0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ARBAIN NAWAWIY HADITHI YA 4 HAKIKA LINAKUSANYWA UMBO LA KILA MMOJA WENU

الحديث الرابع


“إن أحدكم يجمع في بطن أمه”


عن أبي عبْدِ الرَّحْمن عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه قال: حدَّثَنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وهُوَ الصَّادقُ المَصْدوق: [إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يُرْسَلُ إليه المَلكُ فَيَنْفخُ فيه الرُّوحَ ويُؤمَرُ بأرْبَعِ كلماتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ وأَجَلِهِ وعَمَلِهِ وشَقيٌّ أو سَعيدٌ، فَوَاللهِ الَّذي لا إله غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ ليَعْمَلُ بعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ حتى ما يكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَليْه الكِتابُ فَيَعْمَلُ بعَملِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُها. وإنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهل النَّارِ حتى ما يَكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكتابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهل الجنَّةِ فَيَدْخُلُها

رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالىHADITHI YA 4


HAKIKA UMBO LA KILA MMOJA WENU LINAKUSANYWA KATIKA TUMBO LA MAMA YAKE.


Kutoka kwa Abu Abdur-Rahman Abdullaah Ibn Masu’ud Radhi za Mwenyzi Mungu ziwe juu yake ambaye alisema: Mtume Rehma na amani zimfikie yeye naye ndie mkweli, anaesadikiwa alitueleza haya:

[Hakika umbo la kila mmoja wenu linakusanywa pamoja katika tumbo la mama yake kwa muda wa siku arubaini, ikiwa katika hali ya mbegu, baadaye tone la damu kwa muda kama huo, tena huwa ni kipande cha nyama kwa muda kama huo, tena hupelekwa Malaika anaempulizia pumzi za uhai na anaamrishwa mambo manne: kuandika rizki yake, maisha yake, amali yake na akiwa atakuwa (mtu) mbaya au mwema. Kwa Allaah ambaye hakuna Mungu isipokuwa Yeye, mmoja katika nyinyi hufanya vitendo vya watu wa peponi mpaka baina yake na pepo ikawa dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja katika nyinyi hufanya amali ya watu wa motoni mpaka baina yake na moto ikawa dhiraa, na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya amali ya watu wa peponi akaingia peponi.]

[Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim.]


Sikiliza sherehe ya hadithi hii na Sheikh Mahamad Rajab sehemu ya kwanza

Sikiliza sherehe ya hadithi hii na Sheikh Mahamad Rajab sehemu ya pili

Sikiliza sherehe ya hadithi hii na Sheikh Mahamad Rajab sehemu ya tatu

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.