AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Hawa ndio watu katika kundi ambalo linajulikana katika historia ya Uislamu kuwa ndio Waislamu wa mwanzo, wakiongozwa na mke wa Mtume ﷺ, mama wa waumini Bi Khadija binti Khuwailid,
kijana wake Zaid bin Haritha bin Sharahbiyl AI-Kafuy,
mtoto wa ammi yake Ali bin Abi Twalib, wakati huo akiwa bado mtoto mdogo akiishi katika ulezi wa Mtume ﷺ ,
na rafiki yake mpenzi Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake). Hawa walisilimu katika siku ya kwanza ya Da’wa kwa watu katika Dini.
Kwa hivyo wa Kwanza Aliesilimu katika wanaume ni Abubakar Swiddiq (Radhi za Allah ziwe juu yake)
na katika Wanawake ni Bibi Khadija bint Khuwailid (Radhi za Allah ziwe juu yake).
na katika watoto ni Ali bin Abi Twalib (Radhi za Allah ziwe juu yake).
na katika vijakazi ni Zaid bin Harith (Radhi za Allah ziwe juu yake).
* Ar-Raheeq Al Makhtum 119