AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Kusilimu kwa Hamza Bin Abdul Mutwalib: ‘Kafika hali hii ngumu iliyokuwepo ya udhalimu ulioshamiri, Nuru ilichomoza na kuonesha njia kwa waliokuwa wakidhulumiwa. Nuru ilichomoza kwa Hamza bin Abdul Mulwalib (Radhi za Allah ziwe juu yake) katika mwezi wa Dhul Hija mwishoni mwa mwaka wa sita wa Utume.
Imepokewa kuwa siku moja Mtume (ﷺ) alikuwa amekaa katika kituta Cha Mlima Swafa, Abu Jahl alimpita Mtume (ﷺ) akiwa akishutumu Dini aliyokuwa akiilingania. Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) hakujibu kitu isipokuwa alikaa kimya na kusikiliza tu. Kuona hivyo. Abu jahl aliokota jiwe na kumpiga Mtume (ﷺ) kichwani, Iikampasua na damu kutiririka. Baada ya hapo mshambuliaji akaondoka na kuelekea kwenye
genge la Makuraishi mbele ya Al-Ka’aba na kukaa pamoja nao.
Wakati hayo yakitendeka mjakazi wa Abdillah bin ]ad’aan alikuwa ndani ya Nyumba yake juu ya mlima wa Swafa: na aliyashuhudia yote yaliyotendeka. Hamza aliporudi kutoka katika uwindaji akiwa amevaa upinde wake, yule mjakazi akamueleza mambo yote ambayo Abu Jahl alikuwa ameyatenda kumtendea Mtume (ﷺ). Hamza akakasirika sana, (Hamza alikuwa ni mtu anayeheshimika na mshupavu mno miongoni mwa vijana wa Kikuraishi), baada ya kupewa taarifa hizo, alitoka akiwa na dhamira ya kumtafuta Abu Jahl na alikusudia kuwa akikutana nae atamshambulia.
Alimkuta msikitini na kumsimamia, na kisha kumwambia; “Wewe unamshutmnu mtoto wa ndugu yangu na hali mimi ni miongoni mwa Watu wanaofuata Dini yake?.” Hakusubiri jibu, akampiga kwa upinde na kumpasua vibaya kabisa. Kwa kitendo hicho Watu Wa kabila la Banu Makhzoum, kabila la Abu Jahl wakahamaki, na kwa upande mwingine wakahamaki Banu Hashim, watu wa kabila la Hamza.
Abu Jahl alipoona hivyo alisema; “Mwacheni Abu ’Ammar kwani mimi nimemtukana mtoto wa ndugu yake matusi mabaya sana.” (1)
Inaelezwa kuwa matamshi ya mwanzo aliyotatumia Hamza wakati akimkabili Abu Jahl, yalionyesha wazi kabisa jinsi ambavyo hakuwa tayari kuona Mtume (ﷺ) akinyanyaswa. Tangu mwanzo, kusilimu kwa Hamza kulikuwa ni kwa mtu aliyekataa kudhalilishwa kwa jamaa yake, baada ya hapo Mwenyezi Mungu (Subhanahu wataala) Aliukunjua moyo wake akashikamana na kamba madhubuti.(2)
na nguvu ya Waislamu ikaongezeka maradufu
1) Mukhtasar Arrasuul Uk 66. Mukhtasar Sira Uk 135
Rah matul alamiin Juzuu 1, Uk 68 Ibnu Hisham Juuzu1, Uk 261
2) Mukhtasar Arrasuul , Uk 101