0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

AWAMU YA KWANZA -JIHADI YA DA’WA

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


MIAKA MITATU YA DA’WA YA SIRI

Inaeleweka kuwa Makka ilikuwa ndio kituo cha Waarabu. Walikuwapo waangalizi wa Al-Ka’aba, na waangalizi wa masanamu yaliyokuwa matakatifu mbele ya Waarabu wote. Kwa sababu hiyo, kazi ya kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa katika kufanya matengenezo hapo Makka ilikuwa ni kazi pevu iliyokuwa na ugumu wake na matatizo mengine makubwa kabisa. Jambo hilo lilihitaji uimara na azma isiyoyumbishwa. 

Matukio ya misiba na majanga ilikuwa ni katika hekima na busara mbele ya mazingira kama hayo. Katika siku za mwanzo Da’wa ilifanywa kwa njia za siri, ili kuepuka kuzusha mgogoro na watu wa Makka, kwa mafundisho ambayo kwa hali yoyote ile yangewacharura. 

Kundi la Kwanza
Lilikuwa ni jambo la kawaida kwa Mtume . ï·º  kuutangaza Uislamu kwa watu waliokuwa karibu naye kwanza, kwa kuanzia nyumbani kwake na kwa marafiki zake wa karibu. Kwa hivyo aliwaita kwenye Uislamu na alimwita kwenye Uislamu kila ambaye aliiona kheri kwake, miongoni mwa wale anaofahamiana nao, aliokuwa anawajua kwa Kumpenda Mwenyezi Mungu ï·» .

Kwa vile wengi wao walikuwa wanafahamu alivyokuwa mkweli, jinsi alivyokuwa mpenda kheri, na alivyo mwema, walimuitikia. Watu hao hawakuwa na shaka yoyote kwa ukubwa wa jukumu alilopewa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ï·º, utukufu wa nafsi yake na ukweli wa khabari yake.


* Ar-Raheeq Al Makhtum 118-119


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.