mwenyezi Mungu akatufariji, akasema mmoja wao: nilikuwa na wazazi wawili watu wazima na nilikuwa na watoto wadogo na nilikuwa nikiwachungia na ninapokamua nawanywesha wazazi wangu kabla ya watoto wangu, nilipokuja jioni na maziwa nimewakuta wamelala, nikaona vibaya kuwaamsha, pia nikachukia kumtanguliza mtoto wangu kabla yao na mtoto wangu alikuwa akilia na ilikuwa hivyo mpaka alfajiri, ewe Mwenyezi Mungu ukijua tendo langu hilo nikutaka radhi zako basi tufariji, Mwenyezi Mungu akawafariji mpaka wakawa wanaona mbingu.

Na katika kuwatendea wema ni kuwatii maadamu hujakhalifu amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:

{وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا}

[Kaa na wao kwa wema hapa duniani”]

Na haki yao ni kuwapatia matumizi na kuwavisha ikiwa ni maskini, na kuwaombea Mwenyezi Mungu wakiwa hai na baada ya kufa Amesema Mwenyezi Mungu 

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا

[Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu. Na kuwafanyia wema wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee, naye yuko pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata Ah. Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa heshima”]

Imepokewa na Ibn ‘Umar kwamba yeye akitoka kuelekea Makkah alikuwa na punda na kilemba amejifunga nacho kichwani, siku moja alikutana na Bedui, akasema Bedui yule kumwambia Ibn ‘Umar Je, wewe si mtoto wa fulani? Ibn ‘Umar akasema ndio. Pale pale Ibn ‘Umar akampa punda yule Bedui ampande na kilemba ajifunge. Baadhi ya Maswahaba wakasema Mwenyezi Mungu akusamehe umempatia bedui huyu punda ambaye kwamba ulikuwa ukitembea naye na kilemba uliyokuwa umejifunga nacho. Akasema amesema Mtume ﷺ [Bora ya wema ni kuunga mtu vipenzi vya babake baada ya kuondoka duniani].

THAWABU ZA KUWATENDEA WEMA WAZAZI WAWILI

Kuwatendea wema wazazi wawili ni sababu ya kuingia peponi, je umepata kujua kisa cha Uweis Bin Annur Al-Qarni? Huyu ni mtu aliyesimuliwa na Mtume kisa chake na akaamrisha maswahaba zake kutaka dua kutoka kwake, na kukurubishwa kwa Mwenyezi Mungu na haikuwa alama yake isipokuwa kuponya, hadithi ambayo ameipokea Imam Muslim inaeleza kuwa ‘Umar alijiwa na pote kutoka Yemen akauliza jee kuna Uweis kati yenu? Mpaka alipokuja Uweis akasema wewe ndio Uwes? Akasema ‘Umar jee ulikuwa na ugonjwa wa ukoma ukapona isipokuwa sehemu kama ya shilingi, akasema ndio, akasema ‘Umar jee una mama? Akasema ndiyo. Akasema nimemsikia Mtume ﷺ akisema: [Atakujieni Uweis na pote kutoka Yemen na alikuwa na ukoma na akapona ila sehemu ya shilingi na alikuwa mwema kwa mamake akimuapia Mwenyezi Mungu huwa jambo hilo ukiweza akuombee msamaha] Akasema ‘Umar niombee msamaha na akamuombea ‘Umar msamaha.

Na Muhammad Ibn Sirin alikuwa akinyenyekea anapozungumza na mamake.

Hassan bin ‘Ali Ibn Hussein Zeinul ‘Abidin alikuwa akimfanyia wema mamake mpaka akaulizwa siku moja, kwa nini hatukuoni ukila sahani moja na mamako? Akasema naogopa kutangulia mkono wangu sehemu ambao kwamba jicho la mama limekwisha kutangulia, na hapo nitakuwa nimemuasi.

Na huyu Shureyh alikuwa ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa alikuwa akiwafundisha wanafunzi wanaokuja kutoka sehemu mbali mbali na mamake alikuwa akimtuma kwa kumwambia awapatie chakula kuku, basi husimama na kuacha kufundisha. Huu ni mfano wa watu wema waliotangulia, vipi hali ya barobaro wetu leo huenda mmoja wao kukosea heshima mzazi wake na kumridhisha rafiki yake. Nakuusieni kuwafanyia wema wazazi wenu na kwenda mbio kuwaridhisha wao.


SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH SWADIQ ALI



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.