NASABA YA MTUME ﷺ
NASABA YA MTUME KWA UPANDE WA BABAKE.
Nasabu ya Bwana Mtume ﷺ – kwa upande wa baba yake ni kama ifuatavyo:
Yeye ni Muhammad Bin Abdillah Bin Abdil – Mutwalib Bin Haashim Bin Abdi Manaf Bin Qusway Bin Kilaab Bin Murrah Bin Kaab Bin Luayyi Bin Ghaalib Bin Fihr Bin Maalik Bin Nadhr Bin Kinaanah Bin Khuzaymah Bin Mudrikata Bin Ilyaas Bin Mudhwar Bin Nizaar Bin Maad Bin Adnaan.
Huu Adnaan ni katika kizazi cha Nabii Ismail Bin Ibrahim – Amani iwe juu yao.
Anasema Al-Mubaarakpuri katika kitabu chake ‘Ar-Rahiyq Al-Makhtuum;
Nasaba ya Muhammad ﷺ imegawika sehemu tatu tutakazozitaja hapo chini:
Sehemu ya mwanzo inayomalizikia kwa ‘Adnaan inakubaliwa kuwa ni sahihi na maulamaa wote wa Siyrah na wale wanaodurusu nasaba za watu mashuhuri.
Sehemu ya pili inayoanzia kwa ‘Adnaan na kumalizikia kwa Nabi Ibraahiym (‘Alayhis Salaam), wapo katika wanavyuoni wanaoikubali kuwa yote ni sahihi, na wapo wanaoutilia shaka usahihi wa baadhi yake.
Ama sehemu ya tatu, inayoanzia kwa Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) na kumalizikia kwa Adam (‘Alayhis Salaam), hii maulamaa wote takriban wanautilia shaka usahihi wake.
Sehemu ya kwanza ya nasaba ya Mtume wa Allaah ﷺ mpaka kufikia kwa ‘Adnaan (inayokubaliwa na maulamaa wote kuwa ni sahihi) ni kama ifuatavyo:
1. Muhammad bin ‘Abdillaah bin ‘Abdil-Muttwallib (aliyekuwa maarufu kwa jina Shaybatul Hamd) bin Haashim (jina lake hasa ni ‘Amru) bin ‘Abdu Manaaf (akijulikana pia kwa jina la Al-Mughiyrah) bin Qusay (jina lake ni Zayd) bin Kilaab bin Murrah bin Ka’ab bin Luay bin Ghaalib bin Fihr (na huyu ndiye aliyekuwa akijulikana kwa jina la Quraysh na asili ya watu wote wa Kabila la Quraysh inatokana na huyu) bin Maalik bin Nadhar (jina lake hasa ni Qays) bin Kinaanah bin Khuzaymah bin Mudrikatah (na jina lake hasa ni ‘Aamir) bin Ilyaas bin Madhar bin Nizar bin Ma-adi bin ‘Adnaan.
Sehemu ya pili inayoanzia kwa ‘Adnaan kwenda juu:
2. ‘Adnaan bin ‘Aadd bin Hamiyj bin Salaamaan bin Iwaas bin Bawz bin Qamwal bin Ubay bin Iwaam bin Nashid bin Hazaa bin Baldaas bin Badlaf bin Tabikh bin Jahim bin Nahish bin Makhiy bin Abadh bin Abqar bin Abiyd bin Ad da-a bin Hamdan bin Saniyr bin Yathribiy bin Yahzan bin Yalhan bin Ar-awiy bin Ais bin Dishan bin Aysar bin Afnad bin Ayham bin Maqsar bin Nahith bin Zarih bin Samiy bin Maziy bin Awadhah bin Iram bin Qaydaar bin Ismaa’iyl bin Ibraahiym (‘alayhima ssalaam).
Ama sehemu ya tatu inayoanzia kwa Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) ni kama ifuatavyo:
3. Ibraahiym bin Tarih (ambaye jina lake hasa ni Aazar) bin Nahur bin Saruh bin Sarugh bin Rauw bin Falikh bin Amir bin Shalikh bin Arafkhashad bin Sam bin Nuuh (‘Alayhis Salaam) bin Lamik bin Mutawashlakh bin Akhnukh (inasemekana kuwa huyu ndiye Nabii Idriys (‘Alayhis Salaam)) bin Yarad bin Mahlayl bin Qaynaan bin Anushah bin Shiyth bin Adam (‘Alayhis Salaam).
NASABA YA MTUME KWA UPANDE WA MAMA YAKE.
Nasaba yake Bwana Mtume ﷺ kwa upande wa mama yake:
Yeye ni Muhammad Bin Aaminah Bint Wahab Bin Abdi Manaf Bin Zuhrah Bin Hakiym. Huyu Mzee Hakiym ndiye Kilaab ambaye ni babu wa tano wa Mtume kwa upande wa baba yake.
Kwa hvyo kinashikana kizazi cha Baba yake Mtume na mama yake kwa babu wato naye ni Kilaab.