باب الورع وترك الشبهات
وعن وَابِصَةَ بن مَعبدٍ – رضي الله عنه -، قَالَ: أتَيْتُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَ: {جئتَ تَسْألُ عَنِ البِرِّ؟} قُلْتُ: نَعَمْ، فَقَالَ: { اسْتَفْتِ قَلْبَكَ، البرُّ: مَا اطْمَأنَّت إِلَيْهِ النَّفسُ، وَاطْمأنَّ إِلَيْهِ القَلْبُ، وَالإثْمُ: مَا حَاكَ في النَّفْسِ، وَتَرَدَّدَ فِي الصَّدْرِ، وَإنْ أفْتَاكَ النَّاسُ وَأفْتُوكَ} حديث حسن، رواه أحمد والدَّارمِيُّ في مُسْنَدَيْهِمَا
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
68. MLANGO WA UCHAMUNGU NA KUACHA SHUBHA (YENYE KUTIA SHAKA)
Imepokewa kutoka kwa Wâbisah bin Ma’bad (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesimulia: “Nilimwendea Mtume ﷺ akaniuliza: “Umekuja kuuliza juu ya wema?” Nikamjibu: “Ndio.” Akaniambia: “Uulize moyo wako, wema ni ambao nafsi yako imetulia kwake na moyo wako ukatulia. Na dhambi ni inayotia shaka katika nafsi na moyo ukafanya wasiwasi japo watu wakupe fatwa (kuwa jambo hilo lafaa).” [ Imepokewa na Ahmad na ad-Dârimy wameipokea katika Musnad zao. Hadîth hii ni Hasan.]