AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Inawezekana kukigawa kipindi cha maisha ya Mtume (ﷺ) akiwa Madina katika awamu tatu: .
1. Awamu iliyojaa kero mbalimbali, fitna, na vikwazo kutoka ndani na kutoka nje ya Madina, vilivyokuja kwa lengo la kuung’oa ubichi (wa utawala wake madina) kwa nje. Awamu hii inakomea katika mkataba wa Hudaibiya uliofanyika Dhul Qa’da, mnamo mwaka wa sita. toka kuhamia Madina.
2. Awamu ya mkataba na uongozi wa Mushirikina. Awamu hii inaishia pale Fathu Makka, mwezi yva Ramadhani mwaka wa nane toka kuhama. Wakati huo ndio ulikuwa wakati wa kuwalingania wafalme kwenye Uislamu.
3. Awamu ya kuingia watu katika Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) makundi kwa makundi, na hiyo ilikuwa ni tija ya kufika kwa makabila na mataifa mbali mbali Madina. Awamu hii inaendelea hacli kifo cha Mtume Muhammad (ﷺ) katika mwezi wa Rabbiul ‘AwwaI mwaka wa kumi na moja toka kuhamia Madina.