AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Malengo ya Hijrah hayakuwa ni kuepukana na fitna na kuchezwa shere pekee, Iengo kuu lilikuwa ni kupata pahala pa amani, ambapo Waislamu wangeshirikiana katika jamii mpya. Kwa ajili hiyo ilikuwa ni jambo la lazima (faradhi) kwa kila Muislamu ’aliyekuwa na uwezo kuchangia katika kuijenga jamii mpya na nchi mpya na wakati wote kuwa tayari kuilinda kwa hali na mali kuinyanyua hali yake.
Hakuna shaka kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) ndiye aliyekuwa Imamu, Jemadari na kiongozi katika ujenzi wa jamii hii mpya, hatamu za mambo yote zilikuwa mwake, na jambo hili halina upinzani wowote.
Mtume (ﷺ) alipofika Madina alikabiliana na makundi ya watu wa aina tatu. Kila kundi moja lilitofautiana na kundi jingine tofauti iliyo wazi kabisa. Matatizo aliyokuwa akikabiliana nayo Mtume (ﷺ) na kundi moja yanatofautianana makundi mengine. Aina tatu ya makundi hayo ni kama ifuatavyo: –
1). Masahaba zake waliokuwa wema (Radhi za Allah ziwe juu yao).
2). Mushirikina ambao walikuwa bado hawajaamini, miongoni’ mwao wakiwemo watu maarufu katika makabila ‘ya Madina.
3). Mayahudi
(1) Mambo ambayo alikuwa akikabiliana nayo kwa upande wa masahaba wake, ni kuwa mazingira ya Madina kwa upande wao yalikuwa ni tofauti sana ukilinganisha na maisha ambayo walikuwa wameyazoea huko kwao Wakati wakiwa Makka, pamoja na kuwa waliunganishwa na tamko la pamoja (la Uislamu), malengo yanayowiana, lakini jambo kubwa lililokuwa likiwatia uzito lilikuwa ni ile hali ya udhalili na kutotakiwa na mambo yote yakiwa ya maadui zao. Ilikuwa ni vigumu kwao kusimamisha jamii ya Kiislamu pamoja na mafunzo yake ambayo isingeweza kuishi mbali nayo jamii yoyote ya wanaadamu ulimwenguni.
Kwa msingi huo ndio. maana tunaona kuwa sura zilizoshuka Makka zilikuwa zikisisitiza ufafanuzi wa misingi ya Kiislamu na kufundisha Sheria ambazo inawezekana kutekelezwa na kila mtu mmoja mmoja, zikihimiza kufanya wema, kheri na tabia zilizo bora na kujiepusha na mambo machafu yasiyofaa.
Mambo ya Waislamu, Madina, yalikuwa mikononi mwao wenyewe tokea siku ya -kwanza. Hapakuwa na utawala mwingine wa aina yoyote uliokuwa maishayao. Kwa hivyo, ulikuwa umefika wakati kwao wa kuyakabili mambo ya maendeleo na ujenzi wa mji, mambo ya maisha na uchumi, mambo ya siasa na u‘tawala na mambo ya amani na vita. ‘Utenganishaji uliokamilika katika mambo ya halali na haramu, ibada na tabia na mambo yanayofanana na hayo katika mambo ya maisha ya kila siku.
Ulikuwa umefika wakati wa kujenga jamii mpya, jamii ya Kiislamu inayotofautiana katika ngazi zote za maisha na jamii ya kijahilia (Jamii isiyofuata mafunzo ya Kiislamu na maadili yake). Kusimamisha jamii ya Kiislamu inayotofautiana na jamii zingine zinazopatikana ulimwenguni, itakayokuwa yenye kusimamia Da’awa ya Uislamu, ambayo imewafanya watu wateseke kwa sababu ya wito huo.
Waislamu walionja namna nyingi za mateso na adhabu kwa kipindi chote cha miaka kumi ya Makka.
Ni jambo lisilo na kificho kuwa kuijenga jamji yoyote ile katika muundo huu ni jambo lisilowezekana kusimama kwa siku moja, au mwezi mmoja, au mwaka mmoja. Ni jambo linalohitaji muda wa kutosha ili kulikamilisha ili kuwekea sheria na kanuni pamoja na kuielimisha jamii na kuilea katika kufikia ufanisi. Mwenyezi Mungu (s.w.t) Ndiye Mdhamini wa Sheria hii na Mjumbe Wake (ﷺ) alisimama kwa kuitekeleza na kuwaongoza watu kwenye sheria hiyo na kuwahimiza Waislamu waitii:-
هُوَ ٱلَّذِي بَعَثَ فِي ٱلۡأُمِّيِّـۧنَ رَسُولٗا مِّنۡهُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمۡ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَإِن كَانُواْ مِن قَبۡلُ لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ
[ Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.] (62: 2) Masahaba (Radhi za Allah ziwe juu yao) walizifuata Sheria hizo kwa nyoyo zao zote na wakazitekeleza kwa kujipamba na hukmnu zake na kuzifurahia hukumu hizo.
وَإِذَا تُلِيَتۡ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُهُۥ زَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا
“Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.” (8:2)
Lengo letu halikuwa kuyafafanua yote haya katika maudhui hii hmaeleza tu kwa ufupi kadri ya haja.
Hili ndilo jambo kubwa alilokuwa akikabiliana nalo Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) kwa upande wa Waislamu, na hili ndilo lililokuwa lengo linalokusudiwa – kwa ujumla – kutokana na Da’awa ya Uislamu na Risala ya Mtume Muhammad (ﷺ). Hili halikuwa ni jambo lililozuka tu, ijapokuwa kulikuwa na mambo mengine yasiyokuwa hayo ambayo yalifanyiwa haraka kutekelezwa.
Jamii ya Kijslamu iliyoungana ilikuwa katika makundi mawili;
Kundi la kwanza – ni wale waliokuwa katika mji wao na mali zao, haliwashughulishi isipokuwa yale ambayo yanamshughulisha mtu hali yakuwa yumo katika amani ya moyo wake. Hawa ni Answari na miongoni mwao ulikuwepo mgawanyiko na uadui wa muda mrefu.
Kundi la -pili — lilihusisha Muhajirina ambao waliyakosa yote hayo, waliokoa nafsi zao tu toka Makka. Walipokuja Madina, walikuwa hawana pahala pa kukimbilia, wala kazi ambayo wangeifanya kwa ajili ya maisha yao, wala mali ambayo ingewapa angalao msimamo wa maisha. Idadi ya Muhajirina haikuwa ndogo na kila siku ilikuwa inaongezeka, kwani wakati huo Hijra ilikuwa imeruhusiwa (imefaradhiwa) kwa kila mwenye Kumwamini Mwenyezi Mungu (ﷻ) na Mtume wake (ﷺ). Ni jambo linaloeleweka kuwa mji wa Madina haukuwa na uchumi ulioendelea kiasi hicho na kwa sababu hiyo hali ya uchumi ikazidi kuwa mbaya, na katika wakati huu mgumu, maadui wa Uislamu walitangaza kuwatenga kiuchumi Waislamu, bidhaa kutoka nje zilipungua na maisha yakawa magumu zaidi.
(2) Kundi la pili la watu lilikuwa ni kundi la Mushirikina katika watu wa makabila ya Madina ambao hawakuwa na uwezo wowote kwa Waislamu. Miongoni mwao walikuwepo ambao walikuwa katika mashaka na kuzingazinga kati ya kuiacha dini ya mababu zao na kuingia katika Uislamu. Hawa walikuwa hawafichi uadui na vitimbi vyao dhidi ya Uislamu na haukupita muda mrefu na wao wakasilimu na wakaitakasa dini yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (ﷻ).
Miongoni mwao wapo ambao walikuwepo wanaoficha chuki zao na uadui dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) na Waislamu, isipokuwa walilazimika kudhihirisha mapenzi na usafi wa moyo kufuatana na mazingira yalivyo.
Kiongozi wa watu hawa alikuwa ni Abdullah bin Ubayy, kwani Ausi na Khazraji walikuwa wamekubaliana juu ya hadhi yake ndani ya jamii kuwa ni kiongozi wao, baada ya vita vya Buathi, kabla ya hapo hawakuwahi kukubaliana juu ya uongozi wa mtu yeyote. Lengo lilikuwa ni kumvisha taji na wamfanye kuwa ni Mfalme wa watu wa Madina. Ujio wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) ulivuruga mpango huu kwani watu wake walimwacha na kwenda kwa Mtume (ﷺ). Kwa hivyo, aliona kuwa Mtume (ﷺ) amemnyang’anya ufalme, na kwa sababu hiyo alikuwa akificha uadui mkubwa dhidi yake. Alipoona kuwa mazingira hayamsaidii juu ya shirki yake na kuwa yeye atazuiliwa na faida za kidunia, hivyo basi aliamua Kudhihirisha Uislamu wake na hilo lilifanyika baada ya vita vya Badri. Isipokuwa alibaki kuwa ni mwenye kuuficha ukafiri na alikuwa hapati nafasi ya kumfanyia vituko Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) na ‘Waislamu wengine. Waliobaki wakitenda vituko hivyo ni wafuasi wake miongoni mwa viongozi ambao walizujliwa na vyeo ambav’yo wangevipata katika ufalme wake — hawa walishirikiana naye na kumpa msaada katika kutekeleza mpango wake. Hawa waliwafanya baadhi ya watoto wadogo na wanyonge wa akili miongoni mwa Waislamu kuwa ni vibaraka wao katika kutekeleza mipango yao.
(3) Kundi la tatu ni Mayahudi. Kwa hakika wao walikimbilia Hijazi wakati walipokuwa wakiteswa na Al- Ashury na Warumi kama tulivyotangulia hilo, asili yao walikuwa ni Waebrania, lakini baada ya kukaa Hijazi, waliiga tabia na utamaduni wa Kiarabu katika mavazi, lugha, na maendeleo. Mpaka majina ya makabila yao, na ya watu wao yakageuzwa na kuwa ya Kiarabu. Hawa walioleana na Waarabu na kujenga mahusiano ya ukwe, hata hivyo waliendelea kuulinda udugu wao wa kikabila, hawakujiingiza moja kwa moja kwa Waarabu, waliendelea kujifakharisha kwa utaifa wao wa Kiyahudi. Waliwadhuru sana Waarabu na walikuwa’ wakiwaita Ummiyyina, yaani watu wasiojua kuandika wala kusoma na kuwa wao ni wanyama walio duni na wanyonge waliochelewa, walikuwa wanaona kuwa mali za Waarabu zimeruhusiwa kwao, ni halali kuzila kwa namna yoyote waitakayo:-
قَالُواْ لَيۡسَ عَلَيۡنَا فِي ٱلۡأُمِّيِّـۧنَ سَبِيلٞ وَيَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ
“Wakisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo Mwenyezi Mungu, hali nao wanajua.” (3: 75)
Mayahudi hawakuwa na hamasa yoyote katika kuieneza dini yao, ambayo kwa sehemu kubwa ni kutazamia kwa kupiga ramli, uchawi, kupuliza katika matabano na kutengeneza kinga na mambo mengine yanayofanana na hayo na kwa msingi huo walikuwa wanajiona kuwa wao ni watu walio na elimu na uongozi wa kiroho.
Walikuwa hodari katika fani za uchumi na maisha, walishika biashara ya chakula, nafaka, pombe na nguo. Halikadhalika walikuwa wanauza na kuagiza kutoka nje tende, nguo, chakula, pombe, na walikuwa wakifanya kazi nyingine zisizokuwa hizi ambazo walikuwa wakizifanya. Walikuwa wakichukua faida kutoka kwa Waarabu kwa kiwango kikubwa cha nyongeza na hawakutosheka na hayo, lakini wao ndiyo waliokuwa walaji wakubwa wa riba.
Wazee wa Kiarabu walikuwa wakikopeshwa mapesa na Wayahudi hawa ili wapate uwezo wa kuwalipa baadhi ya washairi wanaotunga mashairi ya kuwasifu kwa watu. Baada ya kutumia fedha hizo bila ya faida, hushindwa kuzilipa kwa wenyewe, kwa hivyo baada ya muda mrefu kupita Mayahudi huchukuwa mashamba yao kama fidia ya madeni yao.
Mayahudi walikuwa ni watu wa fitna, njama, kiburi na ufisadi. Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuingiza uadui na uhasama miongoni mwa makabila ya Kiarabu yaliyokuwa jirani nao na kusababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo kimsingi hata makabila hayo yalikuwa hayaelewi Chanzo chake. Kila moto huu wa vita ulipokuwa na dalili za kuzimika Mayahudi waliuwasha tena na kisha kukaa pembeni wakiangalia jinsi Waarabu wanavyouana hovyo. Kwa namna moja au nyingine mikopo ya riba ilikuwa inachochea vita kwa matumaini ya kupata ngawira ambayo labda ingewawezesha baadhi yao kulipa mikopo na riba kubwa zilizokuwa zikidaiwa na Mayahudi.
Kwa kitendo hiki walikuwa wakipata manufaa ya aina mbili; Kwanza walikuwa wanalinda hadhi ya kuwepo kwao kama Mayahudi na pili kwa njia hii walikuwa wakilifanya soko la riba lichangamke, ili waweze kuendelea kula riba nyingi zaidi, na kuongeza utajiri wao.
Yathrib kulikuwepo na makabila matatu yaliyokuwa mashuhuri :~
1) Banu Qainuqaa waliokuwa marafiki wa Al-Khazraji na majumba yao yalikuwamo ndani ya mji wa Madina.
2) Banu Nadhiri.
3). Banu Quraidha, Makabila haya mawili yalikuwa ni marafiki wa Al-Awsi na majmnba yao yalikuwa katika viunga vya Madina. Makabila haya ndiyo yaliyokuwa yakianzisha vita kati ya Al-Awsi na Al-Khazraji, toka muda mrefu sana na yalishiriki moja kwa moja Katika vita vya Buath, kila kabila moja pamoja na rafiki yake. Hata tukiangalia kitabia, kwa hakika mtu asingetegemea Mayahudi wautazame Uislamu isipokuwa kwa jicho la bughudha na chuki, kwani Mtume (ﷺ) hakuwa ni mmojé kutoka kafika Taifa lao, huu ni upande mmoja, upande wa pili ni kuwa Da’awa ya Uislamu ilikusudia mema ndani ya jamii haikuwa isipokuwa ni wito uliokusudia kuja kuuzima moto wa uadui na bughdha na kuunganisha nyoyo za waumini mb_alimbali. Kuhimiza watu washikamane na ibada ya Kumtii Mwenyezi Mungu (ﷻ), kuzingatia uaminifu katika mambo yote na katika kila hali kufuata yaliyo ya halali.
Bila shaka tunaona kuwa kwa mafimdisho ya Uislamu makabila ya Yathrib ya wakati huo yangeweza kuponyoka kutoka katika makucha ya Mayahudi na kwa hivyo harakati zao za kibiashara zingekufa na wao kuzuiliwa na mali za riba ambazo zilikuwa kiini cha uchumi wao.
Si hivyo tu Mayahudi walikuwa na hofu kuwa huenda makabila hayo yakazinduka na kuingiza katika hisabu yake mali za Ri’ba ambazo Mayahudi wamezichukua na hivyo kusimama kidete katika kurejesha
ardhi zao na mabustani yao, ambayo waliyapoteza kwa Mayahudi katika kulipa Riba.
Mayahudi walikuwa wakizingatia yote haya katika mikakati yao.
Walipoelewa kuwa kama Uislamu utazingatiwa utaleta utulivu Yathrib na kwa ajili hiyo wakawa wanaficha
uadui mkubwa dhidi ya Uislamu, na dhidi ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) toka alipoingia Yathri’b. Ijapokuwa hawakuwa majasiri kiasi cha kuweza kuudhihirisha uadui wao haraka, waliudhilhirisha baada ya muda mrefu kupita.
Jambo hili linadhihirishwa kutokana na yale yaliyopokelewa na Ibni Ishaq, kutoka kwa mama wa waumini
Swafiyya (Radhi za Alla ziwe juu yake ). Ibn Ishaq amesema, ”Nimesimuliwa kutoka kwa Swafiyya binfi Huyay bin Akhtab, kuwa; “Alipofika Madina Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) kwa Banu Amru bin Aufi, Quba, na kuelekea kwake wakati wa asubuhi, wakati huo baba yangu Huyay bin Akhtab, na ammi
yangu Abu Yasser bin Akhtab, walikuwa bado wamo katika kiza, “Hawakurejea mpaka jua lilipozama. Wakaja hali ya kuwa ni wachovu wakienda polepole, wakipepesuka Nikawaonesha furaha kama nilivyokuwa ninafanya, Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (ﷻ) hakuna mtu yeyote aliyenishughulikia katika wao. Pamoja na huzuni waliyokuwa nayo. Nikamsikia ammi yangu Aba Yasser akimwuliza,
Huyayy bin Akhtab, ”Ndiye yeye?.’ Naye akajibu, ‘Ndiyo; Hivi unamjua na unamthibitisha kuwa ni yeye’, akajibu, ‘Ndiyo. Akauliza tena, ’Nilipi lililo katika nafsi yako kuhusu mtu huyu?.’ Akajibu, ‘Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu nitaendelea kumfanyia uadui muda wa kuishi kwangu. (1)
Bukhari anayathibitisha haya katika mapokezi ya kusilimu kwa Abdullah bin Salam (Radhi za Alla ziwe juu yake) aliyekuwa mwanazuoni bingwa miongoni mwa wanazuoni wa Kiyahudi. Aliposikia kuwa
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) amefika Madina na yupo kwa Banu Al-Najjari, bila ya kuchelewa alimwendea na kumuhoji maswali ambayo kwa kawaida hayajui isipokuwa Mtume. Aliposikia majibu ya maswali aliyoyauliza, alimuamini wakati uleule na kisha’ akasema kumwambia,
“‘Kwa hakika Mayahudi ni wazushi wa mambo, watakapojuwa kusilimu kwangu kabla hujawauliza hadhi
yangu kwao, watanizulia jambo.” Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akawapeleka ujumbe na wakaja, baada ya kufika Abdullah bin Salam katika chumba, Mjumbe wa Mwenyezi (ﷺ) akawauliza; ”Ni nani kwenu Abdullah bin Salam?’ Wakajibu, “Ni Mbora wetu kielimu na mtoto wa msomi wetu.” Katika riwaya nyingine, “Ni kiongozi na mbora wetu na mtoto wa Kiongozi wetu.” Vilevile katika mapokezi mengine, ”Ni mwema wetu na mbora wetu na mtoto wa aliyekuwa mbora wetu.” Mjumbe wa Mwenyezi Mungu
(ﷺ) akauliza; “]e, mnaonaje iwapo Abdullah ataingia katika Uislamu?” Wakasema; ”Tumaomba Mwenyezi Mungu amkinge na jambo hilo”, na walirudia maneno hayo mara mbili au tatu hivi.
Abdullah akawatokea na kusema; ”Ninashuhudia kuwa hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa
haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ).” Waliposikia hivyo wakabadili maneno na wakamsingizia kila jambo ovu, na katika tamkojengine;Alisema, “Enyi Mayahudi mlio jamaa zangu, Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu
Ambaye hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye;’ Kwa hakika nyinyi mnafahamu kuwa yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) na kuwa yeye amekuja na ukweli.” Wakamwambia, ”Umesema urongo (2)
Haya ndiyo majaribio ya kwanza ambayo Mjumbe wa Mwenyezi Mtmgu (ﷺ) alikutana- nayo kutoka kwa
Mayahudi katika siku yake ya kwanza kuingia Madina.
Haya yote yanahusu hali ya mambo ilivyokuwa ndani ya Madina. Ama kuhusu mambo ya nje uadui mkubwa uliokuwa dhidi ya Uislamu ni Makuraishi.
Hili ni kwa sababu kwa kipindi cha miaka kumi, wakati Waislamu walipokuwa chini ya mikono yao, walikuwa wamejaribu mbinu mbalimbali za kigaidi na kutisha, waliwakandamiza kwa kuwawekea
vikwazo. Waliwatesa, waliwaadhibu kwa njia mbalimbali na kuendeleza vita vya kisaikolojia vyenye kudhalilisha; kisha walipohama Waislamu kuelekea Madina walizichukua ardhi walizokuwa wakimiliki na majumba yao na mali zao nyingine na wake zao na watoto wao walitiwa kizuizin Si hivyo tu,
lakini yule ambaye walimuweza walimfunga na kumuadhibu na hawakutosheka na mambo hayo tu, lakini mwishowe walifanya njama za kutaka kumvamia Mtume (ﷺ) na kumaliza, yeye na Da’awa yake.
Hata baada ya Mtume (ﷺ) kuhama bado hawakupuguza juhudi zao katika kuzitekeleza njama hizo.
Baada ya Waislamu kujiokoa kwa kuhamia kwenye ardhi iliyoko mbali nao kwa kiasi cha kilometa mia tano. Makuraish walisimama kwa nafasi yao ya kisiasa, na uongozi wa waliokuwa nao katika jamii za Waarabu, kutokana na sifa yao ya kuwa ni wakazi wa Al-Haram na kukaa karibu na nyumba
ya Mwenyezi Mungu na kuitumikia, waliwashawishi Waarabu wengine kutoshirikiana na watu wa Madina mpaka Madina ikatengwa.
Uagizaji bidhaa kutoka nje ulipungua sana, wakati idadi ya wakazi wa mji wake ilikuwa inaongezeka siku hadi siku. Hali hii ya uhasama iliendelezwa na watu wa Makkah dhidi ya Waislamu katika nchi yao mpya,
itakuwa ni katika upumbavu kuwabebesha Waislamu mizigo ya uhasama huu. (3)
llikuwa ni haki kwa Waislamu kuzizuia mali za hawa waovu kama zilivyozuiwa mali zao, na kuwafanyia vitendo ambavyo vingekuwa ni fundisho kwa waovu wengine, kama ambavyo wao waliwafanyia Waislamu katika kuonesha uadui wao. Ilikuwa ni haki kuwawekea katika njia ya maisha yao vikwazo, kama vile ambavyo wao waliviweka katika njia ya maisha ya Waislamu, na kwamba walipiziwe kisasi mpaka
wasipate njia yoyote ya kuwateketeza Waislamu, na kuung’oa ustawi wao.
Hay; ndiyo masuala na _matalizo ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alikuwa akikabiliana nayo wakati alipofika Madina kwa sifa yake ya kuwa Mtume mwenye kuongoza na Imamu aliye Jemedari.
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alichukua jukumu la Utume na uongozi alipokuwa Madina. Alimpa kila mtu stahiki yake; ama huruma au adhabu — na hapana shaka kuwa huruma yake ilikuwa imeshinda adhabu. (Mpaka katika miaka michache mambo yakarejea kwenye Uislamu na watu
wakaishi kwa ustawi wa hali ya juu, na msomaji atayakuta yote hayo yakiwa wazi katika kurasa zifuatazo)