١٦٤- باب فضل من مات لَهُ أولاد صغار
وعن أَبي سعيدٍ الخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: جَاءَتِ امرأَةٌ إِلى رَسُولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ ذَهَبَ الرِّجالُ بحَديثِكَ، فاجْعَلْ لَنَا مِنْ نَفْسِكَ يَوْماً نَأْتيكَ فيهِ تُعَلِّمُنَا مِمَّا عَلَّمَكَ اللَّه، قَالَ: ” اجْتَمِعْنَ يَوْمَ كَذَا وَكَذَا”فَاجْتَمَعْنَ، فَأَتَاهُنَّ النبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَعَلَّمَهنَّ مِمَّا علَّمهُ اللَّه، ثُمَّ قَالَ:”مَا مِنْكُنَّ مِن امْرَأَةٍ تُقَدِّمُ ثَلاثةً منَ الوَلَدِ إِلاَّ كانُوا لهَا حِجَاباً منَ النَّار”فَقالتِ امْرَأَةٌ: وَاثنينِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم“وَاثْنَيْن ” متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
164. MLANGO WA FADHILA ZA ALIYEFIWA NA WATOTO WADOGO
Imepokewa kutoka kwa Abû Sa‘îd al-Khudry ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Mwanamke mmoja alimjia Mtume ﷺ akamwambia: “Yâ Rasûlallâh, wanaume wameyachukua maneno yako, basi tutengee siku tukujie ili utufundishe yale Aliyokufundisha Allâh.” Mtume ﷺ akamwambia: “Kusanyikeni siku kadha na kadha.” Wakakusanyika. Mtume ﷺ akawaendea, akawafundisha yale aliyofundishwa na Allâh, kisha akamwambia: “Mwanamke yeyote miongoni mwenu anayefiwa na watoto watatu, watakuwa ni kinga yake ya moto.” Mwanamke mmoja akauliza: “Je, na watoto wawili?” Mtume ﷺ akajibu: “Na watoto wawili (pia).” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].