KUJITOLEA MUHANGA WAKATI WA HIJRA YA BWANA MTUME ﷺ
Alipohama Mtume ﷺ kutoka Makkah kwenda Madinah alimwambia Ali (r.a.) alale kwenye kitanda chake na ajifunike shuka yake. Akawa ‘Ali ameweka mfano mwema katika kujitolea, imani na ikhlasi, Kisha ‘Ali (r.a.) akabakia Makkah kwa muda wa siku tatu ili kurudisha amana za watu ambazo zilikuwa kwa Mtume ﷺ.
Alipomaliza, kuregesha akatoka Makkah, akawa anatembea usiku na kupumzika mchana mpaka akawasili Madinah. Nyayo zake zilikatika katika kwa sababu ya kutembea sana. Alipowasili Madinah alifikia kwa Kulthum ibn AI-Hadam mjini Qubaa. Na huko ndiko alikoshukia Mtume ﷺ alipotoka Makkah. Alipojua Mtume ﷺ kuwasili kwa ‘Ali (r.a.) alisema: “Niitieni ‘Ali Akaambiwa: ” Ali hawezi kutembea kwa sababu ya maumivu ya kutembea.” Mtume ﷺ akaja mpaka kwa ‘Ali (r.a.) na kumkumbatia kisha -akalia kwa sababu ya kumsikitikia ‘Ali (r.a.) kwa kufura miguu yake. Mtume ﷺ akatia mate mikono yake akapitishia juu ya miguu ya ‘Ali (r.a.). Toka siku hiyo ‘Ali (r.a.) hakuumwa na miguu mpaka alipouawa. [Al-Kamil Juz. 2 uk.75]
*Al Khulaafau Arrashidun 129-130