Fadhila za Mwezi wa Allah Muharram
1- Ni miongoni mwa miezi mitukufu (Ash’hurul Hurum) Allah amesema:
إِنَّ عِدَّةَ ٱلشُّهُورِ عِندَ ٱللَّهِ ٱثۡنَا عَشَرَ شَهۡرٗا فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِ يَوۡمَ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ مِنۡهَآ أَرۡبَعَةٌ حُرُمٞۚ
“Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na miwili… katika hiyo ipo minne mitakatifu.” [At-Tawbah: 36]
Miezi hiyo mitukufu ni: Dhul-Qa’dah, Dhul-Hijjah, Muharram na Rajab Mwezi wa Muharram umeitwa hivyo kwa sababu ulikuwa ni mwezi mtukufu tangu zama za ujahili.
2- Ni mwezi bora zaidi wa kufunga baada ya Ramadhani
Mtume ﷺ amesema: “Funga bora baada ya Ramadhani ni kufunga mwezi wa Allah Muharram.” [Imepokewa na Muslim] Na kuitwa “mwezi wa Allah” ni ishara ya heshima na utukufu mkubwa.
3- Ndani yake kuna siku ya Ashuraa Siku ya kumi ya Muharram huitwa Ashuraana ni siku yenye daraja kubwa. Ibn ‘Abbas amesema:
عن عبد الله بن عباس -رضي الله عنه- أنّه قال: (ما رَأَيْتُ النبيَّ صَلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ يَتَحَرَّى صِيَامَ يَومٍ فَضَّلَهُ علَى غيرِهِ إلَّا هذا اليَومَ، يَومَ عَاشُورَاءَ، وهذا الشَّهْرَ يَعْنِي شَهْرَ رَمَضَانَ)
“Sikumwona Mtume ﷺ akijitahidi kufunga siku yeyote akaitanguliza kuliko siku ya Ashuraa na mwezi wa Ramadhani.” [Imepokewa na Bukhari]
Mtume ﷺ pia amesema:
(وَصِيَامُ يَومِ عَاشُورَاءَ، أَحْتَسِبُ علَى اللهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتي قَبْلَهُ)
“Kufunga siku ya Ashuraa, natarajia kwa Allah atasamehe madhambi ya mwaka uliopita.” [Imepokewa na Muslim]
4- Ni siku ambayo Allah alimnusuru Musa ( Amani ya Mungu iwe juu yake) dhidi ya Firauni
Mtume ﷺ amesema:
قَدِمَ النبيُّ صَلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ المَدِينَةَ فَرَأَى اليَهُودَ تَصُومُ يَومَ عَاشُورَاءَ، فَقالَ: ما هذا؟، قالوا: هذا يَوْمٌ صَالِحٌ هذا يَوْمٌ نَجَّى اللَّهُ بَنِي إسْرَائِيلَ مِن عَدُوِّهِمْ، فَصَامَهُ مُوسَى، قالَ: فأنَا أحَقُّ بمُوسَى مِنكُمْ، فَصَامَهُ، وأَمَرَ بصِيَامِهِ
Mtume alifika Madina akawaona Mayahudi wanafunga Siku ya Ashuraa akwauliza ni funga gani hii wakasema: “Hii ni siku njema, ni siku ambayo Allah aliwaokoa Bani Israil dhidi ya adui yao, basi Musa akaifunga.” Mtume ﷺ akasema: “Sisi tunastahili zaidi kumfuata Musa kuliko nyinyi. Kisha akaifunga na kuwaamrisha Waislamu waifunge pia.” [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
5- Ni Sunna kufunga Ashuraa pamoja na siku moja na Siku ya Tisa Au kufunga au kufunga siku baada yake Mtume ﷺ alisema:
(فَإِذَا كانَ العَامُ المُقْبِلُ إنْ شَاءَ اللَّهُ صُمْنَا اليومَ التَّاسِعَ)
“Nikifika mwakani nitafunga siku ya tisa (Tasuu’aa).” [Imepokewa na Muslim]
Hii ina maana: afadhali kufunga siku ya 9 na 10, au 10 na 11.
6: Ni mwanzo wa mwaka mpya wa Kiislamu, Muharram ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu, na inafaa sana kuanza mwaka kwa ibada, dua na taqwa.
📌Muhtasari wa Fadhila za Muharram:
1. Mwezi mtukufu katika Uislamu.
2. Ni funga Bora baada ya Ramadhani.
3. Una siku ya Ashuraa yenye fadhila ya kufuta madhambi ya mwaka mmoja uliopita.
4. Ndani yake Allah alimnusuru Musa (Amani ya Mungu iwe juu yake)
5. Ni mwanzo wa mwaka wa Hijria.
6. Umeheshimiwa kwa kuitwa “Mwezi wa Allah”.
Na Allaah Anajua Zaidi.