131 – MLANGO: FADHILA YA KUTOA SALAMU NA AMRI YA KUISAMBAZA
كتَاب السَّلاَم
١٣١- باب فضل السلام والأمر بإفشائه
قَالَ الله تَعَالَى: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَدْخُلُوا بُيُوتاً غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّى تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَى أَهْلِهَا} [النور: ٢٧] .
وقال تَعَالَى: {فَإذَا دَخَلْتُمْ بُيُوتاً فَسَلِّمُوا عَلَى أنْفُسِكُمْ تَحِيَّةً مِنْ عِنْدِ اللهِ مُبَارَكَةً طَيِّبَةً} [النور: ٦١]
وقال تَعَالَى: {وَإِذَا حُيِّيتُمْ بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا} [النساء: ٨٦]
وقال تَعَالَى: {هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلاماً قَالَ سَلامٌ} [الذاريات: ٢٥,٢٤]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
KITABU CHA KUTOA SALAMU
131 – MLANGO: FADHILA YA KUTOA SALAMU NA AMRI YA KUISAMBAZA
Amesema Menyezi Mungu Mtukufu : “Enyi mlioamini! Msiingie nyumba zisizo nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na muwatolee salamu wenyewe.” [24:27].
Amesema Menyezi Mungu Mtukufua: “Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu, kuwa ni maamkio yanayotoka kwa Allâh, yenye baraka na mema.” [24:61].
Amesema Menyezi Mungu Mtukufu: “Na mnapoamkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo.” [4:86].
Allâh Amesema: “Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrâhîm wanaohishimiwa? Walipoingia kwake wakasema: Salama!” [51:24, 25].
.