0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ARBAIN NAWAWIY HADITHI YA 02 DARAJA ZA DINI

الحديث الثاني


“مجىء جبريل ليعلم المسلمين أمر دينهم”


عَن عُمَر رضي اللهُ عنه أَيْضاً قال: بَيْنَما نَحْنُ جُلْوسٌ عِنْدَ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ذات يَوْم إذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَياضِ الثِّيَاِبِ شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عليه أَثَرُ السَّفَرِ ولا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتى جَلَسَ إلى النَّبِّي صلى الله عليه وسلم، فأسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إلى رُكْبَتَيْهِ ووَضَعَ كَفَّيْهِ على فَخِذَيْهِ، وقال: يا محمَّدُ أَخْبرني عَن الإسلامِ، فقالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم:[ الإسلامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمِّداً رسولُ الله، وتُقِيمَ الصَّلاةَ، وتُؤتيَ الزَّكاةَ، وتَصُومَ رَمَضان، وتَحُجَّ الْبَيْتَ إن اسْتَطَعتَ إليه سَبيلاً]. قالَ صَدَقْتَ. فَعَجِبْنا لهُ يَسْأَلُهُ ويُصَدِّقُهُ، قال : فَأَخْبرني عن الإِيمان. قال: [أَن تُؤمِنَ باللهِ، وملائِكَتِهِ وكُتُبِهِ، ورسُلِهِ، واليَوْمِ الآخِرِ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ وشَرِّهِ] قال صدقت. قال : فأخْبرني عَنِ الإحْسانِ. قال:[ أنْ تَعْبُدَ الله كَأَنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاك]. قال: فأَخبرني عَنِ السَّاعةِ، قال: [ما المَسْؤولُ عنها بأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ ]. قال: فأخبرني عَنْ أَمَارَتِها، قال:[ أن تَلِدَ الأمَةُ رَبَّتَها، وأَنْ تَرَى الحُفاةَ العَُراةَ العالَةَ رِعاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ في الْبُنْيانِ] ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيّاً، ثُمَّ قال : [يا عُمَرُ، أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟] قُلْتُ: اللهُ ورسُولُهُ أَعلَمُ . قال: [ فإِنَّهُ جِبْرِيلُ أَتاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ

رَوَاهُ مُسْلِمٌ


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى الجزء الأول



 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى الجزء الثاني



شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى الجزء الثالث



شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى الجزء الرابع



HADITHI YA 2


KUJA KWA JIBRIIL ALAYHI SALAAM KUWAFUNDISHA WAISLAMU MAMBO YA DINI YAO


Kutoka kwa ‘Umar Radhi za Mwenyeezi Mungu ziwe juu yake ambaye amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Mtume Rehma na amani zimfikie yeye, hapo alitokea mtu ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Mtume Rehma na amani zimfikie yeye, akaweka magoti yake karibu na magoti yake (Mtume) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ewe Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu. Mjumbe wa Allaah Rehma na amani zimfikie yeye,alisema: [Uislamu ni kukiri kuwa hakuna mola isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mjumbe wake, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.]

Akasema (yule mtu) Umesema kweli. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake Mtume na kumsadikisha. Na akasema tena: Niambie kuhusu Imani. Akasema (Mtume Rehma na amani zimfikie yeye) [Ni kumwamini Mwenyeezi-Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake na siku ya Qiyaama, na kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake (Allaah alie tukuka )]. Akasema: Umesema kweli, akasema hebu nielezee kuhusu Ihsaan. Akasema Mtume Rehma na amani zimfikie yeye, [Ni kumuabudu Allaah Sub’hanahu wata’aala kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona.] Akasema (Jibriyl): Niambie kuhusu Qiyaama. Akajibu (Mtume Rehma na amani zimfikie yeye) : [Hakuwa mwenye kulizwa ni mjuzi kuliko alie uliza]. Kisha akamwambia: Nijulishe alama zake: Akajibu (Mtume Rehma na amani): [Kijakazi atazaa bwana yake, na utaona wachunga mbuzi miguu wasio kuwa na viatu, wenda uchi  mafukara wakishindana kujenga majumba ya fahari.] Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo. Kisha akasema Mtume Rehma na amani [Ewe ‘Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? ] Nikasema: Allaah na Mjumbe wake wanajua zaidi. Akasema Mtume Rehma na amani [Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.]

[Imepokewa na Imam Muslim]

Sikiliza sherehe ya hadithi hii na Sheikh Mahamad Rajab sehemu ya kwanza

Sikiliza sherehe ya hadithi hii na Sheikh Mahamad Rajab sehemu ya pili

Sikiliza sherehe ya hadithi hii na Sheikh Mahamad Rajab sehemu ya tatu

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.