June 17, 2021
0 Comments
KUZALIWA KWAKE, KUKUA KWAKE
Jina lake ni ‘Uthman ibn ‘Affan ibn Abi-AI-‘As ibn Umayyah ibn ‘Abdush-Shams ibn ‘Abdu Manafi AI-Qurayshy.
Jina la mama yake ni Arwa bint Al-Baydha’ bint ‘Abdul-Mut’Talib babu yake Mtume ﷺ.
‘Uthman (r.a.) alizaliwa Taif baada ya kuzaliwa Mtume ﷺ kwa miaka mitano.
Baba yake alikuwa mmojawapo wa wafanyi biashara maarufu wa Kiquraishi, alifariki baba akiwa katika msafara wa biashara akielekea Shamu. ‘Uthman (r.a.) alimrithi baba yake, yakazidi mali yake, na ikakua biashara yake kila zama. Alikuwa ni miongoni mwa watu maarufu wa Kiquraishi. Alisifika ‘Uthman kwa tabia njema na ukarimu, alikuwa mwenye kupendwa na watu.