June 16, 2021
0 Comments
HUKMU YA KUITIKIA SALAMU KATIKA SEHEMU ZA KUTAWADHIA ZILO KARIBIANA NA CHOO
Swali: Ni ipi hukumu ya kumsalimia mtu akiwa katika sehemu ya kutawadhia ambapo pako karibu na choo?
Jawabu: Choo ni sehemu iliokusudiwa kukidhia haja. Kwa sababu ni sehemu mtu anakuwa peke yake na haonekaniwi na watu. Lakini akiwa kandoka yuko sehemu ya kutawadhia basi yafaa kuitikia salamu wala haihisabiwi kuwa yuko chooni hata kama choo kiko karibu na yeye. Vile vile yuwafaa kutoa salamu na kupiga Bismallahi wakati wa kutawadha.
Na Allah ndie mjuzi zaidi.