0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

519. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Njaa, Maisha Ya Chini Kutosheka Kwa Vichache Katika Vyakula…..

 باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات


وعن جابر – رضي الله عنه -، قَالَ: إنَّا كُنَّا يَوْمَ الْخَنْدَقِ نَحْفِرُ، فَعَرَضَتْ كُدْيَةٌ شَدِيدَةٌ، فَجَاؤُوا إِلَى النبي – صلى الله عليه وسلم -، فقالوا: هذِهِ كُدْيَةٌ عَرَضَتْ في الخَنْدَقِ. فَقَالَ: {أنَا نَازِلٌ} ثُمَّ قَامَ، وَبَطْنُهُ مَعْصُوبٌ بِحَجَرٍ، وَلَبِثْنَا ثَلاَثَة أيّامٍ لاَ نَذُوقُ ذَوَاقاً فَأخَذَ النبي – صلى الله عليه وسلم – المِعْوَلَ، فَضَرَبَ فَعَادَ كَثيباً أهْيَلَ أَو أهْيَمَ، فقلت: يَا رسول الله، ائْذَنْ لي إِلَى البَيْتِ، فقلتُ لامْرَأتِي: رَأيْتُ بالنَّبيِّ – صلى الله عليه وسلم – شَيئاً مَا في ذَلِكَ صَبْرٌ فَعِنْدَكِ شَيْءٌ؟ فقالت: عِنْدي شَعِيرٌ وَعَنَاقٌ ، فَذَبَحْتُ العَنَاقَ وَطَحَنْتُ الشَّعِيرَ حَتَّى جَعَلْنَا اللَّحْمَ في البُرْمَةِ، ثُمَّ جِئْتُ النبي – صلى الله عليه وسلم -، وَالعَجِينُ قَدِ انْكَسَرَ، وَالبُرْمَةُ بَيْنَ الأثَافِيِّ قَدْ كَادَتْ تَنْضِجُ، فقلتُ: طُعَيْمٌ لي، فَقُمْ أنْتَ يَا رسول اللهِ وَرَجُلٌ أَوْ رَجُلانِ، قَالَ: {كَمْ هُوَ}؟ فَذَكَرْتُ لَهُ، فَقَالَ: {كثيرٌ طَيِّبٌ قُل لَهَا لاَ تَنْزَع البُرْمَةَ، وَلاَ الخبْزَ مِنَ التَّنُّورِحتى آتِي} فَقَالَ: {قُومُوا}، فقام المُهَاجِرُونَ وَالأنْصَارُ، فَدَخَلْتُ عَلَيْهَا فقلتُ: وَيْحَكِ قَدْ جَاءَ النبيُّ – صلى الله عليه وسلم – وَالمُهَاجِرُونَ وَالأنْصَارُ ومن مَعَهُمْ ! قالت: هَلْ سَألَكَ؟ قُلْتُ: نَعَمْ، قَالَ: {ادْخُلُوا وَلاَ تَضَاغَطُوا} فَجَعَلَ يَكْسرُ الخُبْزَ، وَيَجْعَلُ عَلَيْهِ اللَّحْمَ، وَيُخَمِّرُ البُرْمَةَ وَالتَّنُّور إِذَا أخَذَ مِنْهُ، وَيُقَرِّبُ إِلَى أصْحَابِهِ ثُمَّ يَنْزعُ، فَلَمْ يَزَلْ يِكْسِرُ وَيَغْرِفُ حَتَّى شَبِعُوا، وَبَقِيَ مِنْهُ، فَقَالَ: {كُلِي هَذَا وَأهِدي، فَإنَّ النَّاسَ أصَابَتْهُمْ مَجَاعَةٌ}    متفقٌ عَلَيْهِ

وفي رواية قَالَ جابر: لَمَّا حُفِرَ الخَنْدَقُ رَأيْتُ بالنبيِّ – صلى الله عليه وسلم – خَمَصاً، فَانْكَفَأْتُ إِلَى امْرَأتِي، فقلت: هَلْ عِنْدَكِ شَيْءٌ؟ فَإنّي رَأيْتُ برسول الله – صلى الله عليه وسلم – خَمَصاً شَديداً، فَأخْرَجَتْ إلَيَّ جِرَاباً فِيه صَاعٌ مِنْ شَعِيرٍ، وَلَنَا بَهِيمَةٌ دَاجِنٌ فَذَبَحْتُهَا، وَطَحَنتِ الشَّعِيرَ، فَفَرَغَتْ إِلَى فَرَاغي، وَقَطَعْتُهَا في بُرْمَتها، ثُمَّ وَلَّيْتُ إِلَى رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، فقالت: لاَ تَفْضَحْنِي برسول الله – صلى الله عليه وسلم – وَمَنْ مَعَهُ، فَجئتهُ فَسَارَرْتُهُ، فَقُلْتُ: يَا رسول الله، ذَبَحْنَا بهيمَة لَنَا، وَطَحَنْتُ صَاعاً مِنْ شَعِيرٍ، فَتَعَالَ أنْتَ وَنَفَرٌ مَعَكَ، فَصَاحَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَ: {يَا أهلَ الخَنْدَقِ: إنَّ جَابِراً قَدْ صَنَعَ سُؤْراً فَحَيَّهَلا بِكُمْ} فَقَالَ النبي – صلى الله عليه وسلم -: {لاَ تُنْزِلُنَّ بُرْمَتَكُمْ وَلاَ تَخْبزنَّ عَجِينَكُمْ حَتَّى أجِيءَ} فَجِئْتُ، وَجَاءَ النبي – صلى الله عليه وسلم – يَقْدُمُ النَّاسَ، حَتَّى جِئْتُ امْرَأتِي، فقالَتْ: بِكَ وَبِكَ ! فقُلْتُ: قَدْ فَعَلْتُ الَّذِي قُلْتِ. فَأخْرَجَتْ عَجِيناً، فَبسَقَ فِيهِ وَبَاركَ، ثُمَّ عَمَدَ إِلَى بُرْمَتِنا فَبصَقَ وَبَارَكَ، ثُمَّ قَالَ: {ادْعِي خَابزَةً فَلْتَخْبِزْ مَعَكِ، وَاقْدَحِي مِنْ بُرْمَتِكُمْ، وَلاَ تُنْزِلُوها} وَهُم ألْفٌ، فَأُقْسِمُ بِالله لأَكَلُوا حَتَّى تَرَكُوهُ وَانْحَرَفُوا، وَإنَّ بُرْمَتَنَا لَتَغِطّ كَمَا هِيَ، وَإنَّ عَجِينَنَا لَيُخْبَزُ كَمَا هُوَ.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Jâbir (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesimulia; ‘Siku ya Vita vya Khandaq tulikuwa tukichimba, ukatokeza mwamba mgumu, Maswahaba wakamwendea Mtume wakamwambia: “Kuna mwamba mgumu umejitokeza katika shimo.” Akasema: “Mimi nitateremka.” Akasimama, tumbo lake lilikuwa limefungwa jiwe (kwa sababu ya njaa). Tuliketi siku tatu hatuonji chakula. Mtume  akachukua mtaimbo, akaupiga mwamba, ukawa laini kama mchanga. Nikamwambia: “Yâ Rasûlallâh, niruhusu niende nyumbani.” Nilipofika nyumbani nilimwambia mke wangu: “Nimeona kitu kwa Mtume ﷺ na hakuna namna ya kusubiri, una kitu (chakula)?” Akanambia: “Nina shayiri na mbuzi.” Nikamchinja mbuzi yule, nikaisaga shayiri na tukaiweka nyama sufuriani. Nikamwendea Mtume ﷺ na unga ulikuwa umeshalainika (tayari kupikwa), na sufuria iko juu ya mawe, nyama imekaribia kuiva. Nikamwambia (Mtume): “Nimetengeneza chakula kidogo, kwa hivyo Yâ Rasûlallâh, njoo wewe na mtu mmoja au wawili.” Akaniuliza: “Chakula cha watu wangapi?” Nikamweleza kilivyo. Akasema: “Ni kingi kizuri, mwambie (mkeo) asiiondoshe sufuria wala mkate kutoka katika tanuri mpaka nitapokuja.” Akawaambia Maswahaba: “Inukeni.” Muhajirina na Ansari wakasimama. Nikamwendea (mke wangu), nikamwambia: “Nakuhurumia! Mtume ﷺ amekuja na Muhajirina, Ansari na wote walio pamoja nao!” Akaniuliza: “Alikuuliza?” Nikamwambia: “Ndio.” (Mtume ﷺ) akawambia: “Ingieni wala msisongamane.” Akawa akiukata mkate na akiweka nyama juu yake, na akiifunika sufuria na tanuri wakati anapochota, akiwasogezea Maswahaba zake kisha akirudi. Akaendelea kukata mkate na kuchota (mchuzi) mpaka wote wakashiba na ikabakia. Akamwaambia (mke wangu): “Kula hiki na utoe hadiya (zawadi), hakika watu wamepatwa na njaa.”              [ Wameafikiana Bukhari na Muslim].
Riwaya nyingine imesema: “Jâbir amesimulia: “Lilipochimbwa shimo (khandaq) nilimuona Mtume ana njaa. Nikamwendea mke wangu nikamwambia: “Una kitu? Nimemuona Mtume ﷺ ana njaa kali.” Akanitolea mfuko uliokuwa una pishi ya shayiri, tulikuwa tuna kijimbuzi kilichozowea pale nyumbani, nikamchinja naye akaisaga shayiri. Nilipomaliza naye alikuwa ameshamaliza pia. Nikaikata nyama kwenye sufuria kisha nikamwendea Mtume ﷺ (kumwalika). Mke wangu akanambia: “Usinifedheheshe kwa Mtume ﷺ na Maswahaba zake!” Nikamwendea Mtume ﷺ nikamnong’onezea: “Yâ Rasûlallâh, tumechinja kijimbuzi chetu na nimesaga pishi moja ya shayiri, njoo wewe na watu wachache walio pamoja nawe.” Mtume ﷺ akapiga uyowe: “Enyi watu wa Khandaq, Jâbir ametengeneza karamu, njooni!” Mtume ﷺ akatwambia: “Msiteremshe sufuria yenu wala msiupike unga wenu mpaka nije.” Nikarudi nyumbani, Mtume ﷺ akaja akiwa yuko mbele ya umati wa watu. Nikamwendea mke wangu, akanitetesha na kunishutumu. Nikamwambia: “Nilifanya kama ulivyosema.” Akautoa unga (uliokuwa umeshakandwa), Mtume ﷺ akautemea mate na akauwombea baraka, halafu akaenda katika sufuria yetu akatema mate na akaombea baraka, kisha akamwambia (mke wangu): “Mwite mwenye kuoka mikate aoke pamoja nawe, uchote kutoka katika sufuria yenu wala musiiteremshe.” Wageni waliohudhuria walikuwa ni watu elfu moja. Basi naapa kwa Allâh! Walikula mpaka wakakiacha na wakarejea na sufuria yetu bado inatokota kama ilivyo, na unga wetu unapikiwa mikate kama ulivyo.”

Begin typing your search above and press return to search.