0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

HISHIMA YA MWANAMKE KATIKA UISLAMU

HISHIMA YA MWANAMKE KATIKA UISLAMU

Ndugu katika imani, suala la mwanamke ni suala ambalo liliwashughulisha watu wengi walio pita, na linaendelea kuwashughulisha wengi katika zama zetu hizi. Dini na mila mbalimbali zimezungumzia hali ya mwanamke katika jamii. Wasomi wa elimu na falsafa tafauti wamejaribu kuzungumzia cheo cha mwanamke katika jamii. Lakini kila kundi linajaribu kumzungumzia mwanamke kwa misingi ya kufikia malengo yao. Katika Makala haya tutajaribu kuangazia cheo cha mwanamke katika jamii mbalimbali. Tutaangalia hali ya mwanamke kabla ya kuja Uislamu, na hali yake katika Uislamu, na hali yake katika mataifa ya magharibi.

HALI YA MWANAMKE KABLA YA UISLAMU

Alikuwa mwanamke katika zama za ujinga akionekana kama bidhaa ambayo haina thamani. Kila mtu anaweza kumiliki bidhaa hiyo wakati wowote.
Wanaume wakioa wanawake bila ya idadi maulumu na kuacha bila ya idadi ya talaka. Mwanamke haruhusiwi kumiliki chochote, hana haki ya kurithi, anaweza kuolewa na zaidi ya mume mmoja. Mwanamke hakuwa na cheo katika jamii ya ujahiliyah, bali alikuwa akionekana ni mtu anayeleta aibu katika jamii. Ikafikia hali hiyo, baadhi ya wanaume kuwazika mabanati wao wakiwa wadogo kuogopea kuleta aibu katika jamii. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Anatueleza hali ya mwanamke Akisema:

{وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِالْأُنثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ يَتَوَارَىٰ مِنَ الْقَوْمِ مِن سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمْسِكُهُ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ}     النحل:58

[Na mmoja katika wao anapopewa khabari ya kuzaliwa mtoto wa kike, unabadilika uso wake huwa mweusi na akajaa sikitiko. Anajificha na watu kwa sababu ya khabari mbaya ile alioambiwa. (anafanya shauri) Je, akae naye juu ya fedheha hiyo, au amfukie udongoni. Ni mbaya mno hukumu yao hiyo].   [Al-Nnahl:58]

Hii ndio hali halisi ya mwanamke kabla ya kuja Dini ya kislamu. Na hali hii ilikuwa sawa katika mataifa yote, sawa taifa la kiarabu na wasiokuwa waarabu.

HALI YA MWANAMKE KATIKA UISLAMU

Baada ya mwanamke kuishi katika dhulma kwa muda mrefu, bila ya kupata haki zake. Allah Subhaanahu wa Taala Alimtumiliza Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam kuja kumkomboa mwanamke na dhulma na udhalilifu alikuwa akipata kutoka katika jamii anayo ishi. Dini ya Kiislamu inamtukuza mwanamke na inampa haki zake zote katika jamii. Miongoni mwa haki hizo:-
Mwanamke sawa na mwanamume katika kutekeleza majukumu ya Dini. Amesema Allah Subhaanahu wa Taala:

{مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ}    النحل:97}

[Wafanyaji mema, wanaume au wanawake, hali ya kuwa ni Waislamu, tutawahuisha maisha mema, na tutawapa ujira wao mkubwa kabisa].      [Al-Nnahl:97]

Na Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala alimfadhilisha mwanamume kuliko mwanamke katika baadhi ya mambo, kwasababu ya majukumu mazito ya mwanamume katika kusimamia familia.
Mwanamke anastahiki kurithi. Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amesema:

لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا}  النساء:7}

[Wanaume wana sehemu katika mali wanayoacha wazazi wao na jamaa walio karibu. Na wanawake pia wanayo sehemu katika yale waliyaacha wazazi wao na jamaa walio karibu. Sawa yakiwa kidogo au mengi. Ni sehemu zilizofaridhishiwa (na Mwenyezi Mungu]. [Al-Nnisaa:7]
Mwanamke ana haki ya kuchagua mume wa kumwoa. Hawezi kuolewa bila ya ridhaa yake. Kinyume na zama za jahiliyah, mwanamke alikuwa ni bidhaa na chombo cha starehe kila mtu anakichukuwa kwa thamani ndogo, na kwa lengo la kutekeleza matamanio yake.
Mwanamke ana haki ya kujikomboa kutokana na mume dhalimu. Sheria ya kiislamu imempatia mwanamke haki ya kutoa talaka kwa mwanamume mwenye tabia mbaya, mwenye kumnyima mkewe haki zake.
Haya ni baadhi ya mambo muhimu mabao mwanamke amepewa katika Dini ya kiislamu. Na hii ndio hali halisi ya mwanamke katika Uislamu. Uislamu ulimrejeshea mwanamke hadhi na utukufu wake katika jamii, na ikatambua mchango wake mkubwa katika kuandaa kizazi cha kesho na kulea viongozi wa kusimamia Dini ya kislamu. Amesema Mtume ﷺ katika Hija:

اتقوا الله في النساء فإنهن عوان عندكم]       رواه مسلم]

[Mcheni Mwenyezi Mungu katika kuwasimamia wanawake, kwa sababu wao ni wasaidizi wenu].     [Imepokewa na Muslim]

Mtume ﷺ anaweka wazi cheo cha mwanamke nacho ni wasaidizi wa wanaume, sio mtumwa au mtumishi kama wanavyomdai watu wengine kwamba uislamu umemfanya mwanamke kuwa ni mtumwa hana haki yoyote katika jamii.

SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH ABUU HAMZA

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.