Kwa ajili ya kutekeleza mipango hii miwili, Waislamu walianza harakati za kijeshi kwa vitendo. Baada ya kushuka ruhusa ya kupigana, walisimama na kuanza harakati za kijeshi Wanahistoria wamelipa jina tukio lolote la mapigano ambalo Mtume (ﷺ) ameshiriki mwenyewe kuwa ni Ghazwa, na lile ambalo alituma
Masahaba wake bila kushiriki, Sariya.
zilizofanana na doria za upelelezi, kwa lengo la kutaka kujua hali ya njia zilizokuwa Madina na nyendo za
misafara ya kibiashara ya Makuraishi na mipango yao mingine ya kuwavamia. Pamoja na kuwekeana mikataba na watu wa makabila yaliyokuwa na makazi yao katika njia hizi.
Hekima ya yote haya pia ilikuwa ni kuwafahamisha Mushirikina wa Yathrib, Mayahudi na mabedui wa viunga vinavyoizunguuka Madina kuwa Waislamu sasa ni wenye nguvu na si wanyonge kama ilivyokuwa siku za niwanzo. Na pia kuwaonya Makuraishi uwezekano wa mwisho mbaya wa vurumai zao, ili wazinduke na kuachana na upotevu uliokuwa ukiwaelekeza shimoni.
Ilikuwa ni katika njia ya kuwapa tanbihi huenda wao wangehisi kuwepo kwahatari katika uchumi wao na njia za maisha yao na kwa hivyo kuelekea kwenye njia ya amani na kuizuia nia ya kutaka kupigana na Waislamu ndani ya mji wao, na kuacha kuwazuia watu kufuata njia ya Mwenyezi Mungu. (s.w.t) na kuacha kuwaadhibu wanyonge miongoni mwa waumini huko Makka ili Waislamu wawe huru katika kuufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika maeneo mbalimbali ya Bara Arabu.
November 20, 2025
0 Comments