June 17, 2021
0 Comments
KUHAMA KWA ABU BAKAR (RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE) KUELEKEA MADINAH
Mtume ﷺ alipowaamrisha Masahaba wake kuhamia Madinah, wakaanza kuhama, Abu Bakar (r.a.) alienda kwa Mtume ﷺ kumuomba ruhusa ya kuhama. Mtume ﷺ akamuamuru asubiri huku akitaraji kupata ruhusa ya kuhama ili wapate kuhama pamoja.Na muda aliporuhusiwa, walihama pamoja. Mwenyezi Mungu ameashiria jambo hilo aliposema:
{إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّهَ مَعَنَا}
[Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Mwenyezi Mungu alikwisha mnusuru walipo mtoa walio kufuru, naye ni wa pili katika wawili walipo kuwa katika pango, naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.]
[9:40]