0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

927. Riyadhu Swalihina Mlango wa kufaa kumlilia Maiti na uharamu wa kuomboleza

 باب جواز البكاء عَلَى الميت بغير ندب وَلاَ نياحة أمَّا النِّيَاحَةُ فَحَرَامٌ


وعن أَنسٍ رضيَ اللَّهُ عنه أَنَّ رسُولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم دَخَلَ عَلى ابْنه إِبَراهِيمَ رضيَ اللَّهُ عنْه وَهُوَ يَجودُ بَنفسِه فَجعلتْ عَيْنا رسولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم تَذْرِفَانِ. فقال له عبدُ الرَّحمن بنُ عوفٍ: وأَنت يَا رسولَ اللَّه؟، فَقَالَ:”يَا ابْنَ عوْفٍ إِنَّها رَحْمةٌ” ثُمَّ أَتْبَعَها بأُخْرَى، فقال صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “إِنَّ الْعَيْنَ تَدْمَعُ والقَلْب يَحْزَنُ، وَلا نَقُولُ إِلا ما يُرضي رَبَّنا وَإِنَّا بفِرَاقِكَ يَا إِبْرَاهيمُ لمَحْزُونُونَ”         رواه البخاري، وروى مُسلمٌ بعضَه


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



153 – MLANGO WA KUFAA KUMLILIA MAITI NA UHARAMU WA KUOMBOLEZA


Imepokewa na Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa Mtume aliingia kwa mwanaye Ibrâhîm (Radhi za Allah ziwe juu yake) naye anatoa pumzi zake za mwisho, macho ya Mtume yakawa yanadondoka machozi. ‘Abdurrahmân bin ‘Awf akamwambia: “Hata nawe Yâ Rasûlallâh!” Akasema: “Ewe Ibni ‘Awf, hii ni rehema.” Kisha akafwatisha chozi jingine, akasema: “Hakika jicho linatoa chozi na moyo unahuzunika, wala hatusemi ila linalomridhisha Mola wetu. Ee Ibrâhîm, hakika sisi tunahuzunika kwa kukukosa wewe!”        [ Imepokewa na Bukhârî.]


Begin typing your search above and press return to search.