0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

HALI YA VIKOSI HIVI ILIKUWA KAMA IFUATAVYO

Hali ya Vikosi Hivi Ilikuwa kama Ifuatavyo:
1) Kikosi cha Saifu Al-Bahri, Mnamo mwezi wa Ramadhani mwaka wa 1 A.H., sawa na mwaka 623 C.E, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () alimpa uongozi wa kikosi hiki Hamza bin Abdi Al-Muttalib (Radhi za Allah ziwe juu yake) na aliongoza watu thelathini katika Muhajirina. Alitumwa akazuie msafara wa kibiashara wa Makuraishi uliokuwa ukitoka Sham. Katika msafara huo alikuwemo Abu Iahli bin Hisham, akiwaongoza watu mia tatu. Walipofika Saiful-al-Bahri kwa upande wa Al-Idhi, wakakutana na wakapanga safu kwa ajili ya vita. Majdy bin Amru A-Juhani alikuwa ni rafiki wa makundi yote mawili, akawazuia kupigana. Hii ilikuwa ndiyo bendera ya kwanza ya vita iliyotungikwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (), ilikuwa nyeupe na alikabidhiwa Aba Marthad Kanazi bin Huswaini Al-Ghanawy kuibeba.
2) Kikosi cha Rabighi: Katika mwezi wa Shawwal mwakail A.H, mwafaka na mwezi wa April mwaka wa 623 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mungu () alimpeleka Ubaida bin al-Harith bin Abdul Muttalib (Radhi za Allah ziwe juu yake) akiongoza Muhujiriml sitini wakiwa na farasi, njiani wakakutana na Abu Sufyani akiwa
anaongoza kikosi cha watu mia -mbili katika jangwa la Rabighi. Makundi mawili haya yalitupiana mishale, lakini havikutokea vita. Katika kikosi hiki walijiunga watu wawili na Uislamu kutoka katika Jeshi la Makka; nao ni Al-Miqdadi bin Amri Al-Bahrani, na Utba bin Al-Maaziny. Walitoka pamoja na makafiri, ili hiyo ndiyo iwe njia ya kufika kwa Waislamu. Bendera ya Ubaida (Radhi za Allah ziwe juu yake) ilikuwa nyeupe na mbebaji wake alikuwa ni’ Mistani bin Athatha bin Al-Muttahb bin Abdil Manafi (Radhi za Allah ziwe juu yake).
3) Kikosi cha Al-Kharar, katika mwezi wa Dhulqa’duh mwaka wa 1 wa A.H. sawasawa na mwezi Mei mwaka 623 C .E. Mtume wa Mwenyezi Mungu () alimpeleka tena Sa’ad bin Abi Waqqasi (Radhi za Allah ziwe juu yake) akiwaongoza watu ishirini kwa leng la kuuzuia msafara wa kibiashara wa Makuraishi na akachukua
ahadi kutoka kwake kuwa asivuke Al-Kharrazi. Wakatoka hali ya kwenda usiku na wakijificha mchana. Walifika AL-Kharrazi asubuhi ya Alkhamisi, na wakakuta kuwa msafara umekwishapita kutoka siku iliyopita. Bendera ya Sa’ad (Radhi za Allah ziwe juu yake) ilikuwa nyeupe na mbebaji alikuwa ni Al-Miqdadi bin Amri (Radhi za Allah ziwe juu yake).
4) Ghazwa Al-Abwa, au Waddan: Katika mwezi wa Safar mwaka wa 2 A.H sawa na mwezi Agosti mwaka 623 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mungu () alitoka yeye mwenyewe baada ya kumfanya Sa’ad bin Ubada (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa Khalifa wa Madina, akiongoza kikosi cha watu sabini katika Muhajirina, alikwenda kwa madhumuni ya kuuzuia msafara wa biashara, mpaka wakafika Waddani bila kukutana na upinzani wowote.
Katika vita hivi Mtume () alifunga mkataba wa kusaidiana na Amru bin Makhashi Ad-Damari; aliyekuwa
kiongozi na Bwana wa Banu Dumari katika zama zake.
Mkataba ulikuwa kama ifuatavyo:-
Waraka huu kutoka kwa Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu () kwenda kwa Banu Dhamrah,
kuw amani ya mali zao na maisha yao. Kwamba wana haki ya kunusuriwa kwa atakaye wakusudia kwa
ubaya, isipukuwa watakapoipiga vita Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t); na kuwa Mtume () atakapowaita kwa ajili ya kumnusuru watamwitikia. (1)

Hivi ndivyo vita vya kwanza alivyopigana Mtume wa Mwenyezi Mungu ().

Mtume () alikaa nje ya Madina kwa siku kumi na tano, bemdera yaké ihikuwa nygupe na mchukuzi wa bendera hiyo alikuwa ni Hamza bin Abdil Muttalib (Radhi za Allah ziwe juu yake).
5) Vita vya Buwat; Ilipofika Rabiul Awwal mnamo mwaka wa 2 wa A.H. sawa na Septemba mwaka 623 C.E. Radhi za Allah ziwe juu yake wa Mwenyezi Mungu () alitoka akiongoza watu mia mbili katika Masahaba wake ili kuuvamia msafara wa biashara wa Makuraishi, akiwemo Umayya bin Khalaf, Jumahi na watu wengine mia moja katika Makuraishi, wakiwa na ngamia elfu mbili na mia tano. Alifika Buwat kwa upande wa Ridawi na
hakukutana na upinzani wowote. Katika vita hivi uongozi wa Madina alimwachia Sa’ad bin Muadhi (Radhi za Allah ziwe juu yake). Bendera yake ilikuwa nyeupe na mchukuzi wa bendera hiyo alikuwa ni Sa’ad bin Abu Waqqas (Radhi za Allah ziwe juu yake).
6) Vita vya Safwan; Ilipofika Rabiul Awwal mwaka wa 2 C.E. sawa na mwezi Septemba mwaka 623 C.E., Kurzi bin Jabir A17 Fihry alifanya mashambulizi akiwa na askari wachache kafika kikosi cha Mushirikina katika eneo la malisho ya wanyama wa Madina na akanyang’anya baadhi ya mifugo. Mtume wa Mwenyezi Mungu () alitoka akiwa na watu sabini katika Masahaba wake ili kumfukuza. Alifika mpaka katika jangwa
linaloitwa Safwan katika upande wa Badri, lakini Kurzi na wenzake hawakupatikana, na akarejea bila kupigana vita. Vita hivi vinajulikana kwa jina la vita vya Badri vya kwanza, na katika vita hivi uongozi wa Madina alipewa Zaid bin Haritha (Radhi za Allah ziwe juu yake), bendera ilikuwa nyeupe na mchukuzi wake alikuwa ni Ali bin Abu Twalib (Radhi za Allah ziwe juu yake).
7) Vita vya Dhil Ushairah; Katika mwezi wa Jumadal-al-Ula na Jumada-al-Akhirah mwaka wa 2 wa AH. sawa na Novemba na Desemba mwaka 623 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mungu () alitoka akiongoza watu mia moja na khamsini 150 na wengine wanasema kuwa walikuwa ni watu mia mbili 200 katika Muhajirina, waliotoka kwa hiari zao bila ya mtu yeyote kulazimishwa. Walitoka wakiwa na ngamia thalathini walokuwa wakiwapanda kwa zamu, na walitoka kwa lengo la kuingilia kati msafara wa biashara uliokuwa ukielekea Sham. Walikuwa wamekwisha pata khabari kupitia wapelelezi wake waliokuwa Makkah kuwa ndani ya msafara huo mna mali za Makuraishi. Alipofika mahali paitwapo Dhil Ushairah akapata khabari kuwa msafara Umekwishapita siku nyingi. Msafara huo ndiyo uliosababisha vita vya Badri Kuu.
Kulingana na mapokeo ya Ibn Ishaq, Mtume () alitoka mwishoni mwa Jamada-al-Ula, na kurejea mwanzoni mwa Jamadal Akhirah. Huenda hii ndiyo ikawa sababii ya watu wa somo la Sira kutofautiana katika kuainisha mwezi wa vita hivi.
Katika vita hivi Mtume wa Mwenyezi Mungu () alifunga mkataba wa kutofanyiana uadui na Banu Mudliji na washirika wao katika Banu Dhumra. Uongozi wa Madina katika vita hivi alipewa Abu Salama bin Abdil Assad Al-Makhzoumy (r.a). Bendera katika vita hivi ilikuwa ni nyeupe
na mbebaji wake alikuwa ni Hamza bin Abdil A1-Muttalib
(Radhi za Allah ziwe juu yake.)
8) Kikosi cha Nakhlah: Katika Mwezi wa Rajab mwaka wa pili AH. sawa na Januari mwaka 624 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mungu () alimpeleka Abdallah bin Jahshi Al- Assad (Radhi za Allah ziwe juu yake), kwenye mji wa Nakhlah akiwa anawaongoza watu kumi na wawili 12 katika Muhajirina, kila watu wawili
walipokezana kumpanda ngamia mmoja.

Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa amemuandikia barua na akamuamrisha kuwa» asiisome mpaka aenda mwendo wa siku mbili, kisha aisome. Kisha Abdullah akaenda baada ya siku mbili akaisoma, akakuta maneno yafuatayo: ”Utakapoyangalia maandishi yangu haya nenda mpaka Nakhlah kati ya Makka na Taif, ukatishe msafara wa biashara wa Makuraishi na kusanya khabari zao.” Akasema: “Nimesikia na nimetii.” Akawaeleza wenzake khabari hiyo, nakuwa yeye hawalazimishi kwa hiyo mwenye kupenda kufa shahidi (kufa katika vita vya kuitetea Dini ya Mwenyezi Mungu) na asimame, na mwenye kuichukia arudi. Ama mimi nina simama, wakasimama wote, isipokuwa Sa’ad bin Abi Waqqas
(Radhi za Allah ziwe juu yake) na Utba bin Ghazwan (Radhi za Allah ziwe juu yake) walimpoteza ngamia wao ambaye walikuwa wanapokezana kumpanda, wakabakia nyuma wakimtafuta.
Abdullah bin Jahshi (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikwenda mpaka akafika Nakhlah, ukapita msafara wa biashara wa Makuraishi ukiwa umebeba zabibu, ngozi na biashara zingine. Katika msafara huo alikuwepo Amri bin Al-Hadhramy, ’Uthman na Nawfal, watoto wawili wa Abdill-ah bin Al-Mughira, na Al-Hakam bin
Kisan, huru wa Banu Al-Mughirab Waislamu wakashauriana na wakasema: “Sisi tumo katika siku ya mwisho ya mwezi wa Rajab, mwezi mtukufu, iwapo tutapigana nao tutakuwa tumevunja heshima ya mwezi mtukufu na iwapo tutawaacha, usiku huu wataingia Haram.” Waliamua kupigana nao na Amri bin Al-Hadhrami aliuawa kwa kupigwa mshale. Wakamteka ’Uthmani na Al-Hakam. Nawfal aliponyoka.
Kisha wakafika na ule msafara na wale mateka wawili mpaka Madina, wakiwa wametenga katika mali hiyo khumsi (moja ya tano). Na hili ndilo likawa fungu la khumsi ya kwanza kutolewa katika Uislamu. Wakawa ni watu wa kwanza kuuawa katika Uislamu na wakawa ni mateka wawili wa mwanzo katika Uislamu.
Mtume wa Mwenyezi Mungu () alishutumu lile ambalo walilolifanya na akasema: “Sikuwaamrisha kupigana katika mwezi mtukufu”, akasimamisha kufanya jambo lolote kuhusu mali ya msafara na wale mateka wawili. Mushirikina walipata sababu ya kuwatuhumu Waislamu kuwa wao wamehalalisha yale ambayo Ameyaharamisha Mwenyezi Mungu. Maneno mengi ya hapa na pale yalizungumzwa
mpaka wahyi ukashuka uliotoa jawabu ambalo lilionyesha kwamba vitendo vya Mushirikina vilikuwa vibaya sana kuliko vitendo vya Waislamu :

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلشَّهۡرِ ٱلۡحَرَامِ قِتَالٖ فِيهِۖ قُلۡ قِتَالٞ فِيهِ كَبِيرٞۚ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَكُفۡرُۢ بِهِۦ وَٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ وَإِخۡرَاجُ أَهۡلِهِۦ مِنۡهُ أَكۡبَرُ عِندَ ٱللَّهِۚ وَٱلۡفِتۡنَةُ أَكۡبَرُ مِنَ ٱلۡقَتۡلِۗ 

Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa. Lakini kuzuilia watu wasende katika Njia ya Mwenyezi Mungu na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasende kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.” (2:217)
Kwa hakika wahyi huu umeweka wazi, kuwa mzozo ambao ulizushwa na Mushirikina ili kuleta mashaka katika mwendo wa wapiganaji Waislamu, mzozo huo hauna sababu yoyote ya kukubalika, kwani mambo yote matukufu na matakatifu yalikwisha vunjwa katika kuupiga vita Uislamu na kuwakandamiza waumini wake. Hivi Waislamu hawakuwa wakiishi katika mji mtukufu wa Makka? wakati walipoamua kuwanyang’anya mali zao na kutaka kumnuuwa Mtume wao?;
Sasa ni jambo gani ambalo limeyarejeshea haya mambo utukufu wake ghafla?; kukawa kuyavunja kwake ni fedheha?.
Kwa hakika madai ya Mushirikina ni madai yaliyojengwa juu ya ubaya na uchafu. Baada ya hapo, Mtume wa Mwenyezi Mungu () aliwaachia huru wale mateka wawili na akalipa fidia kwa mawalii wa wale watu wawili waliouliwa. (2)
Hivyo ndivyo vikosi vya uchunguzi na vita vilivyotokea kabla ya Badri, haukutokea uporaji wa mali wala uuaji katika vita hivyo isipokuwa baada ya yale ambayo waliyatenda Mushirikina katika uongozi wa Kurzi bin Iabir Al-Fihry. Utakuta mwanzo wa yote hayo unatokana na Mushirikina pamoja na yale ambayo walikuwa wameyafanya kabla ya hapo.
Baada ya kutokea yaliyotokea katika kikosi cha Abdillah bin Jahshi (Radhi za Allah ziwe juu yake) ilithibiti khofu ya Mushirikina, na wakaiona hatari ya kweli ikiwakabili. Wakajiingiza katika lile ambalo walikuwa wanaogopa kujihusisha nalo na wakajua kwamba Madina iko katika ulinzi madhubuti, na inafatilia harakati zao zote za biashara na kwamba Waislamu walikuwa na uwezo wa kwenda takriban umbali wa maili mia tatu, wakauwa watu na kuwateka wengine, na kuzichukua mali zao, na wakarudi hali ya kuwa wako salama wakiwa na ngawira.

Mushirikina walihisi kuwa biashara yao ya Sham iko hatarini. Badala ya kuzinduka na kuacha upotevu na kuishika njia ya wema na utulivu kama walivyofanya Juhaina na Banuu Dhumra, wao wakaongeza chuki na ghadhabu. Wakashikilia vigogo na wakubwa wao wengine juu ya yale ambayo walikuwa
wanakamiwa na wanatishwa kwayo huko nyuma. Miongoni mwa hayo ni kuwateketeza Waislamu katika mji wao, na huku ndiko kurukwa na akili ambako kuliwaleta Badri ili kupigana na Waislamu.
Ama kwa upande wa Waislamu, Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliwafaradhisha kupigana baada ya tukio la kikosi cha Abdillah bin Jahshi (Radhi za Allah ziwe juu yake), katika mwezi wa Shaaban, mwaka wa
2 A. H. na katika hilo Mwenyezi Mungu (s.w.t) Akateremsha
aya nyingi zilizowazi:

وَقَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يُقَٰتِلُونَكُمۡ وَلَا تَعۡتَدُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ  وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡ وَأَخۡرِجُوهُم مِّنۡ حَيۡثُ أَخۡرَجُوكُمۡۚ وَٱلۡفِتۡنَةُ أَشَدُّ مِنَ ٱلۡقَتۡلِۚ وَلَا تُقَٰتِلُوهُمۡ عِندَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَٰتِلُوكُمۡ فِيهِۖ فَإِن قَٰتَلُوكُمۡ فَٱقۡتُلُوهُمۡۗ كَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ  فَإِنِ ٱنتَهَوۡاْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ  وَقَٰتِلُوهُمۡ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتۡنَةٞ وَيَكُونَ ٱلدِّينُ لِلَّهِۖ فَإِنِ ٱنتَهَوۡاْ فَلَا عُدۡوَٰنَ إِلَّا عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ 
“Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.

Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.

Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu.
Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliteremsha aya za namna nyingine, anawafundisha namna ya kupigana, kuwahimiza na kuwawekea wazi baadhi ya hukumu:

فَإِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَضَرۡبَ ٱلرِّقَابِ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَثۡخَنتُمُوهُمۡ فَشُدُّواْ ٱلۡوَثَاقَ فَإِمَّا مَنَّۢا بَعۡدُ وَإِمَّا فِدَآءً حَتَّىٰ تَضَعَ ٱلۡحَرۡبُ أَوۡزَارَهَاۚ ذَٰلِكَۖ وَلَوۡ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَٱنتَصَرَ مِنۡهُمۡ وَلَٰكِن لِّيَبۡلُوَاْ بَعۡضَكُم بِبَعۡضٖۗ وَٱلَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَلَن يُضِلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ  سَيَهۡدِيهِمۡ وَيُصۡلِحُ بَالَهُمۡ  وَيُدۡخِلُهُمُ ٱلۡجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمۡ  يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تَنصُرُواْ ٱللَّهَ يَنصُرۡكُمۡ وَيُثَبِّتۡ أَقۡدَامَكُمۡ  

Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a’mali zao.

Atawaongoza na awatengezee hali yao. Na atawaingiza katika Pepo aliyo wajuulisha. Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” (47:47“ (3)

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) Amewataja kwa ubaya Wale ambao nyoyo zao zilitetemeka na kutaharuki wakati waliposikia imeteremka amri ya kupigana vita na maadui:

 فَإِذَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ مُّحۡكَمَةٞ وَذُكِرَ فِيهَا ٱلۡقِتَالُ رَأَيۡتَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ نَظَرَ ٱلۡمَغۡشِيِّ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡمَوۡتِۖ فَأَوۡلَىٰ لَهُمۡ  

”…Na inapo teremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake khabari ya vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anaye zimia kwa mauti. Basi ni bora kwao” (47: 20)
Kufaradhishwa vita na kufanya maandalizi kabla ya mapambano ni jambo lisiloepukika kutokana na hali
ilivyokuwa. Endapo kungekuwa na jemedari ambaye aliyatathmini mazingira yaliyokuwepo angewaamrisha askari wake wajiandae kwa vita sembuse Mola Aliye Mjuzi na Mtukufu.

Hivyo, mazingira yalikuwa yanalazimisha kutokea kwa mapambano ya kumwaga damu kati ya haki na batili.
Tukio la kikosi cha Abdillah bin Iahshi (Radhi za Allah ziwe juu yake) lilikuwa ni pigo kubwa liliondosha kiburi chao na likawaacha wanapinduka pinduka mfano wa kaa la moto.
Aya za kuamrisha vita zilifahamisha, kukaribia mapambano ya umwagaji damu na kuwa nusra na ushindi ni wa Waislamu. Tazama namna Mwenyezi Mungu () Alivyowaamrisha Waislamu kuwatoa Mushirikina mahali pale ambapo waliwatoa, na namna Anavyowafundisha jinsi askari atakavyowatendea mateka wake, na namna ya kumaliza nguvu za maadui mpaka vita vitakapokwisha. Hizi zote mpaka sasa ni ishara zenye kuonyesha ushindi kwa Waislamu, isipokuwa yote yalikuwa yamesitiriwa hadi atakapoonesha mtu binafsi uchungu wake.
Katika masiku haya, katika mwezi wa Shaaban mwakawa 2 A.H. sawa na Februari 624 C.E., Mwenyezi Mungu () Aliamrisha kugeuzwa kwa Qibla kutoka Baitul-Muqaddas na kuelekea Msikiti Mtukufu Wa Makka. Tukio hili liliwaathiri watu wenye imani dhaifu na wanafiki wa Kiyahudi ambao
walikuwa wameingia katika safu za Waislamu kwa madhumuni ya kuzusha machafuko. Walifichuka na walirejea kwenye yale waliyokuwa wakiyafanya. Hivyo ndivyo zilivyosafika safu za Waislamu, zikaondokana na udanganyifu na khiyana.
Qibla kugeuzwa ilikuwa ni ishara nzuri sana ya kuanza kwa Awamu mpya ya mapambano ya kukiteka Qibla hiki. Kwani ilikuwa muhali Qibla cha Waislamu kubaki mikononi mwa maadui zao. Baada ya maamrisho haya na ishara mbalimbali, Waislamu walizidisha hamasa, hali ya kupenda
Jihadi, kukutana na maadui katika vita vyenye kupambanua mambo ya haki na batili, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu () iliongozeka.


1) Al-Mawahibu Alladunniya, ]uzuu 1 Uk. 75.

2) Maelezo haya ya Ghazwa na Saraya, yamenukuliwa kutoka kitabu, Zaad Ma’ad, juzuu 2, Uk 83-85; Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 561-605. Rahmatun Lil ’Alamin, Juzuu 1, Uk. 115-116, Juzuu 2, Uk. 215-216, 468-470. Katika rejea hizi kuna tofauti za mtiririko wa kutajwa Saraya na Ghazawat. Rejea zetu
zimetegemea uhakiki wa Wanazuoni wawili Ibn Qayyim na Mansourpuri

3) Abu ‘Ala Maududi amehakiki na kusema kuwa Surntu Muhammad
imeteremka kabla ya Badr (Angalia, Tafhimul Qur’an, Iuzuu 5, Uk. 11-12).

Begin typing your search above and press return to search.