باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات
وعن أنسٍ – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ أَبو طَلْحَةَ لأُمِّ سُلَيمٍ: قَدْ سَمِعْتُ صَوْتَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – ضَعيفاً أعْرِفُ فيه الجُوعَ، فَهَلْ عِنْدَكِ مِنْ شَيْءٍ؟ فَقَالَتْ: نَعَمْ، فَأخْرَجَتْ أقْرَاصاً مِنْ شَعِيرٍ، ثُمَّ أخَذَتْ خِمَاراً لَهَا، فَلَفَّتِ الخُبْزَ بِبَعْضِهِ، ثُمَّ دَسَّتْهُ تَحْتَ ثَوْبِي وَرَدَّتْنِي بِبَعْضِهِ، ثُمَّ أرْسَلَتْني إِلَى رسولِ الله – صلى الله عليه وسلم -، فَذَهَبتُ بِهِ، فَوَجَدْتُ رسولَ الله – صلى الله عليه وسلم -، جَالِساً في المَسْجِدِ، وَمَعَهُ النَّاسُ، فَقُمْتُ عَلَيْهمْ، فَقَالَ لي رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: {أرْسَلَكَ أَبو طَلْحَةَ؟} فقلت: نَعَمْ، فَقَالَ: {ألِطَعَامٍ؟} فقلت: نَعَمْ، فَقَالَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم -: {قُومُوا} فَانْطَلَقُوا وَانْطَلَقْتُ بَيْنَ أيْدِيهِمْ حَتَّى جِئْتُ أَبَا طَلْحَةَ فَأخْبَرْتُهُ، فَقَالَ أَبو طَلْحَةَ: يَا أُمَّ سُلَيْمٍ، قَدْ جَاءَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – بالنَّاسِ وَلَيْسَ عِنْدَنَا مَا نُطْعِمُهُمْ؟ فَقَالَتْ: الله وَرَسُولُهُ أعْلَمُ. فَانْطَلَقَ أَبو طَلْحَةَ حَتَّى لَقِيَ رسولَ الله – صلى الله عليه وسلم -، فَأقْبَلَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – مَعَهُ حَتَّى دَخَلاَ، فَقَالَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم -: {هَلُمِّي مَا عِنْدَكِ يَا أُمَّ سُلَيْمٍ} فَأتَتْ بِذلِكَ الخُبْزِ، فَأمَرَ بِهِ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – فَفُتَّ، وَعَصَرَتْ عَلَيْهِ أمُّ سُلَيْمٍ عُكّةً فَآدَمَتْهُ، ثُمَّ قَالَ فِيهِ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – مَا شَاءَ اللهُ أنْ يَقُولَ، ثُمَّ قَالَ: {ائْذَنْ لِعَشْرَةٍ} فأذنَ لَهُمْ فَأكَلُوا حتى شَبِعُوا ثُمَّ خَرَجُوا، ثُمَّ قَالَ: {ائْذَنْ لِعَشْرَةٍ} فأذِنَ لهم حَتَّى أكَلَ الْقَوْمُ كُلُّهُمْ وَشَبِعُوا وَالقَوْمُ سَبْعُونَ رَجُلاً أَو ثَمَانُونَ. متفقٌ عَلَيْهِ.
وفي رواية: فَمَا زَالَ يَدْخُلُ عَشرَة، وَيخرجُ عشرةٌ حَتَّى لَمْ يَبْقَ مِنْهُمْ أحَدٌ إِلاَّ دَخَلَ، فَأكَلَ حَتَّى شَبعَ، ثُمَّ هَيَّأهَا فَإذَا هِيَ مِثْلُهَا حِيْنَ أكَلُوا مِنْهَا
وفي رواية: فَأَكَلُوا عَشرَةً عَشرةً، حَتَّى فَعَلَ ذَلِكَ بِثَمَانِينَ رَجُلاً، ثُمَّ أكَلَ النبيُّ – صلى الله عليه وسلم – بَعْدَ ذَلِكَ وَأهْلُ البَيْتِ، وَتَرَكُوا سُؤْراً
وفي رواية: ثُمَّ أفْضَلُوا مَا بَلَغُوا جيرانَهُمْ
وفي رواية عن أنس، قَالَ: جِئتُ رسولَ الله – صلى الله عليه وسلم – يوماً، فَوَجَدْتُهُ جَالِساً مَعَ أصْحَابِه، وَقَدْ عَصَبَ بَطْنَهُ، بِعِصَابَةٍ، فقلتُ لِبَعْضِ أصْحَابِهِ: لِمَ عَصَبَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – بَطْنَهُ؟ فقالوا: مِنَ الجوعِ، فَذَهَبْتُ إِلَى أَبي طَلْحَةَ، وَهُوَ زَوْجُ أُمِّ سُلَيْمٍ بِنْت مِلْحَانَ، فقلتُ: يَا أبتَاهُ، قَدْ رَأيْتُ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – عَصَبَ بَطْنَهُ بِعِصَابَةٍ، فَسَألْتُ بَعْضَ أصْحَابِهِ، فقالوا: من الجُوعِ. فَدَخَلَ أَبو طَلْحَةَ عَلَى أُمِّي، فَقَالَ: هَلْ مِنْ شَيءٍ؟ قالت: نَعَمْ، عِنْدِي كِسَرٌ مِنْ خُبْزٍ وَتَمَرَاتٌ، فَإنْ جَاءنَا رسول الله – صلى الله عليه وسلم – وَحْدَهُ أشْبَعْنَاهُ، وَإنْ جَاءَ آخَرُ مَعَهُ قَلَّ عَنْهُمْ… وَذَكَرَ تَمَامَ الْحَدِيثِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesimulia: “Abû Talha alimwambia Ummu Sulaim: “Hakika nimeisikia sauti ya Mtume ﷺ ikiwa dhaifu, nahisi ana njaa. Una kitu?” Akajibu: “Ndio. Akaitoa mikate ya shayiri, kisha akauchukua mtandio wake akautatia mkate, halafu akautia chini ya nguo yangu na akanitatia sehemu nyingine ya mtandio ule. Akanituma kwa Mtume ﷺ , nikaenda nayo. Nikamkuta Mtume ﷺ ameketi Msikitini pamoja na watu. Nikasimama kando yao. Mtume ﷺ akaniuliza: “Abû Talha amekutuma?” Nikamjibu: “Ndio.” Akaniuliza: “Chakula?” Nikamjibu: “Ndio.” Mtume ﷺ akawaambia Maswahaba: “Inukeni.” Wakaondoka, nami niko mbele yao, mpaka nikamjia Abû Talha nikamweleza. Abû Talha akasema: “Ee Ummu Sulaim, Mtume ﷺ amekuja na watu wala hatuna cha kuwalisha!” (Ummu Sulaim) akasema: “Allâh na Mtume Wake Wanajua.” Abû Talha akaenda kumlaki Mtume ﷺ , Mtume ﷺ alikuwa amekuja na watu, (Abû Talha na Mtume) wakaingia. Mtume ﷺ akasema: “Ee Ummu Sulaim, lete ulichonacho.” Akauleta mkate ule, Mtume ﷺ akaamuru ukatwe vipande vipande, Ummu Sulaim akakamua juu yake kopo (la samli) akafanya ndio kitoweo chake. Mtume ﷺ akausomea mkate huo kiasi Alivyopenda Allâh, kisha akasema: “Waruhusu watu kumi (waingie).” Akawaruhusu, wakala mpaka wakashiba, wakatoka. Akasema: “Waruhusu watu kumi.” Wakaruhusiwa wakala mpaka wakashiba, wakatoka. Kisha akasema: “Waruhusu watu kumi.” Wakaruhusiwa, mpaka watu wote wakala na wakashiba. Walikuwa ni watu sabiini au thamanini.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim].
Riwaya nyingine imesema: “Wakaendelea kuingia watu kumi na wakitoka watu kumi, hakuna aliebakia, wote waliingia kila mmoja alikula mpaka akashiba. Kisha akaikusanya, ikawa vile vile kama ilivyokuwa.”
Riwaya nyingine imesema: “Wakala watu kumi-kumi mpaka wakatimia watu thamanini, kisha baada ya hapo Mtume ﷺ akala, na watu wa nyumbani pia, wakabakisha masaza.”
Riwaya nyingine imesema: “Kisha wakawapelekea majirani zao kilichobaki.”
Riwaya nyingine kutoka kwa Anas imesema: “Siku moja nilimwendea Mtume ﷺ , nikamkuta ameketi pamoja na Maswahaba zake, alikuwa amefunga kitambaa tumboni mwake. Nikawauliza baadhi ya Maswahaba zake: “Kwa nini Mtume ﷺ amelifunga tumbo lake?” Wakanijibu: “Kwa sababu ya njaa.” Nikamwendea Abû Talha naye ni mume wa Ummu Sulaim binti Milhan, nikamwambia: “Baba yangu! Nimemuona Mtume ﷺ amelifunga tumbo lake kwa kitambaa, nikawauliza baadhi ya Maswahaba zake, wakaniambia ni kwa sababu ya njaa!” Abû Talha akaingia kwa mama yangu, akamwuliza: “Una kitu?” Akajibu: “Ndio, nina vipande vya mkate na tende chache, iwapo Mtume ﷺ atatujia peke yake, tutamshibisha, na akija na mtu mwingine chakula kitawapungukia…” akaendelea mpaka mwisho wa Hadîth.