0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ARBAIN NAWAWIY HADITHI YA 36 KUWAKIDHIA WAISLAMU HAJA ZAO


الحديث السادس والثلاثون


“من نفس عن مسلم كربة”


عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال: [ مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً من كُرَبِ يوْمِ القيامَةِ، ومَنْ يَسَّرَ على مُعْسِرٍ يَسَّرَ اللهُ عليه في الدنْيا والآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ الله في الدُّنْيا والآخِرَةِ واللهُ في عَوْنِ الْعَبْدِ ما كانَ الْعَبْدُ في عَونِ أخيهِ. ومَنْ سلك طَريقاً يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْماً سَهَّلَ اللهُ له بِهِ طَرِيقاً إلى الجنَّةِ وَمَا اجتَمَعَ قَوْمٌ في بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ويَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إلا نَزَلَتْ عليهمُ السَّكِينَةُ، وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وحَفَّتهُمُ المَلائِكَةُ، وذَكَرَهُمُ اللهُ فيمَنْ عِنْدَه  وَمَنْ بَطَّأ بِه عَمَلُهُ لمْ يُسْرِعْ به نَسَبُهُ]

رَوَاهُ مُسْلِمٌ بهذا اللفظ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى



HADITHI YA 36


ATAKAYEMUONDOSHEA SHIDA MUISLAMU MWENZAKE, ALLAH ATAMUONDOSHEA SHIDA ZAKE


Kutoka kwa Abu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye amesema kwamba Mtume ﷺ kasema:

[Yeyote atakaemuondoshea shida ya kidunia Muislamu mwenzake, Allaah Atamuondoshea moja katika shida za siku ya Kiyama. Yeyote yule anaemsaidia muhitaji (maskini) Allaah Atamsaidia haja zake hapa duniani na akhera. Yeyote yule anayemsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri hapa duniani na akhera.
Mwenyeezi Mungu humsaidia mja wake wakati wote mja anapomsaidia nduguye (Muislamu). Yeyote yule anayekamata njia kutafuta elimu, Allaah Atamrahisishia njia ya peponi. Hawakutaniki watu katika nyumba ya Mwenyeezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyeezi Mungu na wakasomeshana pamoja ila watashukiwa na utulivu (sakina) na kheri. Rehema (za Allah) huwafunika na Malaika huwazunguka na Allaah Huwakumbuka kwa wale walioko pamoja Nae. Yeyote yule anayeakhirishwa (anayecheleweshwa) na vitendo vyake (kwenda peponi) hatoharakishwa na Nasab yake.]
[Imepokelewa na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.