AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Mwezi wa Ramadhani mwaka huo huo, Mtume (ﷺ) aliingia Haram Tukufu ambapo kulikuwa na kundi kubwa la Mushirikina wa Kikureshi, wakiwa pamoja na watu maarufu na mashuhuri. Mara akaanza kusoma Surat An-Najm (sura ya 41). Maneno ya heshima yanayotia moyo kutoka kwa Allah yalIshuka bila wao kutanabahi na mara yakawatia bumbuwazi. Ilikuwa mara yao ya kwanza kushitushwa na Ufunuo wa kweli. ilikuwa ni hila waliyoipendelea ya kukanusha Ufunuo, si kwamba hawakutaka kumsikiliza tu bali walizungumza kwa saufi ya juu na. yenyé dharau ilipokuwa Qur’ni inasomwa ili hata wasikilizaji wa kweli wasiweze kuisikia. Walikuwa wakidhani wanaififisha Sauti ya Allah (s.w.t); kwa-hakika walikuwa wakijikusanyia mateso tu;. kwani Sauti ya Allah (s.w.t) Haiwezi kuzimwa.
Wale wasioamini wanasema:-
لَا تَسْمَعُوا لِهَٰذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ
[Msiisikilize Qur’ani hii, na timueni zogo, huenda mkashinda.] (41:26)
Maneno ya Allah (s.w.t) yanayovutia sana yalingia katika mioyo yao. Waliingiwa na maneno wasiyoyatambua wala kuweza kuyapata katika ulimwengu wa kiyakinifu uliowazunguka. Wakakutwa katika hali ya usikivu wa Maneno Matakatifu kiasi ambacho Mtume (ﷺ) alipofikia
mwisho mapigo yao ya moyo yakawa yanaongezekaz Kisha Mtume (ﷺ) akasoma,
فَٱسۡجُدُواْۤ لِلَّهِۤ وَٱعۡبُدُواْ
[ Basi msujudieni Mwenyezi Mungu na mumuabudu.] (53:62). ]
Mushirlkina bila kujitambua na kwa kuridhia, walisujudu kwa unyenyekevu kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu (S.W.). Kwa hakika ulikuwa wakati wa shani, kwa ukweli uliopenya nyoyo shupavu za watu wenye kiburi na wafanya dhihaka. Walisimama kwa mshangao, walitambua kuwa Maneno ya Allah (s.w.t) yalikuwa yameteka mioyo yao na yalikuwa yamefanya kile ambacho walikuwa kukizuia na kukiangamiza.
Mushrikina wenzao ambao hawakuwepo katika tukio lile waliwalaumu sana, wakati huo huo wakaanza kuzua urongo na wakidai (yale maneno) yalitoka kwa Mfume (ﷺ) Walimsingizia pia kuwa aliyatukuza na kuyaheshimu masanamu yao na kuyapa uwezo wa kuombwa.
Juhudi zote hizi zililenga kutafuta udhuru wa kitendo chao cha kusujudu pamoja na Mtume (ﷺ) siku ile. Tabia za kipumbavu na tabia za uzushi zilikuwa pamoja na maisha yao ya kusema urongo na kubuni njama. (1)
Arraheeq Al Makhtuum Uk 161-162
(1) Tafhimul Qu’ani Juzuu 5, Uk. 188