0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

922. Riyadhu Swalihina Mlango wa yanayosemwa kwa maiti na anayosema mtu aliefiwa

باب ما يقال عند الميت وَمَا يقوله من مات له ميت


وعن أَبي موسى رضي اللَّه عنه أَنَّ رسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ: “إِذا ماتَ وَلدُ العبْدِ قَالَ اللَّهُ تَعَالَى لملائِكَتِهِ: قَبضْتُم وَلدَ عَبْدِي؟ فيقولُونَ: نعَم، فيقولُ: قَبَضتُم ثمَرَةَ فُؤَادِهِ؟ فيقولونَ: نَعم. فَيَقُولُ: فَمَاذَا قَالَ عبْدِي؟ فيقُولُونَ: حمِدكَ واسْتَرْجعَ، فيقولُ اللَّهُ تَعَالَى: ابْنُوا لعبدِي بَيتاً في الجَنَّة، وَسَمُّوهُ بيتَ الحمدِ ”       رواه الترمذي وقال: حديث حسن


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



152. MLANGO WA YANAYOSEMWA KWA MAITI NA ANAYOSEMA MTU ALIEFIWA


Imepokewwa na Abû Mûsâ (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ amesema: “Anapofariki mtoto wa mja, Allâh Huwauliza Malaika Wake: “Mmemchukua mtoto wa mja Wangu?” Nao hujibu: “Ndio.” Huwauliza: “Mmelichukua tunda la moyo wake?” Wao hujibu: “Ndio.” Huwauliza: “Mja Wangu amesema nini?” Wao hujibu: “Amekuhimidi (amekushukuru) na amesema Innâ lillâhi wa innâ ilaihi râji‘ûn, [Sisi ni wa Allâh na Kwake tutarejea_, basi hapo Allâh Huwaambia: “Mjengeeni nyumba mja Wangu Peponi, na muiyite Baytul-Hamd “Nyumba ya Shukrani.”    [ Imepokewa na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]


Begin typing your search above and press return to search.