0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

JUU YA MLIMA SWAFAA

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Baada ya Mtume kuwa na uhakika kutokana na ahadi ya Abu Twalib kuwa atamhami, wakati akifikisha ujumbe kutoka kwa Mola wake. Siku moja alisimama juu ya Jabali la Swafa, akipiga kelele kwa kusema; Tee asubuhi!’ zikakusanyika koo za Makuraishi, walipokusanyika akawanasihi katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu , na kuuamini ujumbe wake;. na kuamini siku ya mwisho. 

Bukhari amepokea sehemu ya kisa hiki, kutoka kwa Ibn Abbas Radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: lliposhuka aya hii.

{وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ}

[Na waonye Jamaa zako walio karibu (nawe).]   [26:214].
Mtume alipanda juu ya Jabali Swafa, akawa anatoa ulingano,

يا بني فهر، يا بني عدى، يا بني فلان، يا بني فلان
يا بني عبد مناف، يا بني عبد المطلب

[Enyi Banu Fihri, Enyi Banu Adiy, … ‘

aliziita Koo za Makuraishi, mpaka wote wakahudhuria na kwa wale ambao hawakuweza kufika wenyewe walituma ujumbe kwenda kuangalia kuna nini? 

Abu Lahab alihudhuria na Makuraishi. Naye Mtume  akauliza: 

أرأيتكم لو أخبرتكم أن خيلا بالوادي تريد أن تغير عليكم أكنتم مصدقي قالوا نعم ما جربنا عليك إلا صدقا قال فإني نذير لكم بين يدي عذاب شديد

[Hivi mnaonaje kama ningeioaeleza kuwa wako Farasi katika jangwa hili wanajiandaa kuwavamia, je, mngeniamini? Wote kwa pamoja wakajibu, ‘ndiyo’, maana hatujawahi kusikia kutoka kwako isipokuwa ukweli tu. Akasema; ‘Hakika mimi ni mkhofishaji niliyetumwa kwenu kuhusu siku ya adhabu kali,]

Abu Lahab akamwapiza, ‘Maangamivu ni yako siku yote hii, hivi ni kwa ajili hii tu ndio umetukusanya hapa?’ Hapo Mwenyezi Mungu Akateremsha aya ya Quran iliyoarifu:

تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ

[Pana kuangamia mikono miwili ya Abu Lahab! Naye amekwisha angamia.]   [111: 1] (1)

Muslim naye amepokea sehemu nyingine ya kisa hiki, kutoka kwa Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye amesema wakati iliposhuka aya hii:

{وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ}

[Na waonye jamaa zako toaliokaribu.]    [26:214] 

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwaita ndugu na jamaa zake na akawausia kwa kuwaeleza:

يا معشر قريش أنقذوا أنفسكم من النار، يا معشر بني كعب أنقذوا أنفسكم من النار، يا معشر بني هاشم أنقذوا أنفسكم من النار، يا معشر بني عبد المطلب أنقذوا أنفسكم من النار، يا فاطمة بنت محمد أنقذي نفسك من النار، فإني والله لا أملك لكم من الله شيئا، إلا أن لكم رحما سأبلها ببلائها

[Enyi Makuraishi, ziokoeni nafsi zenu na moto wa jahanamu, Enyi jamaa katika Banu Kaab, ziokoeni nafsi zenu na moto, Enyi jamaa katika Haashim, ziokoeni nafsi zenu na moto Enyi jamaa katika Banu Abdul Muttwalib, ziokoeni nafsi zenu na moto Ewe Fatima binti Muhammad iokoe nafsiyako na moto, kwani kwa hakika Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu ﷻ siwezi kuwasaidia nyinyi (katika kukuokoeni na adhabu za Mwenyezi Mungu) , isipokuwa nyinyi ni ndugu zangu ambao mimi nitauunga udugu 
huo. ]
(2)

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alianza kufikisha ujumbe kwa watu walio karibu naye zaidi, na aliwaeleza wazi kuwa kuukubali kwao ujumbe huu ndio uhai wa mahusiano kati yao na kati yake, na kuwa kamba ya udugu na mategemeo yao katika walichokuwa wakikiamini yameyeyuka kutokana na hali hii iliyojitokeza ya mafundisho mapya yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu .


1) Sahihil Bukhari, [uzuu 2, Uk. 702, 743. Sahihil Muslim, Juzuu 1, Uk. 114.

2) Sahihil Muslim, Juzuu I, Uk.114. Sahihil Bukhari, [uzuu I, Uk. 385. [uzuu 2, 

Uk. 702. Mishkatil Masabih, Juzuu 2, Uk. 460.

* Arraheeq Al Makhtum 128-129


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.