KUCHUNGA MBUZI ﷺ
Mtume ﷺ alikuwa hana kazi maalumu mwanzoni mwa ujana wake, isipokuwa imepokelewa kuwa alikuwa akichunga mbuzi kwa Banu Saad na mbuzi wengine wa watu wa Makka kwa malipo maalumnu.(1)
Na Manabii wote waliwahi kuchunga mbuzi,Asema Mtume ﷺ:
ما بعث الله نبياً إلا رعى الغنمَ] فقال أصحابهُ: وأنت؟ قال : [ نعم، كنت أرعاها على قراريط لأهلِ مكةَ] رواه البخاري]
[Mwenyezi Mungu hakutumiliza Mtume ila alichunga Mbuzi,] wakasema Maswahaba je na wewe? akasema [Ndio nilikuwa nikichunga mbuzi kwa vijipeni kwa watu Makka] [Imepokewa na Bukhari]
Nawanazuoni wameelezea hikma ya Manabii kuchunga mbuzi,ili waweze kuwa na unyeyekevu,na kustahimili katika kuwachunga wanyama hawa kwa kuweza kuwatafutia lisho bora,na kumchunga alie dhaifu katika wanyama hao,ipate kuwa ni kama chanzo cha kuweza kutahimili na majuku atakapokuwa amepewa utume na kuongoza binaadamu.
1) Ibnu Hisham, uzuu 1, Uk. 187-188