0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

HAKI ZA JIRANI

HAKI ZA JIRANI

Kila Muislamu anahitaji kujua jambo ambalo Jibril (A.S) hakuacha kumuusia Mtume ﷺ kuhusu jirani mpaka akadhani ana haki ya kurithi.

Jirani ana haki zinapaswa kulindwa na hizo haki za jirani huyo ni sawa awe Muislamu au Kafiri, mwema au muovu, rafiki au adui aliyekuwa karibu au mbali. Na kila mmoja ana daraja kuliko mwingine inazidi au inapungua kutokana na ukaribu wake, dini yake, tabia yake na ukaribu wake. Uislamu umeusia kuhusu jirani na kuhifadhi haki zake ambazo hazijatambuliwa na kanuni. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ :

{وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ}

[Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali,] [Al-Nnisaa:36]

Amepokea Ibn ‘Umar, amesema Mtume ﷺ:

[ما زال جبريل عليه السلام يوصيني بالجار حتى ظننت أنه سيورثه]   رواه البخاري ومسلم

[Hakuacha Jibril kuniusia kuhusu jirani mpaka nikadhani kuwa jirani atarithi]. [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na Amepokea Abu Huraira hadithi kutoka kwa Mtume ﷺ akisema:

من كان يؤمن بالله واليوم الآخر ، فليقل خيرا أو ليصمت ، ومن كان يؤمن بالله واليوم الآخر ، فليكرم جاره       رواه البخاري ومسلم

[Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho azungumze mambo ya kheri au anyamaze, na anayemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho amkirimu jirani yake].    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Amesema Sheikh Abu Muhammad: Kuhifadhi haki ya jirani ni katika kukamilika kwa Imani. Na watu katika zama za jahilia walikuwa wakihifadhi haki za jirani na wakiusia kwa kuwafanyia wema mfano kumpa zawadi, kumtolea salamu, kumuonyesha uso wa furaha na kujua hali yake na kumsaidia anacho kihitaji.

Amepokea Abu Huraira: ‘ Haki za Muislamu juu ya Muislamu mwenzake ni sita:-
Kumsalimia anapokutana naye
Kuitikia mwito anapokuita
Kupokea nasaha anapokuusia
Kumrehemu anapo chemua
Kumtembelea anapokuwa mgonjwa
Kufuata jeneza lake anapo kufa

TAHADHARI NA KUWAUDHI MAJIRANI

Ndugu Muislamu ni haramu kuudhi majirani. Mtume ﷺ amesema:

[مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ، فَلا يُؤْذِ جَارَهُ]    رواه البخاري ومسلم

[Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi asiudhi jirani zake].  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Imepokewa na Shureyh amesema ﷺ:

[والله لا يؤمن، والله لا يؤمن، والله لا يؤمن، قيل: من يا رسول الله؟ قال: [الذي لا يأمن جاره بوائقه]   متفق عليه

[Naapa kwa Mwenyezi Mungu Haamini! Haamini! Haamini! Akaulizwa: Nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni yule ambaye kwamba majirani zake hawasalimiki na shari zake].  [Imepokewa na Bukhari na Muslim].
Miongoni mwa sura za kuwaudhi majirani ni kuwaudhi watoto wake, kuchezea milki yake kuinua sauti kama ya nyimbo na kumpangisha mtu asiyeridhika nae.
Na kuwaudhi majirani kama kuwafanyia khiyana, kuwachunguza, kufuatilia aibu yake, kuangalia maharimu zake, kupitia dirisha lake au kumtembelea mke wake. Imetolewa onyo kali kutoka kwa Mtume ﷺ kwa mwenye kufuatilia aibu za jirani zake, Ibnu Masoud asema nilimuliza Mtume ﷺ Ni dhambi gani kubwa? Mtume akasema:

[أن تجعل لله ندّاً وهو خلقك، قلت: إن ذلك لعظيم . قلت: ثم أي ؟ قال: وأن تقتل ولدك تخاف أن يطعم معك، قلت: ثم أي ؟ قال: أن تزاني حليلة جارك ]     متفق عليه

[Ni kumjalia Mwenyezi Mungu, mshirika hali yakuwa yeye ndie aliekuumba] nikasema: bila shak hili ni jambo kubwa  nikasema kisha ni dhambi gani? Akasema Mtume: ni [kumuua mtoto wako kwa kuchelea kutomlisha,] nikasema kisha ni dhambi gani? Akasema [Ni kuzini na mke wajirani yako”. ]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim].

Amesema Mtume ﷺ:

[لأَنْ يَزْنِيَ الرَّجُلُ بِعَشْرِ نِسْوَةٍ ، أَيْسَرُ عَلَيْهِ مِنْ أَنْ يَزْنِيَ بِامْرَأَةِ جَارِهِ]     رواه البخاري في أدب المفرد

[Kuzini mtu na wanawake kumi ni (dhambi zake) ni nyepesi kuliko kuzini na mwanamke wa jirani yake].    [Imepokewa na Bukhari katika Adabul Mufrad]
Tumuogopeni Mwenyezi Mungu, kukhini Majirani ima kwa kuwapigia simu au kwa njia ya ujumbe au kwa njia ya kuangaliana. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:

{وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا}     الأحزاب:58

[Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri.]    [Al Ahzaab:58]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.