0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUUNGANISHA UDUNGU MIONGONI MWA WAISLAMU


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Kama ambavyo Mtume () alivyosimama kwa ajili ya ujenzi wa msikiti, makao makuu ya kukutanika Waislamu na kuzoeana kwa siku mara tano, pia alisimamia kazi nyingine. Miongoni mwa mambo bora ambayo yamepokelewa na historia ni kazi ya kuunganisha udugu kati ya Muhajirina kutoka Makka na ndugu zao Maansar pale Madina.
Ibn Qayyim alisema; “Kisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () aliunganisha udugu, kati ya Muhajirina kutoka Makka na Ansaar pale Madina, katika nyumba ya Anas bin Walikuwa watu sabini, nusu yao ni katika Muhajirina, na nusu ni katika Answar, alifanya udugu kati yao kwa kuliwazana na walikubaliana kurithiana baada ya kufa, hali hii iliindelea mpaka wakati wa vita vya Badri, Mwenyezi Mungu (ﷻ) Alipoterenisha Maneno haya:-

 وَأُوْلُواْ ٱلۡأَرۡحَامِ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلَىٰ بِبَعۡضٖ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِۚ

“Na ndugu wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (katika kurithiana. Ndio ilivyo) katika kitabu cha Mwenyezi Mungu.. .” (8:75) ‘
Imeelezwa pia kuwa alijenga udugu kati ya Muhajirina wenyewe kwa wenyewe na baadhi kufanya udugu wa pili, na kauli iliyo madhubuti ni ile ya kwanza. Muhajirina walikuwa wametosheka na udugu wa Kiislamu, udugu wa mji, na udugu wa kuzaliwa. (1)
Kama alivyosema Muhammad Al-Ghazaly, ”Maana ya udugu huu ilikuwé ni kuyayuka kwa ung’ang’anizi wa kijahilia na kuporomoka kwa tofaufi za uzawa, rangi na nghi. Kukawa hakuna, heshima, utukufu na ari isipokuwa kwa ajili ya Uislamu; na kwa sababu hiyo ikawa hatangulizwi mtu yeyote wala hawekwi nyuma isipokuwa kwa murua wake, na uchamungu wake.

Kwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu () aliufanya udugu huu kuwa ni mkataba uliopitishwa nakutekelezwa, na sio tamko lililokosa utekelezwaji; na aliufanya udugu huu kitendo kinachofumgamana na damu na mali, siyo maamkizi ambayo zinaporoja kwayo ndimi na haisimami kwayo athari yoyote.

Hali ya udugu wa Kiislamu na hisia za kumjali mwenzake ziliondoa ubinafsi katika mioyo ya Waislamu na kuza matumda mazuri (2)  Kwa mfano, Saad bin Rabia (Radhi za Allah ziwe juu yake) – Answaar, alirnwambia nduguye Abdur-Rahman bin Awf (Radhi za Allah ziwe juu yake);

”Mie ni tajiri sana miongoni mwa Answaar. Nina furaha kugawana nawe mali yangu nusu kwa nusu. Nina wake wawili, niko tayari kumtaliki mmoja na baada ya kuisha eda yake umwoe. Lakini Abdur Rahman bin Awf hakuwa tayari kupokea chochote, si mali wala nyumba. Alimshukuru nduguye na akamwambia, ”Tafadhali nielekeze sokoni ili nipate kuchuma kwa mikono yangu.” Alifanikiwa katika shughuli zake na akaweza kuoa baada ya muda mfupi.

Akafululiza kutoka wakati wa asubuhi kwa kipindi kirefu na siku moja akaja akiwa na alama ya umanjano; Mtume () akamuuliza, ‘Ni lipi lililokuzukia?.’ Akajibu, ’Nimeoa.’ Akamuuliza, Ni kiasi gani umempa mke?.’ Akajibu, ’Kipande cha dhahabu (mfano wa Kokwa la tende). (3)

Imepokewa kutoka kwa‘ Abu Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa amesemh; ”Answar walimwambia Mtume () agawe kati yao na Muhajirina mitende, sawa kwa sawa, Mlume () aliona wasitoe, hivyo akawaambia Muhajirina wafanye kazi kalika mashamba ya mitende na Ansaar, na wagawane mavuno sawa kwa sawa. Wakasema, ”Tumesikia na tumetii  (4)
Kitendo hiki kinatufahamisha jinsi Answari walivyokuwa na moyo wa ukarimu kwa ndugu zao Muhajirina na kuwa tayari kutoa wanavyovipenda kwa ajili ya ndugu zao katika Answari walitoa kipaumbele katika mambo yote yaliyo muhimu katika kuhakikisha kuwa Muhajirina hawapati shida isiyo ya lazima. Muhajirina kwa upande wao waliushukuru, waliuthamini na kuuheshimu ukarimu huu wa kweli kutoka
kwa ndugu zao. Walichukua kile kilichowatosha tu kuishi maisha ya kawaida.
Kwa ufupi ni kuwa sera hii ya udugu wa kipekee wa kisiasa ilijengwa kwenye misingi ya hekima kubwa
iliyosababisha kuleta uuumubuzi wa kiajabu wa matatizo yaliyokuwa yakiwakabili Waislamu.


1) Fiqhi Siim, Uk. 140-141..
2) Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 553.
3) Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 312

Begin typing your search above and press return to search.