0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

HALI YA WAARABU KABLA YA UISLAMU

HALI YA WAARABU KABLA YA UISLAMU


 Ukitaka kujua ubora wa Uislamu,basi kwanza ni uje hali ya warabu namna walivyo kuwa wakiishi kabla ya Uislamu,katika nja zote za kimaisha.

Kabla ya Uislamu waarabu walizama mno katika ibada ya masanamu mpaka wakaijaza Al-Kaaba masanamu ambayo idadi yake ilifikia masanamu mia tatu na sitini (360).

Kila kabila lilikuwa na sanamu lake pekee na kila kaya/familia ilikuwa na sanamu malum kwa ajili ya familia hiyo tu.

Mtu alipotaka kusafiri, alilichukua safarini sanamu moja ilikufanikiwa safarini na walikuwa wakiyatakasa na kuyatukuza masanamu haya kiasi cha kuyatolea Qurubaani na dhabihu (sadaka za kuteketeza).

Waarabu walipokuwa wakitaka ushauri katika mambo yao mfano ndoa, biashara au safari basi uliendea “Hubal” sanamu lililokuwa ndani ya Al-kaaba wakampa ngamia na dir-ham mia mshika kete ambazo moja ilikuwa imeandikwa juu yake maneno”Mungu wangu amenikataza” na ya pili “Mungu wangu ameniamrisha” ya tatu “Naam/Ndiyo” ya nne “Hapana”.

Jumla kete zilikuwa ni saba, mshika kete huzizungusha na kuzichanganya kisha akaitoa moja na kilichoandikwa juu yake ndio huwa amri iliyotoka kwa Mungu sanamu.

Ukabila ulikuwa ndio sera ya kila kabila, na kila kabila lilikuwa tayari kuilinda sera yake hiyo ya ukabila dhidi ya uadui wa wote ule kutoka makabila mengine kwa gharama yoyote ile.

Msimamo huu na sera hii ya ukabila ilisababisha mizozo, ugomvi na mapigano ya mara kwa mara baina ya makabila haya.

Kugombea vyanzo vya maji, machungo na kujifakharisha kwa nasabu pia vilichochea kwa kiasi kikubwa mizozo na mapigano.

Kama ambavyo watu hutofautiana katika vyeo/hadhi, kazi na hali za kimaisha, Waarabu pia waligawanyika katika matabaka yafuatayo:

1. Mabwana/Viongozi: hawa ndio waliokuwa na mamlaka juu ya wengine na hatamu za uongozi zilikuwa chini yao.

2. Makuhani: hawa walikuwa ndio viongozi wa kidini wakiyatawalia mambo yote yanayohusu dini ikiwa ni pamoja na ibada, sherehe za kidini na mengineyo.

3. Wafanyabiashara: hawa walijishughulisha na usambaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya maeneo yao.

4. Wachungaji: hawa ndio waliokuwa wakijishughulisha na uchungaji wa wanyama na kazi ya kilimo kwa kiasi fulani.

Ama kwa upande wa kitabia,Waarabu za jahilia kama walivyo watu wa zama hizi walikuwa na tabia nzuri na nyingine mbaya.

Miongoni mwa tabia njema walizokuwa nazo ni kama vile ukarimu, murua, ushujaa na utekelezaji wa ahadi.

Tabia mbaya zilizoitawala jamii ile ni pamoja na ulevi, uchezaji wa kamari, ulaji riba na kuwazika watoto wa kike wakiwa hai kama ilivyoelezwa na Qur-ani:

وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ  بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ}    التكوير:8-9}

[Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa, Kwa kosa gani aliuliwa?]    [81:8-9]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.