June 25, 2021
0 Comments
KIPINDI CHA KUKATIKA KWA WAHYI
Ibni Saad amepokea kutoka kwa ‘lbn Abbas maneno yaliyohusu “kukatika kwa Wahyi ambayo’ kimsingi yanafahamisha kuwa kipindi hicho kilikuwa ni cha siku nyingi. Baada ya uchunguzi wa kina imeonekana kuwa maelezo haya ndiyo yenye nguvu.
Ama yale ambayo yametangaa miongoni mwa watu kuwa ukatikaji wa wahyi uliendelea kwa muda wote wa miaka mitatu au miaka miwili na nusu si kauli sahihi kwa hali zote, lakini hapa hatutoeleza suala hilo.
Siku za kukatika kwa Wahyi zilikuwa ni za huzuni kubwa kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ, zikiambatana na mastaajabu na mfadhaiko.*
*Arraheeq Al Makhtum Uk 107