باب استحباب تكثير المصلين عَلَى الجنازة وجعل صفوفهم ثلاثة فأكثر
وعن مَرْثَدِ بن عبدِ اللَّه اليَزَنِيِّ قَالَ: كانَ مالكُ بنُ هُبَيْرَةَ رضي اللَّه عنه إِذا صلَّى عَلى الجنَازَةِ، فَتَقَالَّ النَّاسَ عَليها، جزَّأَهُمْ عَلَيْهَا ثَلاثَةَ أَجْزَاءٍ ثُمَّ قَالَ: قالَ رَسُولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “مَنْ صَلَّى عليهِ ثَلاثَةُ صُفُوف، فَقَدْ أَوْجَبَ”. رواه أَبُو داود، والترمذي وقال: حديث حسن
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
156. MLANGO WA SUNNAH YA WANAOSWALIA JENEZA KUWA WENGI NA SAFU ZAO KUZIFANYA ZIWE TATU NA KUENDELEA
Imepokewa na Marthad bin ‘Abdullâh al-Yazany amesimulia: “Mâlik bin Hubairah (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa anapotaka kuswalia jeneza na akaona watu kuwa ni wachache, huwapanga safu tatu, na husema: “Mtume ﷺ amesema: “Anayeswaliwa na safu tatu, ameshapasa kuingia Peponi.” [ Imepokea na Abû Dâwûd na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]