Swali: Je, inaruhusiwa kulipa siku za Ayamu al-Bidhi ikiwa mtu anaanza kuzifunga kisha akazuiliwa na jambo fulani na kuacha kufunga?
Jawabu: Inafaa kwa muumini mwanamume au mwanamke kufunga siku tatu kila mwezi, na ikiwa atazifunga katika siku za Ayamu al-Bidhi (siku nyeupe), basi hiyo ni bora zaidi. Lakini ikiwa atazifunga siku nyingine yoyote ya mwezi huo, inatosha, kwa sababu Mtume aliusia kufunga kila mwezi siku tatu, na akabainisha kuwa kufunga siku za Ayamu al-Bidhi (Masiku meupe) ni bora zaidi kuliko siku nyingine. Kwa hiyo, ikiwa mwanamume au mwanamke anafunga siku za Ayamu al-Bidhi, kisha wakazuiliwa kufunga kwa sababu ya jambo fulani, wanaruhusiwa kufunga siku nyingine yoyote ya mwezi, na Alhamdulillah. Wala hii haitwi kuwa ni kulipa kwa kuwa mwezi wote ni wakati unaofaa kwa kufunga kuanzia mwanzoni hadi mwisho wake. Kwa hiyo, ikiwa muumini mwanamume au mwanamke atafunga siku tatu mwanzoni, katikati au mwishoni mwa mwezi, atakuwa amepata lengo na kupata thawabu za Sunna, hata kama hakuzifunga siku za Ayamu al-Bidhi.
Chanzo: Fatawa Sheikh Ibnu Baaz (Allah amrahamu