NI IPI ITIKADI YA UDONGO WANAYOAMINI MASHIA?
Makusudio ya udongo katika itikadi ya Raafidhwah, ni udongo wa kaburi ya Husayn (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza mmoja wa wapotevu miongoni mwao aitwae Muhammad An-Nu’umaan Al-Haarithiy, ambae wanamuita ‘Ash-Shaykh Al-Mufiyd’ katika kitabu chake ‘Al-Mazaar’ imepokewa kutoka kwa Abu ´Abdillaah kwamba amesema: “Katika udongo wa kaburi ya Husayn, kunapatikana ponyo la kila maradhi, nao ndio dawa iliyo kubwa kabisa.”
Na amesema ´Abdullaah: “Wafanyieni tahniki (yaani watilieni mdomoni mara tu baada ya kuzaliwa kwao) watoto wenu kwa udongo wa kaburi la Husayn.”
Na akasema vilevile: “Alitumiwa ´Abdul-Husayn Ar-Ridhwaa mzigo (furushi la nguo) kutoka Khurasaan ndani yake mkiwa na udongo, akaulizwa alietumwa mzigo huo, ni kitu gani hiki? Akasema: “Huu ni udongo kutoka katika kaburi la Husayn.”
Hapakuwa panatumwa mzigo wowote isipokuwa ndani yake panawekwa udongo, anasema: Udongo huu ni amani kwa idhini ya Allaah.
Na inasemakana kwamba mtu mmoja alimuuliza Asw-Swaadiq (Abu ‘Abdillaah) kuhusu kutumia udongo wa kaburi la Husayn, akajibu kumwambia: Pindi utakapoula basi sema hivi: “Ewe Mola wangu hakika mimi nakuomba kwa haki ya ufalme ulioushika, na kwa haki ya Mtume aliyehifahiwa, nakuomba umpe Rahma Muhammad (ﷺ) pamoja na watu wa nyumba yake, na Ujaalie udongo huu kuwa ni ponyo la kila ugonjwa, na uwe ni kitulizo cha amani kutokana na kila khofu, na ni ulinzi kutokana na kila baya.”
Pia Raafidhwah wanadai kwamba, Mashia wameumbwa kwa udongo maalum, na Sunni wameumbwa kwa udongo mwengine kisha ukachanganywa udongo huo wote, basi maasi na maovu yanayofanya Mshia yeyote ni kutokana na athari ya udongo walioumbiwa Masunni. Na kheri na uongofu anaekuwanayo Sunni yeyote ni kutokana na athari za Udongo walioumbwa Shia. Pindi itakapofika siku ya Qiyaamah, basi maovu ya Mashia watabebeshwa Masunni, na mema ya Masunni watapewa Shia. (1) *
1) ‘Ilalu Ash-Sharaai’ uk. 490-491. Bihaarul-Anwaar 5/247-248.
* * MIONGONI MWA ITIKADI ZA MASHIA ‘Abdullaah Bin Muhammad As- Salafiy Uk / 25