SOMO LA FIQHI
Tukiyaangalia maji kwa kuuzingatia wingi na uchache wake tutayakuta yamegawanyika sehemu/mafungu mawili:-
1. Maji mengi, na
2. Maji machache
MAJI MENGI: Haya kwa mtazamo wa sheria ni yale yaliyofikia Qullatein na zaidi yake.
Qullatein ni miongoni mwa vipimo vilivyokuwa vikitumiwa na Waarabu zamani. Kwa vipimo tuvitumiavyo leo Qullatein ni sawa na lita 216 za ujazo.
Kwa vipimo vya ukubwa Kullatein ni sawa na dhiraa moja na robo upana, urefu na kina. Dhiraa moja ni sawa sawa na sentimeta 48 (48 cm)
HUKUMU YA MAJI MENGI
Maji yaliyofikia Qullatein na kuendelea hayanajisiki kwa kuingia tu najisi ndani yake bali ya kuwa yamenajisika ikiwa najisi hiyo itaharibu mojawapo ya zile sifa tatu za maji.Kwa hadithi ya bwana Mtume ﷺ:
[إذَا كَانَ الْمَاءُ قُلَّتَيْنِ لَمْ ، يَحْمِلْ الْخَبَثَ] رواه أحمد إبن ماجة وغيرهما
[Maji ya kifikia Qullatein haya bebi Uchafu] [Imepokewa na Ibnu Majah na Ahmad]
Kwa Mafhumu ya hadithi hii inamanisha Maji ya kiwa ni chini ya Qullatein yanabeba Uchafu.
MAJI MACHACHE
Maji yatahukumiwa kuwa ni machache ikiwa hayakufikia kiwango cha kullatein yaani yako chini ya lita 216 za ujazo ambazo ni karibu ya madebe 12 yaliyojaa.
HUKUMU YA MAJI MACHACHE
Maji haya yatanajisika kwa kuingiwa na najisi hata kama najisi hiyo haikuharibu mojawapo ya sifa za maji, na yatahukumiwa kwa mujibu wa sheria kuwa ni maji najisi.
KUMBUKA
Msimamo huu ni kulengana na Madh’habu ya Imamu Shafi na Imam Ahmad Mungu awerehemu,ama Imam Malik na wengineo wamesema hakuna tafauti ya Maji mengi na mai kidogo,na wakasema Maji hayanajisiki mpaka ya badilike moja katika sifa zake Rangi yake au harufu yake au ladha yake,sawa ya kiwa ni Maji mengi au maji kidogo.Na huu ndio msimamo wa Sheikhul-Islam Ibnu Taymiyah Mungu amrehemu.